TFF lawamani mapato Simba vs Yanga

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
WAKATI wingu la utata wa hesabu sahihi za mapato katika mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, iliyopigwa Jumatano iliyopita likitanda, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesisitiza sh 390,568,000 ilizotangaza ni sahihi.TFF ilitangaza kuwa, fedha hizo zinatokana na mauzo ya tiketi kwa watazamaji 50,455 walioingia kushuhudia pambano hilo, kwa viingilio vya sh 5,000, sh 7,000, sh 10,000, 15,000, sh 20,000 na sh 30,000.Hata hivyo, hesabu hiyo ya watazamaji iliyotangazwa na TFF inapingana na ile iliyooneshwa na kituo cha SuperSport kilichoonesha watu 58,000 waliingia uwanjani kushuhudia pambano hilo la mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu bara.Kutokana na hali hiyo, wadadisi wa mambo, pamoja na klabu ya Yanga, wamehoji uhalali wa mapato hayo na idadi ya watu walioingia uwanjani siku hiyo na ufanyike uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.Akizungungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, alisema kwamba hali hiyo inatia shaka, kwani hata takwimu za idadi ya watazamaji zilizotolewa na TFF ni tofauti na ile ya SuperSport.Alisema kwa mahesabu ya haraka haraka, hata mashabiki waliohudhuria mechi hiyo wangelipa sh 15,000 kila mmoja, zingepatikana zaidi ya sh milioni 600, hivyo hata klabu husika zilistahili kupata zaidi ya sh 93,345,549.15 walizogawiwa kila moja.Mwalusako aliongeza kwamba, wanashindwa kuelewa hali hiyo inatokana na nini na kuiomba TFF kufanya uchunguzi wa haraka ili kujua tatizo linatoka wapi, lakini kinyume na hapo hali itazidi kuwa mbaya.Katibu huyo aliongeza kuwa, wanatarajia kuwasiliana na viongozi wenzao wa Simba ili kujadili hali hiyo kabla ya kutoa tamko la pamoja.Kwa ypande wake, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema kuwa, idadi waliyoitangaza ni ya watazamaji walionunua tiketi pekee.
 
Watakuja MODS kuihamisha.

Kwa sasa wapo wanakunywa Supu nimewaona hapo Hongera Sinza!
 
Ushauri wa bure kwa TFF watumie IT kama Prime time wanavyofanya,,,tiketi zinakuwa na ID(barcode) so inakuwa rahisi kuhakiki tiketi feki,kujua idadi ya watu pamoja na mapato.

miaka 50 ya uhuru! TFF wana akili za mgando ili kupata loop holes za kufanya ufisadi!! walizoea kuiba kule shamba la bibi cos kuna watu wanasimama,lakini huu uwanja mpya unachukua watu elfu 60,kila kiti kina namba.
 
.Mwalusako aliongeza kwamba, wanashindwa kuelewa hali hiyo inatokana na nini na kuiomba TFF kufanya uchunguzi wa haraka ili kujua tatizo linatoka wapi, lakini kinyume na hapo hali itazidi kuwa mbaya.


Kwani Supersport walihesabu mtu mmoja mmoja? Hovyo kabisa hawa viongozi ndio maana TFF inaendelea kuwaibia tu!

 
Hongera bar ipo sinza kweli??? Mijitu inayoishi mbagala utaijua tuu!! Hongera bar ipo karibu na chuo cha ustawi wa jamii so ipo kijitonyama.
wanachuo wa usitawi wanafeli sababu ya ile bar. ile bar ni noumer. kwa ufupi ipo kinyama. mia
 
Wakati Mabingwa wa afrika mashariki na kati Yanga ikigomea mapato kiongozi moja wa simba anasema wao upande wa MNYAMA wanaafiki hicho kiwango kilichopatikana ya 93 mil huyu kiongozi gani huyu Kamwaga sijui kazoa yani ni NG'OMBE Kabisa hivi anajuwa ile gharama ya kulpa wale waganga tu kule zenji FOS Wamelipa kiasi gani!au anajuwa kambi ya Simba kule mwanakwerekwe imetumika kiasi gani huyu Rage kaingia na Majitu ya AJABU AJABU Kwenye hii timu jitu hatakuongea haliwezi domo kama linakula pariki
 
Wakati Mabingwa wa afrika mashariki na kati Yanga ikigomea mapato kiongozi moja wa simba anasema wao upande wa MNYAMA wanaafiki hicho kiwango kilichopatikana ya 93 mil huyu kiongozi gani huyu Kamwaga sijui kazoa yani ni NG'OMBE Kabisa hivi anajuwa ile gharama ya kulpa wale waganga tu kule zenji FOS Wamelipa kiasi gani!au anajuwa kambi ya Simba kule mwanakwerekwe imetumika kiasi gani huyu Rage kaingia na Majitu ya AJABU AJABU Kwenye hii timu jitu hatakuongea haliwezi domo kama linakula pariki

Kwa wakati huu tunaoendelea nao sijawahi kuona Kiongozi wa ajabu kama huyu Ezekiel Kamwaga,mimi huwa napata shida sana kumwelewa,yeye akiwa kama Msemaji wa Simba yale anayoyasema kila mara mbele ya hadhira ni official taarifa za Club au ni mtazamo wake,Kamwaga ni moja kati ya Wasemaji wa team waongea pumba sana,mimi ndo maana huwa namwitaga Msemaovyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom