tatizo la umeme dar

Wala si kwenu tu watu msasani, nafikiri ni Dar nzima. Kwa mfano kwetu ishajulikana kuwa siku za j'mosi na j'pili umeme unazimwa, na kweli leo umezimwa mapema tu. Ukizingatia kuwa kupatikana maji maeneo mengi ya Dar kunategemea umeme, basi imekuwa shida. Usipowahi kabla ya saa 3 asubuhi unaweza kukosa na maji pia. Kazi kweli kweli!
 
Poleni sana. Hakuna kitu ninachochukia kama kukosa maji na umeme kunakosababishwa na uzembe wa vyombo husika na serikali. Kukosekana hivi vitu kunakosesha raha sana.
 
usipime si kwenu tu kwetu ni kila siku na kila wakati sisi tumesha zoea hapa ustawi tunashindwa hata kusoma kagenerator kakizimwa basi na inavyo onekana bosi mkuu wa tanesco naona madaraka kuliko hata waziri alisema tutakaa gizani na ndo analolifanya,manake ye waziri alisema hatuwezi kuwa gizani,lkn tupo gizani sasa nani boss hapo?
 
Mike 1234, sio kuwa nani boss kuliko mwenziwe baina ya Waziri na boss wa Tanesco.

Tanesco ndio wanaojuwa hali halisi ya umeme walionao. Sasa kama Bunge limepiga stop, basi kwanza tupewe taarifa ya huko kukosekana kwa umeme ili tuweze kutathmini na kujuwa sababu ya kutokuwapo kwa umeme.

Hayo ni majukumu mazito na nyeti kwa wakuu. Kiurahisi tunaweza kulaumu Tanesco lakini sababu inawezekana ikawa sio wao bali ni Bunge kuingilia kazi za kiutendaji.
 
Back
Top Bottom