Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Tunduma, Lowassa alisema kwa vile serikali iliyopo madarakani imechaguliwa kwa kura nyingi, ndiyo maana hawalali usiku na mchana kuhakikisha wanatimiza ahadi zote wazozitoa wakati wakiomba kura.
Lowassa: Tusipotekeleza ahadi zetu mtunyonge 2010
Shedrack Sagati
WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amesema iwapo serikali haitatekeleza ahadi walizoainisha ndani ya Ilani ya CCM, basi wananchi wawanyonge katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Tunduma, Lowassa alisema kwa vile serikali iliyopo madarakani imechaguliwa kwa kura nyingi, ndiyo maana hawalali usiku na mchana kuhakikisha wanatimiza ahadi zote wazozitoa wakati wakiomba kura.
Lowassa alitoa ahadi hiyo baada ya kuulizwa kero mbalimbali za maji pamoja na ahadi za ujenzi wa barabara ya Tunduma kwenda Sumbawanga.
Alisema barabara hiyo itawekewa lami ndani ya kipindi cha miaka mitano, kauli ambayo wananchi hawakuridhika nayo, lakini akawahakikishia kwa kueleza, jamani yaani mnataka sisi tukisema tu leo na kesho ianze kuwekwa lami, haiwezekani ndugu zangu, lakini mtuamini kuwa tutaijenga barabara hii kwa kiwango cha lami.
Waziri Mkuu alisema serikali iko makini kutekeleza ahadi zake na ikifika mwaka 2010 watakuwa wametekeleza kile walichoahidi. Ikifika 2010 bila maji msiichague CCM; lakini nawahakikishia kuwa tutatekeleza ahadi zote, alisema Waziri Mkuu.
Kuhusu maji ambayo ni moja ya kero kubwa zinazowasumbua wananchi wa eneo hilo, aliwahakikishia wananchi hao kutohofu kwani kuna miradi kadhaa ambayo imetengewa fedha ambayo itatekelezwa katika Wilaya ya Mbozi.
Awali Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge aliwaambia wananchi hao kuwa moja ya ahadi za serikali ni kuijenga barabara hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa inalalamikiwa na wananchi.
Hili tutalifanya kwani limo kwenye ilani yetu, alisema Chenge ambaye amefuatana na waziri mkuu na amekuwa anajibu maswali yote yanayoulizwa na wananchi juu ya kero za barabara.
Source: HabariLeo
Na kuondoa ufisadi iko kwenye ilani?
kwani wewe ufisadi unafahamu vipi?
nnaona kama hiyo ilni kuna mtu naweza kutuletea hapa ni bora iletwe mie nnayo hardcopy na kuiscan itakuwa shughuli.
ila kila asubuhi huipita, baada ya kunywa chai na kusoma Quraan, huvuta ilani ya chama na kuangalia ni vipi tumeweza kuleta maendeleo ktk jamii.
tunajitahidi na serikali ya JK kwa kweli inapiga hatua nzuri, mapungufu ya kibinaadamu hayakosi.
na ahadi iko wazi tukishindwa 2010 msitupe tena nchi wapeni kina Mrema si basi
dawa ni kuwang'oa tuu CCM la sivyo hakuna chochote njaa itakuwa mbele kwa mbele tuu
Koba mimi bado nina wasiwasi, nakubaliana sana na wewe kuwa CCM ni mzizi wa matatizo yetu, lakini swali linakuja solution iko wapi? Aondolewe CCM aingie nani? Huyo atakayeingia atakuwaje, amejiandaa kiasi gani kushika dola? These are troubling questions to me.
Tulisema sana kuwa tunataka serikali isiwe ya wazee kama kina Kingunge, tulisema wengi tunakata vijana, na ndiyo maana Kikwete kwa kutumia vazi la ujana(ingawa yeye si Kijana) alipata hizo asilimia 80 ya kura zilizopigwa, ona sasa anavyotupiga bao, sasa hivi tunaona nchi inaelekea kuwa kama ya Mwinyi, uozo tu.
Labda na sisi tungeonja utawala wa kifalme.
Koba mimi bado nina wasiwasi, nakubaliana sana na wewe kuwa CCM ni mzizi wa matatizo yetu, lakini swali linakuja solution iko wapi? Aondolewe CCM aingie nani?
Huyo atakayeingia atakuwaje, amejiandaa kiasi gani kushika dola? These are troubling questions to me.
Tulisema sana kuwa tunataka serikali isiwe ya wazee kama kina Kingunge, tulisema wengi tunakata vijana, na ndiyo maana Kikwete kwa kutumia vazi la ujana(ingawa yeye si Kijana) alipata hizo asilimia 80 ya kura zilizopigwa, ona sasa anavyotupiga bao, sasa hivi tunaona nchi inaelekea kuwa kama ya Mwinyi, uozo tu.
Labda na sisi tungeonja utawala wa kifalme.
Mbowe, Mnyika, Maalim, Mtikila, Cheyo na Zimbwe wasilianeni nami kibinafsi niwauzie mkakati!