Tbc one hii ni aibu kwa kweli........

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Jamani sina uhakika na hawa tbc one na jinsi wanavyoaandaa vipindi vyao
vya tv lakini kilasiku kuna makosa ya kipuuzi hadi unajiuliza
kama kuna watu serious pale....

Waliotazama taarifa ya habari ya jana tarehe 06/july saa mbili usiku

matakubalina na mimi kwamba hawa watu hawapo serious kabisa....

Yaani kwenye habari za kitaifa walionesha na kuripoti kuwa
ris wa brazil aemewasili tanzania na atakuwa mgeni rasmi
wa maonesho ya sabasaba leo tarehe 07/07...
Na oicha za tv zinamuonesha rais wa brazil amewasili airport darsalaam....

Sasa cha ajabu kwenye habari za africa mashariki tena wakaripoti
kuwa rais kibaki anampokea rais huyo huyo wa brazil kwa ziara ya siku mbili
nchini kenya.......yaani habari imetangazwa kama vile ni tukio la siku hiyo hiyo...

Nimebaki mdomo wazi na tbc one.........
 
Tatizo hilo la kweli, makosa huanzia kwa waandishi na kama wahariri hawakupitia vizuri taarifa hiyo basi ndo hayo uliyoyaona yanajitokeza.

Tatizo la taarifa ya Rais wa Brazil kuwasili nchini na wakati huohuo kuwa atapokelewa na Rais Kibaki ni la Mpangilio ambayo wa kulaumiwa ni mhariri aliyepanga na si mtangazaji kwasababu yeye analetewa labda alichopaswa kufanya ni kurekebishia hewana kama naye alipitia kabla ya kuingia studio.

Jambo la Msingi hapa kinachoonekana pale waandishi wa TBC wanajiona wako juu ya wenzao wa vyombo vingine kwahiyo wanasahau mambo ya msingi kikazi hadi taarifa ya habari wanasoma kama vile Clause FM wanavyofanya, hawajui kuwa ile ni chombo cha Taifa. Zamani RTD ilikuwa inaajiri waliofunzwa pale lakini siku hizi kujuana bwana, mtu analeta kijana wake aajiriwe, wanasiasa nao wasumbufu nasikia ikitanagzwa ajira wanapeleka watoto na vimemo hata wasipokuwa na uwezo wataajiriwa.

Naomba kuwasilisha wana jamii.
 
Pole lakini kwa Tanzania our (Public Broadcaster) yaan Tanzania Broadcasting Corporation remain so far the best! Again I compare with local broadcasters.
 
Pole lakini kwa Tanzania our (Public Broadcaster) yaan Tanzania Broadcasting Corporation remain so far the best! Again I compare with local broadcasters.

Hatakama lakini uzembe uwezi kuufumbia mcho kwani kunasiku itatokea kitu kinatangazwa na mtangazaji na wakati huo mtangazaji mkonaye baa nayeye anatazama Taarifa ya habari!!Pili jamani mimi sielewi nikwani hawarekebishi speedya sauti iendane na speed ya picha maan sasa nimda mrefu mtu anakuwa anamalizakuongea after 2esc sauti inamalizia kuongea!!
 
Not to excuse TBC, lakini juzi nilikuwa naangalia CNN hii hapa transcript kutoka kwa Soledad O'Brien on Anderson Cooper's 360, this chick is supposed to be really smart, Harvard grad and all

CNN.com - Transcripts

Was it hot where you were today?

O'BRIEN: Yes.

MYERS: Eighty-six right now in New York, 88 in Philadelphia.

And the queen is coming to New York tomorrow. It will feel like 101 for her.

O'BRIEN: Ooh. We're so sorry, Your Royal Highness.

I guess you could say this was off the cuff, but still...
 
Pole lakini kwa Tanzania our (Public Broadcaster) yaan Tanzania Broadcasting Corporation remain so far the best! Again I compare with local broadcasters.

...aahuh, kumbe kuna nia na haja ya kujiangalia na kujilinganisha na local competitors?? Slightly out of topic, but remember the controversial Samba Boys vs Taifa Stars... was it necessary then? Unapokuwa Public Broadcaster na kujilinganisha na local private outlets, ni mizani gani hiyo unakuwa unatumia?! Won't it be just as wise to once admit failures and strive for improvement Ndugu Kasheshe?!
 
Not to excuse TBC, lakini juzi nilikuwa naangalia CNN hii hapa transcript kutoka kwa Soledad O'Brien on Anderson Cooper's 360, this chick is supposed to be really smart, Harvard grad and all

CNN.com - Transcripts



I guess you could say this was off the cuff, but still...

Ooh pole to Her Majesty !!!!! lol
 
Wana JF,yaani mumeona hayo tu toka TBC!!!!!!!! Mimi nadhani mkuu TM amepoteza ile haiba na taaluma aliyokuwa nayo kule BBC.
1. TBC imekuwa ikitangaza habari za CCM kwa muda mrefu kila siku,taarifa za akina CHADEMA na CUF ni by the way,funika kombe.
TM amesahau kuwa TBC inaendeshwa na Kodi za watu wote na mshahara wake unatoka kwa kila mtu wa CCM,CUF,CHADEMA na hata wapiga madogoli.

2. TBC inapata ruzuku ya serikali kwanini iingiie katika ushindani wa kibiashara na private firm! hapa kuna level field kweli.
3. Wameng'ang'ania world cup wapewe market exclusivity, wakasubiri wiki moja kabla wakasema eti kutokana na bunge itabidi mechi zingine zionyeshwe TBC2, kwahiyo watu wanunue ving'amuzi [decorder]. Hapa masikini wa vijijini waliokuwa wanaonyeshwa mechi bure kupitia ITV,DTV,STAR TV ikawa ndio basi. TM kafanya biashara na sina uhakika kama 10% haikutumika.
Ukweli ni kuwa wale wa mikoa ya pembezoni tulisahau TBC tukawa na KBC,UTV etc. Wafanyabiashara kama mlijua mnatangaza biashara basi ni kwa kakundi kadogo tu.

Mnyonge myongeni lakini haki yake mpeni, ITV ilitusaidia sana! kule vijijini walituwekea japo TV viwanjani tukawa tunafaidi huduma. Sasa TM na ruzuku zote tabu tupu
 
sijui ,siwezi kuunga mkono sana hoja kwani si mpenzi wa tbc.lakini nadhani labda rais wa brazil anaweza kufuingua maonyesho mchana kisha akaenda nairobi jioni na akapokewa rasmi,yote si fungu lipo bwana na viongozi wetu hawana kazi ya kufanya.usishangae kikwete akaenda brazil na akapokewa na maximo.
 
Hatakama lakini uzembe uwezi kuufumbia mcho kwani kunasiku itatokea kitu kinatangazwa na mtangazaji na wakati huo mtangazaji mkonaye baa nayeye anatazama Taarifa ya habari!!Pili jamani mimi sielewi nikwani hawarekebishi speedya sauti iendane na speed ya picha maan sasa nimda mrefu mtu anakuwa anamalizakuongea after 2esc sauti inamalizia kuongea!!
esp msoma habari za biashara always anapishana na sauti.
 
......nipo Tanzania (Tanga) lakini naangalia TBC mara chache chache sana maana ni upuuzi kwenda mbele! angalieni yale maandishi yanayopita kwa chini wakati wa taarifa ya habari, ni typing errors kibao tena kila siku!!! TM kwishnei!
 
kwakeli inaboa asaswala la sauti mara nyingi kwenye taarifa ya habari yanatokea sana
 
Mwanamke anapokuwa mchafu, mumewe ndio anapata kero zaidi kuliko nyie watu "baki". Mimi nilishawahi kuwa ndani ya TBC na kujua uchafu wake wa nguo za ndani, achilia nyie mnaongalia sketi na blauz.

Kwa kifupi, hali ni mbaya na inasikitisha. Hayo mnayoyaona ni madogo tu.

Hivi unajua kuwa kuna vipindi vingine kunakuwa hakuna "Camera man"? Ukiuliza nao wanashangaa eti "He, kwani hakuna mtu kwenye camera?" Mungu atusaidie na uzembe wetu!
 
Back
Top Bottom