Tetesi; Eti Jay Dee ameenda kupandikizwa mimba (artificial insemination)

jamani hakuna mengine ya kuongea,? achana na maishi binafsi ya mtu
 
jamani hakuna mengine ya kuongea,? achana na maishi binafsi ya mtu

Sasa we unataka nani aongelewe kwenye hii Forum, hawa si ndo ma'cerebrity wetu we vipi??
 
artificial insermination au intra vitro fertilization(ivf) ni jambo la kawaida kwa nchi zilizoendelea. ni njia sahihi na bora ya kujipatia watoto kwa wanaohitaji. ni jambo la mke na mume kumuona dokta wa uzazi juu ya tatizo lao la kutopata watoto. mwanamke hupimwa uwezo wa mayai yake na mwanaume hupimwa Strength ya mbegu zake kuweza kurutubisha yai. ikiwa mwanamke ataonekana yuko fit na mume mbegu zipo lakini ni dhaifu kwenye spidi ya kurutubisha, hupewa chombo maalum cha hospital ambacho ataweka mbegu zake baada ya yeye kuwa tayari kuzitoa. kitaalamu huchukuliwa na kuchujwa hadi mbegu imara zibakie bila yale majimaji mengine. mbegu hizi huhifadhiwa kwenye chombo maalum. Hivyo mke huwekewa mbegu hizo wakati akiwa kwenye tarehe yake ya kupevusha yai kwa njia ya mpira maalum wa hospital. Kama Ikiwa jaribio la kwanza halikunasa ataendelea kutaimiwa hivyo hivyo hadi atakapopata ujauzito. Akipata ujauzito kujamiana kutaendelea kama kawaida. Kwa wale wenye uwezo hapa kwetu wanaweza kutafuta mtoto kwa njia hii ila sijui kama utaalamu huu hapa kwetu upo. Nilisoma kwenye mtandao gharama yake inaweza kuwa dola elfu sita($6000). Kama Jide kweli kaamua hviyo kipekee nampongeza kuliko kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati siku hizi utalaamu uko wa kusaidia kupata watoto. Mungu akujalie upate mimba uzae mtoto Jide.
 
all the best card.jpg

Mtoto ni mtoto tu,
ukipata shukuru.
 
Back
Top Bottom