Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,668
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
---JF Doctor na wapendwa wengine,
Hivi ninapoandika niko katika nchi yenye baridi kali sana inayoambatana na barafu. juzi usiku nikiwa nimelala nikaota ndoto iliyonishtua usingizini na nikajikuta nimejaa wasiwasi na papo hapo jasho jingi likaanza kunitoka.
Japo si mara yangu ya kwanza kupatwa na hiki kitu lakini safari hii nimelazimika kuuliza kwa daktari kwa sababu jasho lilikuwa jingi kupita kawaida na hasa ukizingatia kuwa kwa baridi ya huku wakati huu, sikutegemea kabisa kutoka jasho jingi kiasi hicho hata kunilazimu kufikiria kuoga kabla sijarudi tena kitandani kulala.
1. Je, mtu kutoka jasho jingi akiwa na wasiwasi kunasababishwa na nini?
2. Je, kuna hatari yoyote ya kiafya kwa hali kama hii na hasa kama inampata mtu mara kwa mara?
naombeni msaada wa elimu wapendwa
Mungu awabariki sana
Merry Christmas and Happy New Year 2012!!
---Heshima mbele wandugu,
Nimekuwa na tatizo la kutoka jasho sana kila wakati hata kama hali ya hewa ni ya kawaida, tunapokuwa na wenzangu wao wanakuwa katika hali ya kawaida, lakini mimi nakuwa nasikia joto sana na natokwa na jasho jingi, hali hii imekuwepo kwa muda mwingi sasa.
Naomba msaada kwa anaefahamu, kama ni mwanzo wa tatizo gani na nifanye nini.
Wasalaam.
Habari zenu ndugu zanguni.
Nina mtoto mwenye umri wa miaka mitatu. Mtoto huyu amekuwa akitokwa na jasho jingi iwe asubuhi, mchana, jioni hata usiku. Akila anatokwa na jasho. Akilala jasho linammwagika na akilia pia jasho linamfumuka.
Hata kama ni kipindi cha baridi yeye huwa anatokwa na jasho.
Mtoto huyu si mlaji sana ila ni mnywaji sana wa maji.
Je, hali hii ni kawaida au kuna tatizo? Nini chanzo?
UFAFANUZI WA JUMLA WA TATIZO HILI
Tatizo la kutokwa ana jacho mwilini, mikononi na miguuni:Ugonjwa huo unaitwa HYPERHIDROSIS.
Kawaida tunatoka jasho ili kuupoza mwili.Mwili unapokuwa na joto nervesystem inatuma ujumbe automatic kwenye sweatglands ili kupunguza joto.Unapokuwa na hyperhydrosis hizi nervesystem zina kuwa zinafanya kazi pasipo na mpangilio na zinatuma ujumbe wakati wote kwahio jasho linatoka hata kama mwili hauna joto.
Hali hio pia inaweza kusababishwa na mtu kuwa na sukari ya chini,hyperthyroidism au side effects za dawa.
Zipo njia tofauti za kutibu kama.
- Aluminium chloride solution ambayo unaweka kwenye viganja vya mikono na miguu.
- Potassium permanganate.
- Nimeshawahi kuona botox ikitumika pia lakini ni tiba ya muda hali hio hujirudia.
- Iontophoresis:Njia inayotumia kupitisha maji chini ya ngozi kwa kutumia umeme.
- Upasuaji kwenye nerve ambazo zinahusika na jasho.
zinatumika!
UFAFANUZI WA TATIZO HILI ULIOTOLEWA NA WADAU
---Hyperhidrosis ni ugonjwa wa kutokwa na jasho jingi kuliko kawaida. Kutokwa na jasho ni hali ya kawaida kwa binadamu na wanyama na kazi kubwa ya jasho ni kupoza mwili unapopata joto kubwa. Kwa kawaida mwili wa mwanadamu hutengeneza wastani wa lita moja ya jasho kila siku.
Kiwango cha jasho huweza kutofautiana kutokana na mazingira na hali ya mwili kwa mfano kipindi cha joto ama maeneo yenye joto kali, au kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia hufanya mwili kutoa jasho jingi zaidi ya kawaida ili kupooza mwili.
Ugonjwa wa hyperhidrosis hutokea pale mwili unapotengeneza jasho jingi zaidi ya linalohitajika kupoza mwili. Mfano ni kutoka jasho ukiwa umepumzika sehemu isiyo na joto au kutoka na jasho jingi unapoingiwa na hofu nk
Kitaalamu ugonjwa huu umegawanyika katika makundi mawili. Kuna primary hyperhidrosis na secondary hyperhydrosis. Primary hyperhydrosis huanza mara nyingi kipindi cha balehe na husababishwa na urithi wa vinasaba (genetics). Secondary hyperhidrosis huanza kipindi chochote cha maisha na husababishwa na magonjwa mengine ya mwili mfano kisukari, magonjwa ya tezi ya shingo na kadhalika.
Hyperhydrosis ni kilema kilichojificha
Mgonjwa wa hyperhidrosis hupata shida kuendana na shughuli za kawaida za maisha. Wengi hupatwa na aibu pindi jasho jingi linapolowanisha nguo au kushindwa kushikana mikono pindi viganja vinapolowa jasho jingi. Pia kuna baadhi ya shughuli humwia vigumu mfano jasho jingi mikononi husababisha ugumu wa kushika vifaa kipindi cha kazi. Ugonjwa huu huweza kusababisha msongo wa mawazo.
Tiba
Kuna tiba mbalimbali ya ugonjwa huu. Secondary hyperhidrosis hutubiwa kirahisi kwa kutibu ugonjwa unaosababisha secondary hyperhidrosis kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa hiyo ni muhimu kumuona daktari pindi unapopata na tatizo hili na kufanya vipimo ili kugundua magonjwa sababishi mfano kisukari na Magonjwa sababisha yakitibiwa na ugonjwa huu huisha mara moja.
Nitazungumzia zaidi primary hyperhidrosis ambayo husababishwa na vinasaba. Tiba yake nimeigawanya mara tatu. Kwanza ni kubadili mfumo wa maisha, pili ni dawa na tatu ni upasuaji.
Tukianza na kubadili mfumo wa maisha. Mgonjwa mwenye hili tatizo yampasa kubadili mfumo wake wa maisha ili kuendana na tatizo.
Kwanza inashauriwa kunywa maji mengi. Maji husaidia kupoza mwili na hivyo kupunguza kutokwa kwa jasho. Pia inashauriwa kupunguza vyakula vyenye viungo vingi, vinjwaji kama kahawa, pombe, sigara na vinywaji vichangamfu(energy drinks) maana vyakula na vinywaji hivi husababishwa mwili kutengeneza jasho.
Pia inashauriwa kuoga angalau mara mbili kwa siku kwa kutumia maji safi na sabuni yenye dawa mfano dettol.
Pia paka baking soda sehemu zinazotoa jasho jingi pindi tu umalizapo kuoga. Baking soda huharakisha kukauka kwa jasho kwa sababu ya alkalini iliyonayo.
Tumia vitoa harufu (antiperspirants/deodorants) vyenye aluminium chrolide ambayo huharakisha kukauka kwa jasho.
Tumia vikinga jasho (sweat pads) sehemu zinazotoa jasho jingi mfano sehemu za kwapa na kadhalika. Unaweza kununua vikinga jasho madukani au kutengeneza mwenyewe nyumbani kwa kutumia nguo na sponji na kuvaa ndani ya nguo.
Pia chai ya mmea uitwao salvia officinalis usaidia kupoza mwili na inashauriwa kunywa kwa watu wenye tatizo hili.
Kwenye upande wa dawa, dawa ziitwazo kitaalamu anticholinergic husaidia wenye tatizo la kutokwa na jasho hasa wanaopata tatizo hili wanapoingiwa na hofu ya kitu fulani.
Pia kwenye nchi zilizoendelea huduma ya upasuaji hutumika kwa wenye tatizo kubwa ambalo haliwezi kutibika kwa njia nyingine. Tiba hii inajumuisha kuingilia na kufunga kwa njia ya upasuaji mifumo ya fahamu inayosababisha kutoka kwa jasho.
Ukiachana na upasuaji, tiba ya kubadili mfumo wa maisha na dawa husaidia kwa kiwango kikubwa kwa mazingira yetu hapa Tanzania.
Dr Luhaja Nginila, MD
---Wasi wasi na hofu husabaisha mwili kutoa adrenaline hormone, ambayo husabaisha shinikizo la damu (BP) kuongezeza, na basal metabolic rate (BMR) pia huongezeka mwili hutoa joto jingi sana kutokana na kuongezeka kwa BMR, hiyo taarifa hupelekwa kwenye ubongo , na ubongo unatuma taarifa kwenye tezi za jasho ( sweat glands) jasho hutoka ili kuupoza mwiliendapo hii itajirudia mara kwa mara huweza kusabisha High blood pressure, stroke, heart attack na hata sudden death.
Ni vizuri kufanya uchunguzi zaidi na kuizuia hii hali isijirudie.
---Nimonia esinofili (EP) ni ugonjwa ambapo aina fulani ya seli nyeupe za damu ziitwazo eosinofili hukusanyika kwenye mapafu. Seli hizi husababisha kuvurugika kwa nafasi za kawaida za hewa (alveoli) ambako oksijeni huzinduliwa kutoka kwa anga. Aina mbalimbali za nimonia esinofili huwepo na zinaweza kutokea katika kundi la umri wowote. Dalili zinazojitokeza sana sana ni pamoja na kikohozi, homa, tatizo la kupumua, na kutokwa na jasho usiku. EP hutambuliwa kwa kutumia mchanganyiko wa dalili mbalimbali, matokeo ya ukaguzi wa afya unaofanywa na mtoa huduma za afya, na matokeo ya vipimo vya damu na eksirei. Ubashiri huwa bora wakati sehemu kubwa ya EP imetambuliwa na matibabu kwa kutumia kotikosteroidi yameanzishwa.
Aina za nimonia esinofili
Ugonjwa wa nimonia esinofili umegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na kama kisababishi kinaweza kutambuliwa au la. Visababishi vinavyojulikana ni pamoja na baadhi ya dawa au vichochezi vya kimazingira, maambukizi ya vimelea, na saratani. EP pia inaweza kutokea wakati mfumo wa kinga umeshambulia mapafu, ugonjwa uitwao tatizo la Churg-Strauss. Wakati kisababishi hakipatikani, EP hupachikwa jina la "idiopathiki." EP ya idiopathiki inaweza kugawanywa katika "nimonia esinofili kali" (AEP) na "nimonia esinofili sugu" (CEP) kulingana na dalili ambazo mtu anapata
Dalili[hariri
Visababishi vingi vya nimonia esinofili vina dalili zinazofanana. Kikohozi, homa, kuongeza kwa tatizo la kupumua, na kutokwa na jasho usiku ni dalili maarufu na hujitokeza kwa karibu kila mtu anayeugua. Nimonia esinofili kali kwa kawaida huendelea kwa kasi sana. Homa na kikohozi zinaweza kutokea wiki moja au mbili tu kabla ya matatizo ya kupumua yameendelea na kufikia hatua ya kushindwa kupumua hivyo basi kuhitaji uingizaji hewa kwa kutumia mitambo. Nimonia esinofili sugu kwa kawaida huendelea polepole. Dalili hujilimbikiza katika kipindi cha miezi kadhaa na huwa ni pamoja na homa, kukohoa, tatizo la kushindwa kupumua, kukorota, na kupungua kwa uzito. Watu walio na CEP mara nyingi hupatikana kuwa na pumu kabla ya CEP hatimaye kutambuliwa.
EP inayotokana na dawa au vitu mbalimbali kwenye mazingira ni sawa na hutokea baada ya kufichuliwa kwa kitu kinachojulikana kusababisha. EP inayotokana na maambukizi ya vimelea ina dalili za mwanzo pamoja na dalili nyingi tofauti zinazohusiana na aina mbalimbali za vimelea vya msingi. EP katika mazingira ya saratani mara nyingi huendeleza katika muktadha wa utambuzi unaojulikana nwa habari ya uvimbe wa kansa, kansa ya kizazi, nk.
Kumekuwa na matukio ya nimonia esinofili kinachosababishwa na madawa kama vile daptomycin (Cubicin). Mbili za kesi hizi zimebainishwa kuwa kesi sugu zinazotegemea steroidi. (Rejea Clinically Infectious 2010:50 (1 Machi) pp735-739.
Chanzo: Nimonia esinofili - Wikipedia, kamusi elezo huru
===Kutokwa na jasho ni njia mojawapo ya mwili kutoa taka na pia ni mfumo unaotumiwa na mwili ili kuupooza pale hali ya hewa au joto la mwili linapokuwa lipo juu.
Katika hali ambayo ni ya kawaida, mwili hutoa jasho baada ya mtu kufanya shughuli fulani ya kufanya joto lake lipande na ili kuliweka katika kiwango cha kawaida, mtu atatokwa na jasho, au yawezekana ikawa siyo kufanya kazi, bali kutokana na mtu kuwa na msisimko fulani, basi jasho linaweza kumtoka.
Kuna baadhi ya watu mpenzi msomaji, ambao mbali na sababu hizo hapo juu, huwa wanatokwa na jasho jingi bila ya kujali kama mtu huyo kakaa amepumzika, hana msisimko wowote, hali ya hewa kuwa nzuri bila joto, yaani haijalishi, wao hutokwa na jasho jingi muda wote. Hili ni tatizo kiafya ambalo kwa kitaalamu hujulikana kama, Hyperhidrosis.
Mpenzi msomaji, baadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kumfanya mtu apate au awe na tatizo hili la kutokwa na jasho jingi muda wote ni haya yafuatayo:
Pamoja na tatizo hili kuwa gumu kitaalamu, mambo ambayo huhusishwa na tatizo hili ni matatizo ya neva zinazohusiana na glandi za jasho katika mwili na kuzifanya glandi zifanye kazi zaidi ya inavyohitajika, pia tatizo hili huhusishwa na kurithi.
Mambo mengine ambayo husababisha tatizo hili ni matumizi ya baadhi ya dawa, mfano dawa za kuondoa msongo wa mawazo, dawa za kutibu matatizo ya kansa, dawa zinazotumika kutibu magonjwa ya uzazi.
Kuna baadhi ya magonjwa ambayo pia humfanya mtu apate tatizo hili, mfano kifua kikuu, Parkinson, matatizo ya glandi (Over active thyroid gland.
Pia kwa watu wazima na hasa wanawake, hukumbwa na tatizo hili pale umri wao wa kuzaa unapokuwa umeisha (Menopause).
Mpenzi msomaji, ni vyema kama unalo tatizo hili ukawaona wataalamu wa afya ili kuweza kupata msaada unaostahili. Neva zinazotawala glandi za jasho hutumia kemikali asilia mwilini inayojulikana kwa jina la Acetylcholine, na kemikali hii pia huhusika katika mifumo mbalimbali mwilini. Kwa bahati mbaya, dawa zinazotibu tatizo hili huzuia utendaji kazi wa kemikali hii asilia na hivyo, baada ya mtu kutumia dawa huweza kupata madhara kama vile mdomo kuwa mkavu sana na matatizo katika kukojoa.
Chanzo: Tanzlife Company Limited
USHAURI WA NAMNA YA KUTIBU TATIZO HILI
Tiba mbadala ya kutokwa na jasho lisilo la kawaida, kwapani, usoni, viganjani n.k Mwili wa binadamu hutoka jasho fulani jingi ukiwa upo katika mazingira ya jotoridi lililozidi kiwango, mwili unapokuwa katika kiwango fulani cha shughuli ya kukufanya utokwe jasho zaidi na wakati mwingine ukiwa na stress ya jambo fulani.
Sasa jasho linapotoka muda wowote bila activity, stress wala joto kuwa jingi basi kuna hitilafu.
Kitaalam hali hii ya kutokwa jasho kusiko kawaida kwa lugha ya kiingereza wanaita hyperhidrosis, hali hii huathiri baadhi ya maeneo mwilini hasa hasa usoni, kwapani, viganjani na kwenye nyayo.
Wataalam wanasema tatizo hili ni kijenetiki yaani linaweza kurithiwa. Tatizo la kutokwa jasho huchangiwa na overactivity kwenye neva jambo linalosababisha kutrigger tezi jasho.
Vichochezi ni pamoja na, matumizi ya madawa fulani fulani, kitambi, madawa ya kulevya ikiwemo pombe, kiwango cha chini cha sukari, malaria, kifua kikuu, shinikizo la damu na upungufu la virutubisho mwilini.
Tatizo la kutokwa jasho jingi humfanya mhusika ajisikie aibu na wakati mwingine mfadhaiko, wasiwasi na kujitenga, habari nzuri ni kuwa zipo tiba mdabala zinazopatikana kwa unafuu na urahisi ambazo mhusika anaweza kutumia nyumbani na kuondokana na kutokwa jasho jingi iwe viganjani, usoni, kwapani ama kwenye nyayo za miguu.
APPLE CIDER VINEGAR
Hii hupatikana madukani, mini supermakets ama kwenye supermarkets. Inafanya kazi kwa ufanisi kushughulikia tatizo la kutokwa jasho sababu ni kituliza nafsi cha asili kabisa,
Unaweza kuchagua kati ya yafuatayo:
1.Safisha eneo linalotokwa jasho kisha tumia pamba ama kitamba kisafi cha pamba kupaka apple cider vinegar kwenye hilo eneo, iwe viganjani, kwapani, nyayo ama usoni iache usiku mzima ( kama una ngozi sensitive na changanya maji na apple cider vinegar viwango sawa) baada ya kuoga asubuhi paka baby powder kwenye hilo eneo.
2. Changanya viwango sawa vya apple cider vinegar na maji ya uaridi ( Rosewater) na kupaka eneo linalotokwa jasho jingi, mara 2 hadi 3 kwa siku.
3.Tengeneza mchanganyiko wa wa apple cider vinegar kijiko 1 ama 2, asali mbichi kijiko 1 na maji vuguvugu glasi moja kunywa mara mbili kwa siku.
Apple cider vinegar ina manufaa mengi kiafya na pia inapambana na kitambi.
WANGA WA MAHINDI
Tiba Mbadala nyingine ni wanga wa mahindi, wanga wa mahindi unaweza kuutengeneza mwenyewe kutoka kwenye unga wa mahindi, ama kununua sokoni changanya viwango sawa vya wanga wa mahindi na baking soda, weka kwenye chupa ya powder, itumie kama powder maeneo yanayotoka jasho jingi.
MALIMAO
Malimao yapo masokoni na wengine wamepanda majumbani, ni tiba asilia ya majasho yanayotoka kwa wingi na pia inafukuza backteria wabaya, iko hivi
1.Kamua limao moja na lichanganye na baking soda vizuuri, futa jasho kwenye maeneo husika kisha paka, subiri dakika kumi ukiwa umepaka kisha safisha maeneo husika, fanya hivi mara moja kwa siku
2.Ama unaweza safisha maeneo husika chukua kipande cha limao lidondoshee chumvi na kisha paka kwenye hayo maeneo, kufanya hivi hupunguza utendaji kazi wa tezi jasho
NYANYA
Nyanya! huenda tunazitumia kila siku kwenye mboga, chakula, kwenye salad, Juisi na kadhalika lakini nyanya ni zaidi ya kiungo ni kituliza nafsi na inasaidia kurekebisha kutokwa jasho jingi ama hyperhidrosis kama wataalam wanavyoita.
Iko hivi,
1.Kata vipande viwili vya nyanya na paka sehemu husika subiri dakika 10 hadi 15 kisha safisha na maji ya uvugu vugu.
2.Ama unaweza kusaga juisi ya nyanya na kupaka sehemu husika subiri dakika 10 hadi 15 kisha safisha na maji ya uvugu vugu.
3.Ama unaweza kunywa kikombe cha juisi ya nyanya kila siku kisha ukiona tatizo linaanza kuondoka basi punguza na anza kunywa kila wiki, kisha nipigie na kusema asante.
MAJANI YA CHAI
Wengi hatufahamu lakini tumebarikiwa na majani ya chai Afrika ambayo pia ni ina ufanisi katika kuondoa hili tatizo la kutokwa na jasho hovyo,
Lowesha majani ya chai ama chukua majani ya chai yaliyotumika kisha pakaa kama hina kwenye viganja vya mikono na kuloweka miguu kwenye beseni lenye mchanganyiko wa maji ya vuguvugu na majani ya chai kibao walau kila siku kwa dakika 30, siyo tu ngozi ya miguu itakuwa laini pia tatizo la jasho miguuni litatoweka, usisahau kunywa chai ya sturungi asubuhi na jioni.
EPUKA
1.Vyakula vya pilipili
2.Mafuta ya mgando na mengineyo ya mwili yenye viambatanishi vya petroleum
Usisahau Kunywa maji mengi na yakutosha kila siku.
BAADHI YA USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU WA JF
---Hyperhidrosis ni ugonjwa wa kutokwa na jasho jingi kuliko kawaida. Kutokwa na jasho ni hali ya kawaida kwa binadamu na wanyama na kazi kubwa ya jasho ni kupoza mwili unapopata joto kubwa. Kwa kawaida mwili wa mwanadamu hutengeneza wastani wa lita moja ya jasho kila siku.
Kiwango cha jasho huweza kutofautiana kutokana na mazingira na hali ya mwili kwa mfano kipindi cha joto ama maeneo yenye joto kali, au kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia hufanya mwili kutoa jasho jingi zaidi ya kawaida ili kupooza mwili.
Ugonjwa wa hyperhidrosis hutokea pale mwili unapotengeneza jasho jingi zaidi ya linalohitajika kupoza mwili. Mfano ni kutoka jasho ukiwa umepumzika sehemu isiyo na joto au kutoka na jasho jingi unapoingiwa na hofu nk
Kitaalamu ugonjwa huu umegawanyika katika makundi mawili. Kuna primary hyperhidrosis na secondary hyperhydrosis. Primary hyperhydrosis huanza mara nyingi kipindi cha balehe na husababishwa na urithi wa vinasaba (genetics). Secondary hyperhidrosis huanza kipindi chochote cha maisha na husababishwa na magonjwa mengine ya mwili mfano kisukari, magonjwa ya tezi ya shingo na kadhalika.
Hyperhydrosis ni kilema kilichojificha
Mgonjwa wa hyperhidrosis hupata shida kuendana na shughuli za kawaida za maisha. Wengi hupatwa na aibu pindi jasho jingi linapolowanisha nguo au kushindwa kushikana mikono pindi viganja vinapolowa jasho jingi. Pia kuna baadhi ya shughuli humwia vigumu mfano jasho jingi mikononi husababisha ugumu wa kushika vifaa kipindi cha kazi. Ugonjwa huu huweza kusababisha msongo wa mawazo.
Tiba
Kuna tiba mbalimbali ya ugonjwa huu. Secondary hyperhidrosis hutubiwa kirahisi kwa kutibu ugonjwa unaosababisha secondary hyperhidrosis kama ilivyoelezwa hapo juu. Kwa hiyo ni muhimu kumuona daktari pindi unapopata na tatizo hili na kufanya vipimo ili kugundua magonjwa sababishi mfano kisukari na Magonjwa sababisha yakitibiwa na ugonjwa huu huisha mara moja.
Nitazungumzia zaidi primary hyperhidrosis ambayo husababishwa na vinasaba. Tiba yake nimeigawanya mara tatu. Kwanza ni kubadili mfumo wa maisha, pili ni dawa na tatu ni upasuaji.
Tukianza na kubadili mfumo wa maisha. Mgonjwa mwenye hili tatizo yampasa kubadili mfumo wake wa maisha ili kuendana na tatizo.
Kwanza inashauriwa kunywa maji mengi. Maji husaidia kupoza mwili na hivyo kupunguza kutokwa kwa jasho. Pia inashauriwa kupunguza vyakula vyenye viungo vingi, vinjwaji kama kahawa, pombe, sigara na vinywaji vichangamfu(energy drinks) maana vyakula na vinywaji hivi husababishwa mwili kutengeneza jasho.
Pia inashauriwa kuoga angalau mara mbili kwa siku kwa kutumia maji safi na sabuni yenye dawa mfano dettol.
Pia paka baking soda sehemu zinazotoa jasho jingi pindi tu umalizapo kuoga. Baking soda huharakisha kukauka kwa jasho kwa sababu ya alkalini iliyonayo.
Tumia vitoa harufu (antiperspirants/deodorants) vyenye aluminium chrolide ambayo huharakisha kukauka kwa jasho.
Tumia vikinga jasho (sweat pads) sehemu zinazotoa jasho jingi mfano sehemu za kwapa na kadhalika. Unaweza kununua vikinga jasho madukani au kutengeneza mwenyewe nyumbani kwa kutumia nguo na sponji na kuvaa ndani ya nguo.
Pia chai ya mmea uitwao salvia officinalis usaidia kupoza mwili na inashauriwa kunywa kwa watu wenye tatizo hili.
Kwenye upande wa dawa, dawa ziitwazo kitaalamu anticholinergic husaidia wenye tatizo la kutokwa na jasho hasa wanaopata tatizo hili wanapoingiwa na hofu ya kitu fulani.
Pia kwenye nchi zilizoendelea huduma ya upasuaji hutumika kwa wenye tatizo kubwa ambalo haliwezi kutibika kwa njia nyingine. Tiba hii inajumuisha kuingilia na kufunga kwa njia ya upasuaji mifumo ya fahamu inayosababisha kutoka kwa jasho.
Ukiachana na upasuaji, tiba ya kubadili mfumo wa maisha na dawa husaidia kwa kiwango kikubwa kwa mazingira yetu hapa Tanzania.
Dr Luhaja Nginila, MD
---Utokaji wa jasho mwilini una faida za kuboresha ngozi nakuondoa uchafu mwilini pamoja na kuratibu joto la mwili. Mnyama kama mbwaanategemea Zaidi ulimi wake manake hana sweatglands. Kama ambavyo mkojounapokuwa wa njano sana inaashiria upungufu wa maji na hata uti, miili yetuinatabia ya kutupa taarifa muhimu lakini tunaweza ku-respond ndivyo sivyo.
Kuzuia utokaji wa jasho mwilini kwa kemikalini kuhatarisha afya yako na ngozi yako. Mazoezi (especially jogging) huondoamafuta mwilini ndio njia bora ya kupunguza utokaji wa jasho mara nyingi ikiwemokupunguza unywaji wa bia na supu ikiwemo kula kupita kiasi.
Kujikinga ni pamoja na kuvaa vest kablahujavaa nguo kwa nje.kutumia kemikali ni sawa na kujichubua unajihatarisha nacancer za ngozi na complication zingine kama gharama n.k.tiba mbadala kuondoanana tatizo ni njia bora zaidi ya kufuata.tuache kuwaathiriwa na u-consumerism
Mimi ninao huo ugonjwa na huwa natokwa jasho hasa mikononi hadi naona karaha muda mwingine
Ni ugonjwa unaotuathiri psychologically zaidi; kujishtukia, kutotoa mikono wakati wa salamu n.k
Ngoja kwanza nifute jasho mikononi :A S cry:
Nimeshawahi kutumia hizo drysol (Aluminium chloride solution na Potassium permanganate) bila mafanikio yeyote
Botox ni temporary solution na ni gharama sana huku Iontophoresis inaelezwa kuwa njia bora zaidi ya kutibu na salama lakini sijui mahala wanapotoa huduma hii bongo
Cha muhimu kuwa msafi penda kuosha mikono yako mara kwa mara na kutumia hand sanitizer oftentimes na uwe na kitambaa cha walau kukausha mikono yako pindi jasho likizidi
Mwanamama wangu anapenda mikono yangu so far anadai ni laini (labda ananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa sijui!!); thou kweli watu tulio na tatizo hili huwa na mikono laini
Muhimu: usiwe mtumwa wa tatizo hili fanya mambo yako na jamii itakuzoea tu. Nimefarijika kujua tuko wengi waathirika wa huu ugonjwa