Tatizo la umeme Tanzania, je ahadi ya Waziri mkuu ilikuwa hewa?

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,093
Jana baadhi ya waandishi wa habari walitembelea Songosongo ili kujionea uzalishaji na usafirishaji wa gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme. Mojawapo ya taarifa zilizotolewa ni kwamba kwa sasa gesi inayofikishwa Dar es salaam haitoshelezi hata mitambo ya Songas ya sasa. Wiki iliyopita Waziri mkuu alitoa ahadi ya kutatua tatizo la umeme kufikia mwezi wa nane kwani tayari mitambo ya gesi ya kuzalisha MW100 imeagizwa, sasa napata taabu kidogo hapa.....................Je kuna uhalisia wa dhamira katika hili?
 
Ni basi mkutano wa bunge umeisha, Lema angeuliza tena mwongozo wa spika inakuwaje Waziri mkuu anapoliongopea bunge kwa mara ya pili.
Hivi Makinda alisahau kutoa mwongozo kwa Lema hata baada yakupewa ushahidi au alifanya kumpotezea.
 
hao ndio mawaziri wa serekali yetu usiumiize kichwa kuwaamini !
 
Leo ni tarehe 31, siku ambayo Megawats Ngeleja alisema mgao utaisha. Mbona bado kuna giza? Mgao hadi lini ndo uishe?
 
Leo ni tarehe 31, siku ambayo Megawats Ngeleja alisema mgao utaisha. Mbona bado kuna giza? Mgao hadi lini ndo uishe?
<br />
<br />
Sasa hivi wamekuja na mbinu mpya, hakuna kukata umeme wala nini! Sasa hivi mgao ni Mtindo wa "Luku network probem".
Mtajibeba!
 
Huo ni uongo wa WM maana hata Spika angemwambia tu afute kauli labda "angemshepu" ili sikunyingine asirudie kusema uongo, lkn kwa kuwa aliipotezea hoja ya Mhe. Lema sasa WM anaona anayohaki ya kuropoka uongo bungeni, ataendelea hivi hadi wadanganyika tutakapo amka kutoka usingizini na tukapoweza kuona hata kwenye mwanga huu wa jua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom