TCRA Yatoa Ufafanuzi wa Digitali: King'amuzi Kimoja Tuu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,494
113,590
Wanabodi,

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA leo imetoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa digital na kueleza kuwa huna haja ya kuwa na king'amuzi zaidi ya kimoja na wenye TV za migongo wasiwe na wasiwasi tutaingia mfumo wa digitali na TV zao hizo hizo!.

Ufafanuzi huo umetolewa na Meneja Mawasiliano wa TCRA Bw. Innocent Mungy alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa live la TBC-1.

Bw. Mungy amesema matangazo yote yatarushwa na makampuni matatu yanayoitwa Multiplex Operators ambao ni Star Media, Agape Associates na kampuni nyingine moja, ila ili kuziona chanel za bure ambazo ni free to air kama ITV, TBC, Channel Ten, Star TV etc, sio lazima kuwa na ving'amuzi vitatu, kingamuzi kimoja tuu kinatosha na TV zote za bure zitapatikana humo!.

Ufafanuzi huu umemaliza rasmi ile simtofahamu ya wasiwasi wa watu kuzitupa TV zao za migongo au kulazimika kufunga ving'amuzi zaidi ya kimoja!.

Huyu Bw. Mungy wa TCRA, anastahili pongezi kwa kutoa ufafanuzi murua. Hongera Innocent Mungy!.

Pasco.
 
Pasco bana, yani huyu bwana apewe pongezi kwasababu gani??!!

Naona umekuja ki-tbc leo
 
Pasco bana, yani huyu bwana apewe pongezi kwasababu gani??!!

Naona umekuja ki-tbc leo

hata mimi sion sababu ya kumpa pongezi huyo bwana kaajiriwa kwa kazi hiyo altegemea nani ndo aje kutoa ufafanuz
 
We Pasco hebu tuache wenzio tunashangilia ushindi bana, msalimie sana Mwigulu, Lusinde, Lowassa, Nkapa, Wassira na wengine wote wanaonifahamu.
 
pasco unapokuwa unatangaza vipindi vyako vya ppra nani akaupongeza?wakati tunajua kuwa hilo ni jukumu lako na unalipwa kwa kazi hiyo.g.huyo bwana wa tcra hiyo ni kazi yake anapaswa kuífanya kama alivyo fanya.hakuna cha kumpongeza katika hilo kila mtu awajibike mahali pake pa kazi.
 
hayo maneno pekee
aseme kwa uhakika kuwa hao selected service providers watalazimika kuingiza bure matangazo ya tv za ndani(content providers)i ili mwananchi pale atakapoamua kuchukua kingamuzi chochote apate hizo channel za ndani pia.
kuna sheria inayowabana hao service providers kufanya hivo kwa sasa?
au kaamua tu kuwafurahisha watazamaji wa TBC?
pasco unawapongeza nini sisi ni consumer wa TCRA hivo ni wajibu wao kutulinda sisi.
 
Mimi bado sijaelewa hayo mashirika 3 likiwemo agape ni kuwa tutaanza kulipia hivyo ving'amuzi kwa mwezi?
naomba ufafanuzi
 
Kwanza kwa muonekano ulivyo.. kutakuwa hakuna tv ya bure.. Maana ukishakuwa na king'amuzi inabidi ulipe ili uweze kuona.. Na wao wanapanga (kwa mfano star media).. Wanakuwekea kwenye vifurushi na kuvipa majina.. Na kila kifurushi unalipia shs. 9,000.. Na kama hujalipa wanakufungia.. So waache kutudanganya wameshaona mwanya wa kula hela za watanzania..
 
Mkuu Sosoliso, Bwana Mungy amefafanua kuwa ving'amuzi vitalipiwa, ila free to air zitakuwa bure, hata usipolipia, hutaweza kuona tuu zile chaneli zao za kulipia lakini zile tv ambazo zoki free to air zitaonekana, ulipe, usilipe!.
 
hayo maneno pekee
aseme kwa uhakika kuwa hao selected service providers watalazimika kuingiza bure matangazo ya tv za ndani(content providers)i ili mwananchi pale atakapoamua kuchukua kingamuzi chochote apate hizo channel za ndani pia.
kuna sheria inayowabana hao service providers kufanya hivo kwa sasa?
au kaamua tu kuwafurahisha watazamaji wa TBC?
pasco unawapongeza nini sisi ni consumer wa TCRA hivo ni wajibu wao kutulinda sisi.
Mkuu Lokissa, kwa sasa, kila kituo kinajirushia content yake, na ukitaka kurusha content ya mwingine, lazima upmbe kujiunga na akubali, kama tunavyoonaga wakati wa live mbalimbali kwa matukio ya kitaifa.

Kuanzia 1/1/2013, hakuna tena kituo cha TV kitakacho rusha matangazo yake yenyewe, matangazo ya tv zote yatarushwa na yale makampuni matatu, multiplex providers, makampuni hayo yote matatu, yatalazimishwa kurusha tv zote ambazo ni free to air tena bure ili kingamuyzi chochote utachonunua, uweze kuona tv zote za bure, kuwaepusha watu kulazimika kununua ving'amuzi vyote vitatu!

Kuhusu pongezi, japo kweli ni kazi yake, lakini mtu anapofanya kazi yake well done na sisi tunanufaika, anastahili pongezi, its just a matter of appreciation, ndio maana kulipotokea ubishi mkubwa kuwa serikali ya CCM au JK hajawahi kufanya lolote la maana kwa nchi hii, mimi nilipinga, na ndio nikaanzisha ule uzi wa mazuri ya JK, just to appreciate the little. Wana jf wenzangu, tuwe na shukrani katika madogo, ndipo tutaweza kufanyiwa makubwa!. Kwa mliosikiliza hotuba ya Nasari baada ya ushindi mtakuwa mmeona jinsi alivyo mtu wa shukrani!.
 
Back
Top Bottom