THE NATIONAL DEVELOPMENT FORUM: Tamko la Kumpongeza Rais kwa utendaji kazi wake

Aug 11, 2016
13
3
JUKWAA LA MAENDELEO TANZANIA (NATIONAL DEVELOPMENT FORUM)

Tamko la Kumpongeza Rais kwa utendaji kazi wake.
edited_1470497172982.jpg

Ndugu wanahabari awali ya yote nawasalimu!!

Ndugu wanahabari, Leo hii tumejitokeza tena mbele yenu tukiwa na lengo la kutoa maoni yetu sisi kama Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania, kwa misingi hiyo basi tunafurahishwa na utendaji wa serikali ya Mheshimiwa Rais Dr John Joseph Pombe Magufuli aliyeanza kuongeza Taifa letu kwa takribani miezi 9 sasa.

Ndugu wanahabari, mambo yaliyofanywa na Mheshimiwa Rais hadi sasa ni makubwa sana na tunaona kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano anaweza kuwa ametekeleza ahadi zake zote na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 chama kilichopo madarakani kwa asilimia 100%.

Ndugu wanahabari, Jukwaa Huru la Wazalendo, tunatambua juhudi kubwa zinazoendelea kuchukualiwa na serikali ya Rais Dr John Joseph Pombe Magufuli katika uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji nchini sambamba na ujenzi wa madaraja makubwa na madogo likiwemo daraja la kilombero na Ifakara mkoani Morogoro.

Ndugu wanahabari, tunaendelea kuipongeza serikali yetu kwa kuendelea kusambaza huduma ya umeme vijijini kwa mapato yetu wenyewe bila kutegemea ufadhili, hii ni dalili tosha kuwa serikali ya awamu ya tano inalenga kujenga Taifa linalojitegemea, ndugu wananchi hasa wa vijijini na wadau Wa maendeleo tunaomba huduma hii ya umeme itumike kuondoa umaskini kwa kuanzisha miradi midogo midogo inayotumia nishati ya umeme.

Ndugu wanahabari, sote tutakumbuka kuwa serikali ya Mheshimiwa Rais Dr John Joseph Pombe Magufuli hadi sasa imeweza kupambana uboreshaji wa huduma za Afya na kupelekea watanzania kuanza kupata huduma bora za Afya ikiwemo ongezeko la vitanda, magodoro na vifaa tiba vimeongezeka kwenye hospitali zetu hapa nchini, pia tumeshuhudia juhudi za wizara ya Afya kupitia taasisi zake hasa MSD kufungua maduka ya dawa hospitality ili kusogeza huduma za afya karibuni na wananchi.

Ndugu wanahabari, serikali imeweza kuongeza makusanyo ya mapato na kusimamia matumizi ya mapato na kuepusha matumizi holelala ya fedha za walipa kodi ambayo ni wananchi wa Tanzania, pia mianya ya ukwepaji wa kulipa kodi umedhibitiwa na inaendelea kudhibitiwa. Ndugu wanahabari, sisi kama Jukwaa tunaipongeza serikali hatua ilizochukuwa kuboresha huduma za Elimu hapa nchini, hatua zinachukuliwa ni dalili za kuhakikisha kila mtanzania anapata Elimu iliyobora zaidi.

Jukwaa tunapenda Kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa moyo wake wa uzalendo kwa wananchi na taifa Lake, ndugu mwanahabari hivi karibuni tulishuhudia Mheshimiwa Rais akitoa ahadi ya msaada wa babaji kwa mlevu ndugu Thomas Kone baada ya kuona taarifa kwenye moja ya chombo cha habari hapa nchini, hivyo tunaendelea kutoa wito kwa vyombo vya habari kuripiti matatizo ya Watu katika jamii.

Ndugu wanahabari, ju tunaipongeza serikali kuendelea kutoa huduma za Afya kwa mama na mtoto bure, huduma za afya bure kwa wazee. Ndugu wanahabari, Jukwaa tunaungana na vyombo vya habari vya nje ya nchi vinavyoendelea kuandika na kutangaza ubora wa Mheshimiwa Rais wetu, taasisi mbalimbali za nje ya Taifa zimejitokeza wazi wazi kumpongeza Mheshimiwa Rais, pia baadhi ya Taasisi za ndani nazo zimempongeza Mheshimiwa Rais kwa namna moja au nyingine kutokana na utendaji kazi wake na serikali yake .

Jukwaa, tumefurahishwa na taarifa zinazoendelea kuchapishwa na magazeti ya nje ya bara la Africa kwa lugha mabalimbali zikimsifia Mheshimiwa Rais, na kufikia hatua kumuona kama Rais bora kuliko wote barani Afrika na kusema ni mtu aliyesubiriwa zaidi ya miaka 50 na baadhi ya Raia wa nchi mabalimbali Barani Afrika kutamani Mheshimiwa Rais Dr John Joseph Pombe Magufuli awaongozee mataifa yao walau kwa mwezi mmoja tu kama tulivyowashudia kwenye vyombo vya habari, hivyo ni mtu punguani kiasi gani anaweza kwenda mitaani kupinga ubora wa Rais MAGUFULI na serikali yake, watanzania tusikubali kudanganywa na wanaharakati uchwara.

Jukwaa, tunapenda kuwahakikishia jumuhiya za mataifa ya nje zinazofanya shughuli zake hapa nchi kuwa Rais Dr John Joseph Pombe Magufuli anayodhamira ya dhati kabisa kuboresha maisha ya wananchi na tunaomba taasisi na jumuhiya hizo za kimataifa kuendelea kufanya kazi zao huku wakifuata sheria zilipo hapa nchini na kuheshimu na zikifuata Mira na desturi za watanzania.
Jukwaa, linapongeza Mheshimiwa Rais wetu kuliwezesha Taifa letu kushinda zabuni kubwa za ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, na kujenga bomba la mafuta kutoka Uganda hadi nchini DRC Kongo, haya ni Mafanikio makubwa sana yanayotokana na misingi iliyojengwa na serikali za awamu zilizopita, Mheshimiwa Rais hongera sana kwa ushindi huo mkubwa.

Jukwaa, tunaamini katika misingi ya haki za binadamu na utawala bora, hivyo tunaomba vita dhidi ya mapambano ya rushwa hapa nchini kuongezwa na kuungwa mkono na wananchi wote kwa vitendo, msingi wa ukiukaji wa haki za binadamu inatokana na vitendo vya rushwa kwani "rushwa ni adui wa haki" hivyo tunayoimani kubwa kwa mamlaka zinazohusika zitaongeza nguvu katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa, tunaamini mahakama ya mafisadi itasaidia kupunguza tatizo la rushwa. Jukwaa tunatoa ombi maalum kwa serikali kuwa mahabusu ya wahujumu uchumi Kiberege iliyopo mkoani Morogoro itumike rasmi kuwafunga watu watakaokutwa na hatia dhidi ya Ufisadi na uhujumu uchumi kwani historia inaonesha mahabusu hii ilitumika kuwafunga mafisadi miaka ya 1980.

Ndugu wanahabari, tunapongeza juhudi za serikali kuendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa viwanda hapa nchini, hivi karibuni tumeshuhudia Mheshimiwa Waziri Mkuu akifungua viwanda vikubwa vikiwemo viwanda vya nyama na nguo. Pia katika maeneo mabalimbali ya nchi kuna ujenzi mkubwa wa viwanda unaondelea, katika hili tunatoa wito kwa wananchi wenzetu kuachana na propaganda zinazofanywa na wapinga maendeleo hapa nchini na kudai hakuna viwanda hapa nchini.

Mwisho :
Jukwaa la Maendeleo Tanzania linatoa wito kwa watanzania kuendelea kuwapuuza watu wanaotumiwa na mafisadi kwa maslahi yao binafsi na kutumia taasisi au vyama vyao vya siasa kama kichaka cha kuwalinda mafisadi na wizi wa mali za umma, watanzania wote tukatae katu katu kutumika vibaya na wanaharakati wanaolenga kukukwamisha serikali yetu kwa visingizio uchwara visivyokuwa na mashiko kwa ustawi wa jamii ya wananchi.

Tunawaomba wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku na kuepuka kujihusisha na harakati zisizokuwa na maslahi kwao bali kwa watu fulani, tunawapongeza Viongozi wa dini mnaoendelea kuombea amani ya Taifa letu.

Mungu ibariki Tanzania.

Tamko limetolewa kwenu.

Mwenyekiti (Taifa)
Jukwaa la Maendeleo Tanzania
Jasper Jackson Muganyizi
0784097173, muganyizi@yahoo.com
 
Back
Top Bottom