TCU iunganishwe na NACTE & HESLB kuleta ufanisi

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,603
32,287
Mlundikano wa Taasisi nyingi kwenye majukumu yanayokaribia kufanana ni upotevu wa pesa za umma kwa gharama za pango, magari, posho za wajumbe wa bodi na vikao vingi visivyo na tija.

PENDEKEZO: Iundwe BODI YA ELIMU YA JUU, Higher Education Council, HEC (ikiwa na Idara za UDAHILI/Kuboresha Ubora wa Elimu - Quality Assurance, utoaji/urudishaji MIKOPO). Wafanyakazi wengine wapunguzwe kwa kupewa stahiki zao zote.

NB: Ni aibu taasisi kama hizi tena baadhi zinaongozwa na Maprofesa (PhD) kukosa ufanisi wa kudahili wanafunzi wasio na sifa, pia baadhi ya vyuo vikuu binafsi utoaji wa elimu huko ni wa kutiliwa shaka sana, mnasubiri nini kuvifuta? Wasomi mnatuangusha jamani.
 
Tuseme TCU imeishiwa pumzi? Sasa mnataka ziunganishwe na zile "Shangingi" VX/Nissan Patrol itakuaje si tutanyang'anywa? au tutauziwa kwa bei chee?, wale wajumbe wa bodi nao si watakosa ulaji? Jamani muwaonee huruma watu wana familia zinawategemea mjue.
 
Hapo naona walilahisisha majukumu na urasimu wa upatikani Huduma.

Unapitia ngazi ya Kwanza NECTA..Mitihani na Watahiniwa.

Unakuja ngazi ya Pili TCU wanakupangia pakwenda

Unakuja Ngazi ya Tatu Wanakupangia upate mkopo kiasi gani au usipewe kabisa.

Kikubwa ni waboreshe huduma zao, tukumbuke pia unaposema wapunguze wafanyakazi huko pia ni kuongeza Wategemezi.
 
Tena hizo taasisi ziunganishwe hata kesho maana ni kama wanaingiliana katika utendaji wao, na kuongeza gharama za uendeshaji na mzigo kwa mlipa kodi. Sijui kwa nini Waziri hajapeleka muswada bungeni kutaka bunge liridhie kuunganishwa kwa taasisi hizi
 
Mhe. Waziri wa Elimu peleka muswada Bungeni pesa za walipa kodi zinachezewa na hawa watendaji wa TCU, NACTE na HESLB wakati ufanisi ni SIFURI.
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Fikiria enzi zile za Giza, wakati wa Bunge kila Boss wa hizo za taasisi anaenda Dodoma na Shangingi lako kwenda kusikiliza bajeti. Daah Bora awamu hii wamefutilia mbali huu ufujaji wa pesa na muda.
 
Wafanyakazi wa hizo taasisi wapunguzwe maana wengi ni kukaa tu. KAzi wanazofanya hazionekani.
 
TCU wacha ibaki peke yake! Kumbuka TCU ina kazi kubwa sana .. Moja wapo kuhakikisha vyeti vya wanasoma nje ya nchi kama ni vyenyewe au feki! Ukiwapa majukumu ya necta na bodi kutakuwa na mrundikano wa kazi ....

Binafsi nilipitia huo utaratibu niliporudi ilichukua wiki 3 imagine unawapa kazi nyingine si watakaa miezi..
 
Taasisi hizi zinaongozwa na watu wasio na sifa za (kitaaluma & utendaji) maswala ya Elimu. Kama taifa tuje na mpango mkakati wa kuheshimu taaluma za watu.
 
SAWA,zinafanana majukumu.Hivi hakuna taasisi zingine zinazofanana majukumu?.Je,nini maana ya kutengeneza ajira?
 
Back
Top Bottom