TBC1 poleni sana kwa jinsi Mkemia anavyozidi tu kuwadhalilisheni kwa gharama ya Mawingu!

Ikumbukwe kuwa Mkemia pia ni binaadamu kuna anachokipenda angekua mpenzi wa JF basi mngemuona akitoa comments zake na likes kwani unadhani GENTAMYCINE ukiwa Rais si utakua unaleta Mada zako km kawa Mwacheni bwanaa
 
Ni changamoto Kwa TBC ..Rais anawambia kimafumbo kuwa mbadilike. TBC hamna ubunifu..kipind chereko..kipind teknolojia inakuwa na mindset za watu zinabadilika mnabidi na nyie mbadilike. Miye siwez kununua king'amuzi niwaangalie nyie. Mkurugenzi wa TBC jua simu ya tatu ya Rais itakuwa kwako kukusimamisha.
Maisha yamebadilika na nyie badilikeni..Mara chereko, mwanazuoni..alafu Habari zenu zipo biased sana. Mnabidi mjiendeshe profit oriented siyo kusubili subsidies.

Dr. Ryoba mtaalamu wa makala..next time simu ya tatu ya Rais ni kwako kukutengua..Namsikia Nape mawinguni now yupo na wakina Btwangala.
Tido alileta ubunifu uka m cost
 
Tumube Waziri nape atupe ufafanuzi juu ya kedhia hii. Kama ikatokea ameshindwa kutoa majibu ya kuridhisha basi ajiuzulu
 
Jungu kuu ya TBC taifa wanajitahidi sana tofaiti na ndugu zao.
 
Nadhani sasa ni wakati muafaka wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuamua moja ama kubaki hapo TBC na kuendelea kujidhalilisha kama Mwana taaluma mbobezi wa Masuala ya Habari nchini Tanzania au aachane tu na hicho Cheo ili arudi kuendelea Kukufunzi, Kuandika, Kufanya tafiti na Kutoa ushauri wa Kitaalam.

Leo tena asubuhi nimemsikia mwenyewe tena mubashara kabisa Mkemia akipiga simu katika Mawingu na kuwapongeza tena kama kawaida yake kwa kazi nzuri wanayoifanya na nikajiuliza hivi ni kitu gani ambacho Mkemia amevutiwa nacho mno na Mawingu na ambacho hakipo TBC?

Ewe Mkurugenzi Mkuu wa TBC unaonaje labda ukimfuata Mkemia huko huko alipo sasa mapumzikoni ili umuulize anataka TBC iweje ili pengine mkifanyie Kazi ili asiwe anavutiwa na Mawingu na sasa awe anavutiwa nanyi TBC.

Binafsi nilijua kuwa Mkemia siku zote atakuwa namba wani fani wa TBC lakini kumbe wapi Mkemia ni nambari wani fani tena wa kindakindaki kabisa wa Mawingu kitu ambacho naona kama ni ajabu hasa ukizingatia Kiueledi na Kimfumo wa Kiserikali Mkemia ndiyo Mhariri Mkuu wa Vyomba vyote vya Habari vilivyo chini ya Serikali TBC ikiwemo.

Dkt. Ayub Ryoba jitathmini na TBC yako ila kama ni kukushauri tu basi nadhani ile Kalamu yako ya jicho la tatu na ule utaalam wako wa Kihabari tunauhitaji mno huku mitaani kuliko Wewe kuendelea kuwepo hapo TBC na kwa jicho la Kitaaluma kitendo cha Mkemia kila siku au kila mara kupiga tu Simu na kuwa pamoja na Mawingu huku akiwapongeza tena mubashara ni kama vile anakudhalilisha au anakuchora tu Wewe pamoja na Usomi wako wote huo mkubwa ambao hata Matajiri na Mabosi wote wa Mawingu wajikusanye na wajae ukumbi mzima wa Escape One hadi Two bado tu hawawezi kukufikia.

Nawasilisha.
Magufuli hana shida na TBC kisa kupiga simu Clouds TV kwasababu TBC ni moja ya Taasisi zake na unafanya kazi za umma.

Na Dr Rioba hana tatizo na kazi zake na kama kuna changamoto basi ni za kawaida kama Taasisi zingine.

Rais atazipigia simu Taasisi ngapi za umma kuanza kuzipongeza kila kukicha??

Mwacheni Dr Rioba afanye kazi kwa weledi wake kwa kufuata taratibu za Taasisi.

Clouds ni moja ya entertainment TV :D:D:D
 
Back
Top Bottom