The Radar Scandal: Investigation & Progress

Hongera Mkjj, huyo Chenge anajibu kwa kiburi ila haitamsaidia kitu mambo yako hadharani na yatamnyima usingizi kwa sana! Whether anarudi ahera au anarudi Tz sheria ichukue mkondo wake.Pesa za wizi zina kiburi sana huu ni ushahidi tosha!
 
Brazameni yuko wapi atupe commercial break.....

HAYA TENA TIME FOR COMMERCIAL BREAK...MMEZIDI UBISHI

2qu2ply.jpg
 
Sikia, tukubaliane tuwe tofauti, ila usining'ang'anize unachoamini wewe, wala kuniambia niteme mate chini na imani zako hizo. NIMEMSOA biography ya Steve Biko (I was 13), nimesoma Biography ya Mandela (iliniboa). Naheshimu Mandela kukaa miaka yote hiyo jela. Lakini pia katoka jela haelewi dunia inaenda vipi. Ndio huyo huyo hero wake hakuamini aendeshwe na rubani mweusi....hero wako huyo. Naheshimu sacrifice aliyopitia kukomboa South Africa.

Mandela hajaongoza SA, kaongozwa. He was symbolic with no clue of what was going on. Sio kwamba sio intelligent, ni kwamba, kutojua kwakwe na vijana wake, na ushamba wao wa power, ndio kimewafanya south africa wawe wachovu mpaka leo hii. Wanatia aibu kwa waafrika. Yeye na timu yake wamezidi kuonyesha kwamba bila ya mzungu waafrika hatuwezi kujiendeleza. Walivyochezewa huko kwao, ndio wanatuletea hao makaburu watuchezee kwetu.

On that note, ndio maana nasema, naweza jifunza zaidi kuhusu ulimwengu, nikikaa na Chenge kuliko nikikaa na Mandela (miaka 27 ndani sio mchezo hata uwe na akili gani). Thats my belief, its not disrespecting, that is what I believe. Kama wazungu wamekupa propaganda umwabudu Mandela hiyo juu yako!!

Sijaongelea MLK na Malcolm X.

Umesoma biography ya Biko ukiwa na miaka 13? Hongera sana. Nilimsoma Fanon nikiwa na umri huo huo na sikumwelewa hadi nilipomsoma tena nilipokuwa mtu mzima.

MLK= Mandela kabla ya Umkhonto we Sizwe, Malcolm= Steve Biko.

Ndiyo maana nilikuuliza ulimsoma KWELI ukamuelewa?

Najua hii inayofuata iko nje ya mada, lakini nivumilie! With all due respect,ulitaka Madiba afanye nini wakati alipokuwa rais? Kumbuka haikuwa tuu makaburu waliokuwa tumbo moto bali a virtual civil war kati ya ANC na wakina Buthelezi ilikuwa inaendelea kwenye townships! Huyu amabe pamoja na ushindi wa tsunami aliwakaribisha wazulu na wengine kwenye serikali yake? Huyu ambae pamoja na kupendwa (naam bado anapendwa) aliachia ngazi kwa hiari yake?

Ile nchi ina wazungu ambao ni raia kama alivyokuwa yeye. Ulitaka awafukuze ili athibitishe kuwa sisi waafrika tunaweza bila wao? Au ulitaka awagawie mashamba na maghorofa yote wale walioko Alexandria na Soweto? Angekua kama Mugabe ndiyo ungemuona true revolutionary? Potelea mbali watu wanakufa njaa lakini uchumi uko mikononi mwa waafrika weusi wenzetu!

Basi iko kazi! Kwa mtazamo huo, naona kweli utajifunza mengi kutoka kwa Chenge kuliko kwa Madiba!

Kwa vile naona tumeelewana tunatokea wapi, basi mimi nakaa pembeni.
 
Mimi nimekwambia sijacompare MLK na Malcolm X.

The brain behind the leadership even during Mandela's time was Mbeki!! Na Zuma kamshinda Mbeki kwasababu watu watakaomchagua Zuma wanafikiri atatatua matatizo yao, wakati hata Zuma mwenyewe anaelewa waliochemsha ni Mandela, Mbeki and crew! Mandela alikuwepo pale symbolic tu. Aliaachia ngazi kwasababu alikuwa hana nyimbo wala upeo wa kuongoza modern economy. Aliongoza kipindi cha kwanza kwa heshima tu.

Mambo yote uliyoweka thread ya kwanza kuhusu jamaa, nothing special, hata mimi sijasoma form 1. Alikubali atoke jela kwa masharti, ingawa kuna quotation alitoa mtoto wake anasema otherwise......Maaan please.

Kwavile humpendi Chenge, labda nikupe mfano mwingine. Nitajifunza zaidi nikikaa na Attorney General wa South Africa provided kakaa muda mrefu kama Chenge, kuliko nikiongea na Mandela. Mandela namwona kama babu yangu. A wise old man.

People are willing to point at weaknesses of great men like Nyerere, lakini hamtaki Mandela akosolewe? Pleease!

naenda kulala. gnite mate. nothing personal, just difference of opinion.
 
Nzoka,
Chenge alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa miaka mingapi?

hiiiiiii...kumbe hili liNzoka nalo lisomi la mavitabu!!!!..... lol

.........shhhhhhhhhhhi...mwache bana, utamkamatisha bure.....

hahaaa, hamna adabu nyie.
State Attorney from 70s, first post on thread inasema State Attorney. AG kipindi cha Mkapa. Jinsi usingizi unavyozidi, msinitege.

Message sent!
 
Mimi nimekwambia sijacompare MLK na Malcolm X.

The brain behind the leadership even during Mandela's time was Mbeki!! Na Zuma kamshinda Mbeki kwasababu watu watakaomchagua Zuma wanafikiri atatatua matatizo yao, wakati hata Zuma mwenyewe anaelewa waliochemsha ni Mandela, Mbeki and crew! Mandela alikuwepo pale symbolic tu. Aliaachia ngazi kwasababu alikuwa hana nyimbo wala upeo wa kuongoza modern economy. Aliongoza kipindi cha kwanza kwa heshima tu.

Nimekutolea mfano wa MLK na Malcolm kwa vile uliwafananisha madiba na Steve Biko!

Yaani kweli unaamini kuwa Madiba alikuwa mwanasesere tu! Unadhani the biggest challenge walioi'face' South Afrika wakati ule ilikuwa ni uchumi tu? Kweli hamridhiki.Mnapata kiongozi anayekubali kuongoza wakati ambao ni mgumu na kuachia ngazi wakati bado anapendwa leo mnamgeuka na kusema alikuwa figure head tu! Mnapopata know-all despots kama wakina Mugabe ndiyo mnawaona werevu! Iko kazi, kizazi cha kesho.

Kwavile humpendi Chenge, labda nikupe mfano mwingine. Nitajifunza zaidi nikikaa na Attorney General wa South Africa provided kakaa muda mrefu kama Chenge, kuliko nikiongea na Mandela. Mandela namwona kama babu yangu. A wise old man.

People are willing to point at weaknesses of great men like Nyerere, lakini hamtaki Mandela akosolewe? Pleease!

Hii sasa inakuwa tedious!

Asiyempenda Chenge nani? I only took offence ulipomlinganisha na Mandela, that's all.

Zaidi ya kusema kuwa Mandela anakuboa haujatoa criticism yeyote dhidi yake bali myths kama alikuwa akitumiwa na wazungu,na hii ya kuwa Mbeki alikuwa anaendesha nchi! Lord have mercy, huyu bwana alimwachia Buthelezi nchi itakuwa Mbeki! Atakuwaje wise wakati unaona hakuna unachoweza kujifunza kutoka kwake?

Madiba ana matatizo yake. Kwa mfano, aliufumbia macho ugonjwa wa Aids wakati wake. Siwezi kukana hilo. lakini aliacha nchi yenye amani ambayo ingeweza kukumbwa na machafuko makubwa! Hili sio dogo hata kidogo hasa katika mazingira yetu ya Afrika.

For your information, hata ungemfananisha Chenge na Nyerere, nisingekuelewa. Una over-reach katika kujaribu kumtetea Mheshimiwa. Aliyoyafanya ni makubwa lakini there is no way unaweza kumlinganisha na Madiba. Ulikuwa disrespectful, that's all!

Enough said!
 
...Madiba ana matatizo yake... lakini aliacha nchi yenye amani ambayo ingeweza kukumbwa na machafuko makubwa! Hili sio dogo hata kidogo hasa katika mazingira yetu ya Afrika.

Fundi, heshima mbele.

Mimi huwa natatizwa sana tukimpa mtu sifa kwa jambo ambalo anategemewa alifanye. Tukisema sasa siku hizi kuto kupigana vita ndio mafanikio ya Afrika tunakuwa tumeshusha sana viwango. Kwa hiyo sidhani kama Mandela inabidi asifiwe kwa hilo.

Vinginevyo inabidi tumtuze Mkapa, Mwinyi na Kikwete kwa mafanikio makubwa Tanzania kwa sababu wali iepusha nchi na vita. Ahsante.
 
Hiyo jeuri haitamsaidia kabisa kwenye court of public opinion....(not to say that it matters...but in a way it does)
 
Kwa hapwa JF ile sosi ya habari hii inabidi sasa iane kutiliwa shaka ,au kwa inavyoonekana ulaji umeanza kuwafikia wadau wa habari nyeti hapa jungu kuu yaaani sasa badala ya ukoko wanaleta na matandu.
 
Fundi, heshima mbele.

Mimi huwa natatizwa sana tukimpa mtu sifa kwa jambo ambalo anategemewa alifanye. Tukisema sasa siku hizi kuto kupigana vita ndio mafanikio ya Afrika tunakuwa tumeshusha sana viwango. Kwa hiyo sidhani kama Mandela inabidi asifiwe kwa hilo.

Vinginevyo inabidi tumtuze Mkapa, Mwinyi na Kikwete kwa mafanikio makubwa Tanzania kwa sababu wali iepusha nchi na vita. Ahsante.

Hapana Mkuu! Hauwezi kulinganisha hata siku moja hali iliyojiri Tanzania na ile iliyokuwa Afrika Kusini. Hatujawahi sisi kuwa na utawala dhalimu kama wa makaburu. Mandela angeweza kuamua kulipiza kisasi na wengi wetu tungemuelewa. Sijui kama unakumba lakini mapigano na mauaji baina ya wafuasi wa ANC na wale wa chama cha Chief Buthelezi yaliishaanza. Watu walikuwa wanuana ovyo kwenye hostels. Si hizi ngonjera zetu za kila siku, kule chuki na fujo viliishaanza. Ni yeye aliyeweza kuzima kwa kumkaribisha Buthelezi na kumfanya makamu wa rais ingawa ANC ilishinda uchaguzi kwa kishindo. Ilifika hata kuna wakati alisafiri na kumuachia Buthelezi nchi! Ni kiongozi gani wa kiafrika angeweza kufanya hivyo? Sisi hapa tunapata kigugumizi kukabili matatizo ya Zanziba ambako wote tunajua CUF wanakubalika na sehemu kubwa ya jamii? Makaburu waliishaanzisha kasehemu kao mpaka hapo Mandela alipowafuata kuongea na mjane wa nadhani Vorster! Hawa waliomfunga kwa miaka 27! Nani katika viongozi wetu angeweza kufanya hivyo? Nchi ilikuwa imegawanyika imewagawanyika katika michezo ( na kuna ushabiki gani unaoshinda wa kwenye michezo, pengine wa dini) akawaunganisha wakati wa mashindano ya dunia ya Rugby. Huyu bwana aliitwa kama shahidi (akiwa rais) mahakamani akaenda na kukubali kuapishwa kama raia mwingine. Huyu ndiye aliyeanzisha the Truth and Reconciliation Commission kujaribu ku'heal' jamii ya watu wake badala ya kukimbila kwenye visasi. Sasa hivi nchi nyingi zinaiga mfano huu. Na zaidi ya yote, baada ya term moja akaamua kuachia ngazi! Ana matatizo yake kama binadamu wengine lakini hatuwezi hata siku moja kumfananisha na hawa wa kwetu. Yeye na huyo mwengine ambaye hawa arm chair revolutionaries wana gall ya kumuita kibaraka, Archbishop Tutu, ni watu ambao mimi kama mwafrika wananihakikishia kuwa SIVYO TULIVYO.

Amandla!
 
Siri ya mabilioni ya Chenge Jersey

“Ni kweli amelazimika (Chenge) kutuma ujumbe maalumu kwenda Finland ili kumuomba ...aliyeziweka fedha zile katika ile akaunti awe tayari kujitokeza na kueleza sababu ya kuziingiza na malengo yake. Mjumbe anasubiriwa kwa hamu Dar kwani bado hajarudi,” alisema mtoa habari huyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.

“Ni kweli kuna mtu mmoja mzito (anamtaja kwa wadhifa), ametumwa huko nje kwa kazi hiyo ya kuonana na mwenzake anayehusishwa na fedha hizo...mkitaka taarifa zaidi mtafuteni Chenge mwenyewe au mwanasheria wake,” alisema mwanasiasa huyo.

Mh! kweli dunia ni mduara, tuliyoyashuhudia miaka ya '84 ya watu kuzikana pesa zao yameanza tena kujitokeza! ama kweli mzimu wa Sokoine bado unafanyakazi. kweli mtu unatuma ujumbe kwenda kumbembeleza mtu iliakubali kutolea maelezo pesa ambazo ziko kwenye akaunti yako!!???.

Naomba Mungu huyu Mjumbe arudi na jibu bovu kuwa jamaa amekataa kuzitolea maelezo, kisha waniite mimi ama wabandike matangazo sehemu mbalimbali kutafuta mtu mwenye sifa ya kuweza kutolea maelezo zile pesa ajitokeze ili ziwe zake!

Naombeni jamani, huyo mjumbe atakaporudi tujulisheni kaja na jibu gani! Kwani unaweza kujikuta unaanza kuimba zile nyimbo zetu za wakati huo;

Shilingi ya Nyerere katikati kuna mwenge!..dolly dolly, dolly Samora!
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!!

Baada ya kukaa na kutafakari, na kuangalia kisomo cha Chenge, na kwavile kapitia Havard Law school, na pia amekuwa kama State Attorney kwa zaidi ya miaka 30, basi naona kwa kweli kutengeneza hivyo vijisenti ni kitu kidogo sana kwake.

All he needs to have done is a number of consulting jobs or presentations either at Havard itself or other institutions in different parts of the world. For him to be a State Attorney for that long, he has a wealth of information to share to the world.
Clinton analipwa kama £75,000 per lecture. Cherie Blair £30,000. As far as I am concerned someone like Chenge would have been highly regarded due to his position and his education. Even if he got paid £5,000 per lecture, calculate that maybe 5 to 10 lectures/presentation per year, over a stretch of 20years, plus smart investment in property (say UK).

On this logic (and this logic only) I am not surprised he could have that couple million 'vijisenti' in Jersey.

Naona unaweka mkazo kweli kweli kwenye Havard wakati jamaa ameshindwa hata kutengeneza contracts za maana kwa ajili ya mwajiri wake ambaye ni serikali ya TZ?

Mambo yale yale ya kufikiri kwasababu kasoma Havard university basi ana uwezo mkubwa.

Kama ana uwezo mbona hata hizo contracts zimechoka ile mbaya?
 
Hivi kama contract kachemsha hivyo, waTanzania wanasubiri nini kuzibadilisha sasa? All you do is complain and complain, kama uchungu wa nchi upo, nini kinawazuia hayo mabadiliko?
 
Back
Top Bottom