The Radar Scandal: Investigation & Progress

Niliposema wampe Balali Kinga watu walidhani miye nimechanganyikiwa; hili ndilo linapaswa, wakimpa kinga yatakayotoka huko makubwa. Wazungu wanajua kukamatana bwana.. (hapa najihisi niko kama Raj)
 
Nataka ukiranja Je nitaupataje ????

Hakuna ukiranja hapa. Ni nguvu ya umma tu. Kama unavyoona watu wanajiheshimu na kuheshimiana. Hapa JF ukijiheshimu utaheshimiwa ukileta upupu watu pia hawatakulazia damu.
 
Niliposema wampe Balali Kinga watu walidhani miye nimechanganyikiwa; hili ndilo linapaswa, wakimpa kinga yatakayotoka huko makubwa. Wazungu wanajua kukamatana bwana.. (hapa najihisi niko kama Raj)

Itakuwa raha ilioje Ballali naye aamue kucut a deal na hao British investigators ili awape ushahidi wote kama anavyoujua. Ballali kama inavyosemekana alitaka kurudi ili akatoe ushahidi, lakini mafisadi hawakutaka arudi. Jamani kama mnavyoona ufisadi haulipi maana sasa matumbo ya vingunge wengi ndani ya Tanzania waliopita na wale ambao wapo sirikalini yanawaka moto.
 
CCM na JK na serikali nzima hawajawahi kumtafuta huyu Mhindi wala Ballali .Ila wameongelea tu .Hawana issue ya kumtafuta kwa kuwa wote 2 si wabaya wao .UK wanafanya yale kusafisha Nchi yao nakufuta mawazo ya biashara haramu kwa Nchi masikini .Ndiyo maana wao wanaweka rekodi kwa Nchi yao na vizazi vijavyo sisi tumekaa tu hapa .

Ukitaka ujue Usalama unafanya kazi ama polisi ingieni Uchaguzi hata mdogo hapo utawajua TIS ama Polisi nk .Au ukitaja kujua kama wako makini na kuwalinda wakubwa kauliza Mlimani na walio fukuzwa Chuo.Hizi ndiyo kazi zao.Zile za maslahi kwa Nchi hawataki kugusa .
 
Niliposema wampe Balali Kinga watu walidhani miye nimechanganyikiwa; hili ndilo linapaswa, wakimpa kinga yatakayotoka huko makubwa. Wazungu wanajua kukamatana bwana.. (hapa najihisi niko kama Raj)

Mwanakijiji,

Japo naunga mkono suala la kutoa kinga ili kukamata vigogo lakini huu mfano ni tofauti sana. Kwa UK, huyu Mhindi ni dagaa tu na lengo lao ni kukamata hao Kambare ambao ni BAE system na washiriki wao.

Kwa TZ Balali ni mmoja wa hao Kambare wanaotakiwa kunaswa. Pia suala la BOT liko wazi mno na wala hata huhitaji kumpa mtu immunity ili kuwapata wahusika. Kwa TZ walichota kwa uwazi kabisa kwasababu walijua hawatakuja kuumbuliwa, wakati suala la radar, ulitumika utapeli wa kimataifa maana ukiona kampuni kama BAE wanaenda kufungua offshore account lazima ujue walikuwa na lengo la kuficha hasa.

Kinachotakiwa ni will ya serikali yetu kutaka kuwashughulikia hao waliotubia. Kwa ninavyoona mimi, hawataki kufanya hivyo. Hata wakimpa Balali immunity, haitasaidia maana serikali ni kama haitaki kuwashughulikia hao wezi na badala yake inawalinda.
 
Mwanakijiji,

Japo naunga mkono suala la kutoa kinga ili kukamata vigogo lakini huu mfano ni tofauti sana. Kwa UK, huyu Mhindi ni dagaa tu na lengo lao ni kukamata hao Kambare ambao ni BAE system na washiriki wao.

Kwa TZ Balali ni mmoja wa hao Kambare wanaotakiwa kunaswa. Pia suala la BOT liko wazi mno na wala hata huhitaji kumpa mtu immunity ili kuwapata wahusika. Kwa TZ walichota kwa uwazi kabisa kwasababu walijua hawatakuja kuumbuliwa, wakati suala la radar, ulitumika utapeli wa kimataifa maana ukiona kampuni kama BAE wanaenda kufungua account offshore lazima ujue walikuwa na lengo la kuficha hasa.

Kinachotakiwa ni will ya serikali yetu kutaka kuwashughulikia hao waliotubia. Kwa ninavyoona mimi, hawataki kufanya hivyo. Hata wakimpa Balali immunity, haitasaidia maana serikali ni kama haitaki kuwashughulikia hao wezi.



Hiyo Will haipo ndugu Mtanzania na hivyo makelele yanaishia watu kubwaga manyanga wanajiandaa na uchaguzi Mkuu wa 2010,JK hana nia ya kpigania maendeleo ya Tanzaia bali CCM kuwa madarakani na kuendelea kutumaliza .
 
Huyu wakili kama ilivyo kazi yake, katumwa na mteja wake ili aseme na kutoa tahadhari mapema kabisa ili kwamba siku watakapomwaga mboga yote basi na yeye atamwaga ugali. Kumbuka kuwa kwa sasa bwana C bakuli lake la mchuzi limemwagwa na sasa upepo unalifuta bakuli la mboga kwa kasi ya kimbunga na yeye hawezi kukubali kirahisi na ndipo maneno ya wakili kuwa 'nitamwaga siri za vigogo wa serikali' yanapokuja.

Wakigombana tutapata akili ya kuchukua na kudai nchi yetu
 
jambo hili ndio litakalokuwa jambo lamaana pekee walotufanyia wazungu!
manake huu ufisadi bila ya mkono wa mzungu usingefichuka asilan abadan
 
Nguvu ya umma hatimaye inaanza kuchukua upper hand katika vita dhidi ya mafisadi. Mambo yanaanza kuunganika taratibu na wataanza kutajana mmoja baada ya mwingine na hapo ndio kutatokea mtikisiko mkubwa katika Taifa la Tanzania ambalo hatujawahi kuuona tangu tupate uhuru mwaka 1961.

Halafu tumsikie mtu tena aseme hadharani kwamba wahusika ni matajiri wakubwa hivyo kuwakamata kutasababisha nchi kulipuka. Maana kwa wenye mapenzi ya kweli kwa nchi yetu tunadhani kuwaacha watu hao waendelee kuwa huru ndiko kutasababisha nchi kulipuka.

Mungu ibariki Tanzania na Watu wake


Tutayajua yote tu mwaka huu!
Watatajana tu, tuvute subira tukiwa tunaendelea na michakato mingine.
 
GAZETI LA MWANANCHI JUMATANO APRIL 2008

-NI YULE WA MAREKANI

-ADAI ATALIPUA MABOMU YA WANASIASA NCHINI

-ASEMA YUKO TARAYARI KUMTETEA POPOTE DUNIANI

-IKULU YATHIBITISHA KUTOA KIBALI KUMCHUNGUZA



WAKILI ANAEMTETEA FISADI ALIEKUWA WAZIRI WA MIUNDO MBINU MHE A.CHENGE J.LWEISKY MADOSKY AMESEMA ANASUBIRI KWA HAMU MTEJA WAKE AFIKISHWE MAHAKAMANI,,MADORSKY AMBAE NI MARA YA KWANZA KUZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI KWA NJIA YA SIMU ALITAMBA MAHAKAMANI HUKO NDIKO KWENYE KILA KITU NA UONGO AU UKWELI UTABAINIKA
NIMEWASILIANA NA CHENGE AMENIPA MBINU ZOTE ZINAZOTUMIWA NA BAADHI YA WANASIASA KUMWANGAMIZA

TUNASUBIRI KWA HAMU SERIKALI AU TAASISI YOYOTE IMFIKISHE MAHAKAMANI NA MIMI NITATOA USHAHIDIAMBAO UTAITISHA DUNIA NZIMA...MMMHHH PATAMU HAPO,,

KAULI HIYO YA MADORSKY IMEKUJA SIKU MOJA BAADA YA WAZIRI WA UTAWALA BORA SOPHIA SIMBA KUELEZA UWEZEKANO WA CHENGE KUFIKISHWA MAHAKAMANI KAMA USHAIDI UTAPATIKANA

WAKILI HUYO AMEIDHIIRISHIA DUNIA KWAMBA YUKO TAYARI NA MPAMBANO WOWOTE NA KUONYA HATOMWACHA MTU WALA KUMWOGOPA HATA AKIWA MKUBWA KIASI GANI,,

HATA HIVYO ALIVYOULIZWA SWALA LA KIASI GANI ANALIPWA NA CHENGE ALISEMA SIWEZI KUMWAMBIA MTU INAWEZEKANA NAMFANYIA BURE AU ANANILIPA MABILLION AU PESA NDOGO SANA..KAZI IPO JIBU UNALO MSOMAJI..ALISEMA ANATUMAINI TUHUMA ZA CHENGE ZINA MKONO WA SIASA KUTOKANA NA BAADHI YA WATU KUMBAMBIKIZIA ALISEMA MTEJA WAKE WAKATI AKICHUNGUZWA ALIKUWA ANAJUA KILA KITU ..ALIPOULIZWA KWAMBA ANA HABARI MTEJA WAKE KUPEKULIWA ALISEMA HAKUNA ASICHOKIJUA ANA TAARIFA ZOTE NA HUWA ANAWASILIANA NA CHENGE KILA SIKU....

KWENU WAPENDA NCHI NA OLE WENU VIONGOZI MTAKAOTAJWA MTAMFWATA HUYO CHENGE KWA GHARAMA HATA KAMA AWE RAISI WA NCHI..KARIBU MADORSKY UTUFUMBUE MACHO WATANZANIA TUMEPIGWA NA BUTWAA KUMBE KUNA ZAIDI YA HAYO

KWENU WANANCHI

There's no substance at all in this other than hype and nonsense. Ask yourselves, why would Accomplished Gangster Chenge, now that he's been busted, want to implicate his peers in the CCM and Gangsterment while still sitting on a $23 million fortune? Despite having apparently resigned recently, Chenge is still a major figure in the Tangold scam, and will continue being the Grand Vizier of Grand Thieves, big time scammers and swindlers in the CCM and Government for al long time to come.
 
Yaani Chenge kamwaadvise lawyer wake upumbavu mtupu. Siku zote watu walikuwa wanasema Chenge anaogopwa sababu anajua siri nyingi, nadhani na yeye kaamini upumbavu huo.

Siri chenge hawezi kutoa sababu zinawahusu wezi wenzake. Waliomtosa sio mafisadi wakuu, wanaweza kuwa na matatizo kidogo lakini sio level ya Chenge na hao wenzake kina EL, BWM.

Halafu kwa kusema kuwa atatoa siri akipelekwa mahakamani kwangu mimi kwenye court ya public opinion ameshakubali yeye ni mwizi na ana siri za wezi wengine wakubwa, au nimekosea?????

Vilevile sio mzalendo sababu ana siri kubwa lakini kaiweka moyoni.

PR mbovu kupita kiasi na inaonekana kaokota lawyer sijui wapi ambaye hajua kabisa mikimiki ya bongo.
 
NIMEWASILIANA NA CHENGE AMENIPA MBINU ZOTE ZINAZOTUMIWA NA BAADHI YA WANASIASA KUMWANGAMIZA

TUNASUBIRI KWA HAMU SERIKALI AU TAASISI YOYOTE IMFIKISHE MAHAKAMANI NA MIMI NITATOA USHAHIDIAMBAO UTAITISHA DUNIA NZIMA...MMMHHH PATAMU HAPO

Ha ha ha. Huu ni mkwala wa Mbu nje ya Net.

Mimi nitazidi kuomba kwa Mungu ilifikie huko halafu tuone atafanya nini.

Madorsky! Watu wazima hawatiahiwi Nyau. Client wako kachemsha.

Wasifikiri kama tumeyasahauu ya Balali nayo yanakuja.
 
hii habari ya huyu kasema hikina yule kasema vile ni kupoteza muda tu,kwa nini tusimtafute na kumwambia atupe kilicho chetu ?,hayo mengine watajuwana huko kwenye vikao vyao vya siri lakini chetu tuwetumesha chukua.kama akikataa basi tumfafune yeye mwenyewe.
 
Hako ka shy sio kashushushu wala nini. Ni mzembe mmoja tu aliye na access na internet halaf hajui cha kuifanyia. Nahitaji 1 mo week kumtuliza, sasa hivi nafuatilia nyendo zake nilianza kipindi kile cha vurugu UDSM
 
Nina fununu kwamba Chenge pesa nyingi kazipata tokana na cut ya IPTL .Hapa ndipo pana kazi .SFO wanachunguza cut lake kwenye radar which is gonna turn out monor.IPTL hawachunguzi na huko ndiko sasa kuna mapesa ya akina Mgonja, Mama Kejo na wengine .JK wakati wa IPTL alikiuwa nani ? Sasa mchezo mtamu .Je anaweza kupelekwa mahakani halafu wakili wake aje kusema mambo yake ? Serikali ina ubavu ama ndiyo imetoka kama EPA ?
 
Wewe Unasema Nini Kuhusu Habari Hii Uliyoileta ? Au Huna Lolote Kwanza Unasikiliza Upande Gani

Yaani rafiki yangu huwezi kujitahidi kuficha ushushu wako?Tunajua kuwa upo kwa maslahi ya hao mabwana zako (mafisadi) wala haina kukatisha watu tamaa. Hilooo lione limetahayari uso umekushuka JF wote wanakusonya.

Ukikusanya sauti zetu tunazokusonya unaweza kutengeneza beat ya nyimbo!
 
*Ni wale wa makosa ya jinai waliompekua Dar
*Asema wana mkono mrefu katika kuchunguza


Na Ramadhan Semtawa


SIKU moja baada ya wakili wake J Lewis Madorsky, kuibuka na kutema cheche, Andrew Chenge amesema makachero wa kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai kutoka Uingereza yaani Serious Fraud Office (SFO), ni mahiri na wenye mkono mrefu, hivyo hakuna kitu kitakachofichwa.


Wakili Madorsky ambaye alizungumza na Mwananchi juzi kutokea Marekani ikiwa ni chombo cha kwanza cha habari nchini Tanzania kuongea nacho, alisema atamtetea Chenge popote duniani na atalipua mabomu kuhusu baadhi ya wanasiasa wanaomchafua mteja wake.


Kauli hiyo mpya ya Chenge inatoa taswira kwamba, sakata hilo kwa sasa linapaswa kusubiri matokeo ya SFO ambayo itatoa hatima ya ukweli au uongo wa tuhuma zinazomkabili.


Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Chenge alisema mkono mrefu wa SFO utaweka bayana kila kitu kuhusu tuhuma zake; ndiyo maana sasa ameamua kukaa kimya.


Chenge alifafanua kwamba, anachotaka Watanzania wapate ni usahihi na ukweli wa tuhuma zake na si maneno ya kufikirika.


"Sioni haja ya kuendeleza mbinu zisizo na msingi, SFO wana mkono mrefu, hivyo kama ni ukweli utafahamika baada ya uchunguzi wao," alisisitiza Chenge.


Waziri huyo wa zamani wa Miundombinu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa zaidi ya miaka kumi, alisema hadi sasa bado taarifa kuhusu tuhuma zake zimekuwa zikipotoshwa na baadhi ya watu.


Alisema ni vema mkanganyiko huo wa taarifa ukaondolewa kwa Watanzania kusubiri taarifa sahihi za SFO.


"Maana hadi sasa kuna baadhi ya Watanzania hawataki kuelewa ukweli, ni vema sasa wakasubiri kupata taarifa sahihi ili kuondoa mkanganyiko huo wa taarifa," alisisitiza.


Chenge aliongeza kwamba, asichotaka yeye ni kuona Watanzania wanadanganywa kuhusu tuhuma zinazomkabili ndiyo maana anasisitiza wavute subira ili wapate matokeo ya uchunguzi wa SFO.


"Sitaki Watanzania wapewe taarifa ambazo zinapotosha ukweli wa jambo lenyewe lilivyo," aliongeza Chenge.


Kuhusu taarifa kwamba makachero wa SFO walikuta nyumbani kwake kila aina ya fedha kama Duka la Kubadilishia Fedha, alisema mengi yatasemwa, lakini ukweli utabainika baada ya uchunguzi.


"Kwa kipindi hiki kila kitu kitasemwa, nafikiri jambo la msingi ni kusubiri matokeo ya uchunguzi wa SFO."


Chenge ni mmoja wa viongozi waandamizi wa serikali ambao SFO inawachunguza kuhusiana na tuhuma za kuhusika katika sakata hilo.


Kuchunguzwa kwa Chenge haimaanishi kwamba, ameiba au amekula rushwa, isipokuwa SFO inataka kuona Sh1.2 bilioni ambazo amezihifadhi katika akaunti yake moja katika kisiwa cha Jersey kama zina uhusiano na sakata la ununuzi wa rada kutoka BAE System ya Uingereza.


Ndani ya serikali ya Tanzania, inaelezwa sakata hilo linagusa vigogo kumi (Top Ten) wa serikali iliyopita kuanzia Rais mstaafu Benjamin Mkapa na baadhi ya mawaziri, naibu waziri mmoja na makatibu wakuu katika serikali ya sasa.


Chenge anaelezwa kukutwa na kiasi hicho katika akaunti yake moja katika kisiwa hicho cha Jersey, hivyo kufanya makachero hao wa SFO kuchunguza mabilioni hayo kama yana uhusiano na rada iliyonunuliwa mwaka 2002.


Ununuzi wa rada hiyo ambayo pia ilimtikisa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair, inaelezwa kuwa ghali kwa nchi maskini kama Tanzania ambayo ingeweza kununua rada ya Sh 5 bilioni kuliko hiyo ya Sh 70 bilioni.


SFO inaangalia fedha Sh12 bilioni, ambazo dalali wa biashara hiyo alipewa kama aliweza kuwahonga vigogo hao wa serikali kuanzia Rais mstaafu Mkapa na vigogo hao wengine tisa akiwemo Chenge.


Matokeo ya uchunguzi huo yanasubiriwa kwa hamu nchini, ili kuondoa utata na kuweka ukweli kuhusu tuhuma hizo dhidi ya Chenge huku pia Watanzania wakitaka kuona vigogo wengine zaidi wanawajibika baada ya Chenge kufanya hivyo kwa kujiuzulu uwaziri.

Source: Gazeti Mwananchi
 
Evarist H. Mbuya
Firm: J. Lewis Madorsky Co. L.P.A.


Address: 3934 Washington Blvd
Cleveland, OH 44118-3135
Map & Directions


Phone: (21...
Fax: (216) 371-7601

J Lewis Madorsky
Firm: J. Lewis Madorsky Co. L.P.A.


Address: 3934 Washington Blvd
Cleveland, OH 44118-3135
Map & Directions


Phone: (21...
Fax: (216) 371-7601

J. Lewis Madorsky Co. L.P.A.
26 Byron Court, 26 Mecklenburgh Square, London, England
J. Lewis Madorsky Co. L.P.A.
Almeida Park, Bandra, Mumbai 400 050, India
(216)371-7600
J. Lewis Madorsky Co. L.P.A.
Nic Investment House, 14th Floor, PO Box 181, Dar Es Salaam, Tanzania
255-51-44889
 
Back
Top Bottom