Elections 2010 TBC na Daily News kuisusia Chadema, ni baraka na neema kwa Dr Slaa.

Uh, Ufisadi unamaliza watu, karne hii unatetea CCM na makada wake?

Watetezi wa ufisadi bora mmezaliwa baada ya uhuru kwani mgetucheleweshea UHURU wetu
 
Huruma yangu ni kwa Tido na Mkumbwa wa TSN kwani ajira yao itaishia 31.10.2010 baada ya Rais mpya kuingia madarakani. Yeye ndiye anayewateua na kwa umakini wa Dr hawezi kuweka viongozi wanaopelekwa puta na mafisadi kuongoza vyombo muhimu vya umma kama TBC na TSN. Tido aliyejijengea heshima BBC ndio huyohuyo aliyejishushia heshima TBC. Pole sana Mgosi kwa kuharibu heshima yako uzeeni,ungejifunza kutoka kwa wenzio ambao umri unavyo kwenda ndivyo heshima inavyoongezeka.
 
Shida kubwa ya watendaji wetu wengi ni wanafiki. anaangalia upepo wa kula yake unaendaje ndo atategesha huko, we angalia Tido alivyomuhojo Lowassa na hizi habari za Daily News. they always want to show the fisadis kwamba bado wanawaunga mkono. wanasahau nguvu ya umma huwa haishindwi.

Ole nasema ole wao
 
Wewe ukisoma Daily News unasoma habari za Richmond, Chadema na CCM tu? Inawezekana ndiyo maana mnakuwa too local in thinking. Fungua daily news kwenye ma-news juu ya ma-news yaliyopanda juu, kurasa za business news na sports international; uncomparable in East Africa. Hizi habari za Chadema, CCM, richmond, Silaha (slaa) unaweza zipata hata kule kwenye udaku; uwazi et al. (Shigongo).

Haya ni mawazo mgando!

Kwamba habari za kisiasa za hapa kwetu ni swala la kidaku!:nono: .............OK! OK!
 
Hotuba ya Kikwete Pale NEC Dodoma Haikustahili kurushwa na TBC1 live, pale Kikwete hakuwa kama Raisi alikuwa ni kama Mwenyekiti wa Chama, uzito wake Haukuwa na Tofauti na Lipumba, Mbowe, Mtikila< Mrema ama Cheyo, kama Kikwete alipewa zaidi ya masaa Mawili basi pia ilikuwa ni haki ya Vyama vyote kupewa muda huo

Tatizo kubwa la Tanzania ni kuchanganya Siasa na Mambo Mengine ya Maendeleo, na Mambo ya kiserikali, Tido amejisahahu ama anafanya makusudi ya kutokujua kwamba anatumia rasilimali za wananchi vibaya ama kwa maslahia ya CCM, hicho ni chombo cha Umma, Huwezi kutokuweka habari za dokta Slaa ama Kiongozi yoyote mwenye kutambulika kiserikali, na hilo sidhani kwamba ni ombi bali hilo ni jukumu lao na ni wajibu wao kufanya hivyo

hivi itakuwaje pale Slaa atapokuwa tayari kuapishwa, Watamtangaza ama?
 
Wakubwa
mngeona jana jinsi TIBISII ilivyotoa muda mwingi kwa habari ya Rungwe kuchukua fomu ya kugombea uraisi kupitia NCCR, inaleta mashaka kidogo. Mambo ya Chadema kimyaaa!

Nguvu ya umma itashinda tu!
 
Mag3,

Hiyo DAILY NOISE ni gazeti ambalo lilitakiwa lisifungamane na upande wowote lakini halifanyi hivyo. Mhariri wake anajikomba kwa CCM.

Kama ulivyosema, no ammount of bootlicking will stop this tsunami. Gazeti la Tanganyika Standard halikuweza kumzuia Mwalimu asitukomboe. Hili la Daily News ambalo ni mrithi wake halitaweza kumzuia Slaa asitukomboe toka makucha ya CCM.

Maombi yangu kwa WANACHADEMA wa Dar ni kwamba wajipange kisawasawa wampe Mpendwa wetu Dr. Slaa mapokezi ya nguvu atakaporudi. Na asirudi bila maandalizi ya mapokezi makubwa kufanyika.

I will be there kumpokea mkombozi wetu, no matter what!
 
Kwa siku ya pili mfululizo gazeti la Umma la Daily News limeamua kumsusia Raisi Mtarajiwa Dr. Slaa kwa kutoandika lolote linalohusiana na uamuzi wake wa kuchukua fomu kugombea Uraisi kupitia Chadema. Ikumbukwe kuwa Daily News imewahi kuwapa coverage Lipumba wa CUF, Hashim Rungwe na Fausine Sangura wote wa NCCR- Mageuzi, Mutamwega Mugahywa wa TLP na Kikwete wa CCM. Kwa kuwa kati ya hawa wote mwenye nafasi kubwa ya kuutwaa Uongozi wa nchi ni Dr. Slaa wa Chadema, sasa tendo la hivi vyombo vya Umma tuvitafsiri vipi kama si mbinu za kuhujumu haki za msingi za raia katika kuchagua na kuchaguliwa.

Leo tena nawaletea habari zilizopewa umuhimu katika gazeti la Daily News.

  • Chadema & DP yet to sign election code of ethics
  • AU mulls use of DDT to fight malaria
  • Water shortage haunts Bukoba municipality
  • Transporter sues insurance coy 153m/-
  • Government set to address language barrier in education
  • Higher education loan repayment promising
  • Mtikila wants High Court to disqualify Magistrate Dudu
  • AMWA mourns deaths of two women journalists
  • Hearing of Richmond case set for Sept 23
  • Bandits abandon gun at Mbinga school
  • Tamisemi beaten by Police
  • Mrs Sitta in PCCB dragnet
  • NGO to meet institutions leading graft
  • Dull day one for Tanzanian athletes
  • State stresses use of local currency
  • Presidential fund to review loans schem
Mpaka lini sisi wananchi tutaendelea kufumbia macho vitendo hivi vya ukiukwaji wa haki na upendeleo wa wazi wazi wa hivi vyombo vinavyoendeshwa kwa kodi zetu ?
 
Mpaka lini sisi wananchi tutaendelea kufumbia macho vitendo hivi vya ukiukwaji wa haki na upendeleo wa wazi wazi wa hivi vyombo vinavyoendeshwa kwa kodi zetu ?

Tido Mhando na Mkumbwa wameamua kutumia vibaya madaraka waliyopewa. Hiyo ni aina ya ufisadi. Ikiendelea hivi basi wananchi wanaweza kuanza kuwazomea mitaani "Fisadi Mhando! Fisadi Mkumbwa!"

Hata hivyo, Tido Mhando na huyo Mkumbwa kuficha umaarufu wa CHADEMA hakutazima vugu vugu la mabadiliko la wakati huu. Tumevumilia vya kutosha. Tumetawaliwa miaka 50 na watu wale, bila mafanikio. Sasa tunataka kubadilisha chama tawala.

Yaani Mkumbwa na Tido Mhando wanataka CCM iendelee kututawala miaka 5 mingine tena? Si tutakufa! Hawaoni tulivyochoka?
 
Maana ya TBC nini? na Nani alianzisha Serikali au Mtu Binafsi??? Kama Serikali zimetumika Kodi zetu na Pia KOdi za Dr. SLaaa sasa iweje? TUBADILIKE
 
Hilo la raisi wetu matarajiwa Dr.Slaa walilitangaza wapi na muda gani? Nyamungo tuhabarishe labda wenzio tuliupitiwa!

Wametangaza leo asubuhi, nafikiri bada ya kuona hii thread. Wametangaza story ya Slaa alipotua huko kwao lakini with anegativity kwamba alitumia lugha ya kwao! TBC bure kabisa
 
Ipo wakati watalazimika tu kumwandika na kumtangaza tu Daktari Slaa..Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 1985 itawabana tu kufanya hivyo. Kama hawataki, waendelee kutumika kwa ajili ya CCM, vipo vyombo kibao binafsi ambavyo ndivyo vinavyoaminika kwa habari za uhakika na ndivyo vinavyoheshimika pia na wanachi wengi. CHADEMA ikiingia Madarakani, hivyo vyombo vitaendelea kuwa vya UMMA wa watanzania si vya CCM.
 
Wewe ukisoma Daily News unasoma habari za Richmond, Chadema na CCM tu? Inawezekana ndiyo maana mnakuwa too local in thinking. Fungua daily news kwenye ma-news juu ya ma-news yaliyopanda juu, kurasa za business news na sports international; uncomparable in East Africa. Hizi habari za Chadema, CCM, richmond, Silaha (slaa) unaweza zipata hata kule kwenye udaku; uwazi et al. (Shigongo).
Wewe lazima utakuwa ndiye DERE NYUZI MKUBWA...........
 
Back
Top Bottom