kalamu ya chuma
JF-Expert Member
- Jan 22, 2014
- 214
- 62
Moja ya sifa ya biashara ni mhusika kumsikiliza mteja ,kwa lugha za sasa ni mtoa huduma kumjali mlaji,jana naibu waziri wa mawasiliano akiwa huko morogoro amekiri nae kuwa miongoni mwa wahanga wa tigo kununua kifurushi kwa kiasi kadhaa na kujikuta hupati huduma hiyo au unapata chini ya kiwango. Juzi imekula kwangu pia,yaani nilinunua kifurushi cha 1000 nikapata meseji nimepata dk 120 tigo kwenda tigo na dk 20 mitandao yote,lakn baada ya muda mfupi kuangalia salio la kifurushi naambiwa nina dk 71 tigo kwa tigo na dk 2 mitandao yote,nikapiga simu huduma kwa wateja kuuliza kulikoni hawana majibu mara ooh ni promotion imekwisha na umepata hivi,lakn nikawauliza nimepataje ujumbe wa dk 120? akabaki anahesabu hewa hana jibu,kwa kifupi nimechoka sana,cha kunishtua zaidi mpaka Naibu waziri au waziri nae anajitaja kama sehemu ya wahanga! aisee kumbe ndo mchezo wenu? najiuliza michezo hii na malalamiko haya hayaishi why? tcra kama baba yetu mbona hamchukui hatua? imenifanya nibaki nikishangaa sana,hivi matatizo ya mitandao hii mwisho wake lini?
Kampuni ya king'amuzi cha continental nadhani mfunge hii namba ya huduma kwa wateja unapiga simu tena unalipia dk 15 husikilizwi? jamani hata ofisi zenu hapa Dar mahali zilipo ni kitendawili,utaizunguka masaki yote kuja ukapaona ni taabu sana, mnajificha kuna nini jamani? hata hii ofisi haina set up yaani yuko mtu mmoja hata ukiwa na shida anakuangalia kama mbuzi na gitaa,jamaniiiii hivi tumefikishana huko? hivi hawa ndo walioko peke yao sokoni? tcra natamani mchukue hatua,ukipata tatizo la kifundi hakuna huduma na zikiwepo utalipia na ukilipia subiri miezi kadhaa, nadhani wadau tujiunge tuwekeze hapa kwenye ving'amuzi la sivyo ni mapambano.......ukiona mtu kakwambia ukweli anakupenda la sivyo tungeondoka kimyakimya,,,,,lakn tunawapenda continental maana mko vizuri mnaposhindwa kutuhudumia nani atafanya kazi yenu? tcra wachunguzeni hawa mbona hawaeleweki kabisa? tunawapenda tunaogopa KUWAPOTEZA......