Ndugu wanaJF, nionavyo mimi tatizo la ardhi litatuletea mfarakano hapa nchini hapo baadaye. Ingawa viongozi wetu wanasema hakuna nchi iliyoendea bila wawekezaji lakini nchi zilizoendelea zina sheria nzuri kuhusu ardhi yao. Kama hizo nchi nazo zingegawa ardhi kama viongozi wetu wanvyofanya hapa Tz wasingefikia maendeleo waliyonayo leo hii. Vingozi wetu wanatafuta wawekezaji wa kuja kuwaondoa wananchi kwenye ardhi yao kwa kisingizio cha uwekezaji. Lakini watoto na wajukuu wetu watakapotaka kulima baadaye watapata wapi ardhi? Nahisi watakapokosa ardhi wataanza kuidai kwa nguvu na hapo ndipo matatizo yatakapoanza. Nchi ambazo zimewekeza kwenye kilimo zina utaratibu tofauti na tulio nao sisi. Mfano, katika hizo nchi wawekezaji wachache wamewekeza kwenye kilimo kwa kulisha nchi nzima na hata kusafirisha ziada nje. Lakini utaratibu unaotumika ni tofauti na huu unaotumika hapa kwetu maana huko husikii wananchi wanalalamikia kuondolewa kwenye ardhi yao kwa nguvu bila fidia nzuri au kupewa sehemu nyingine ya kuishi au kulima. Hapa kwetu Tz mwananchi anaondolewa au anazuiwa kuendeleza ardhi yake bila fidia na hivyo kutojua afanye nini. Mpaka aje afidiwe unakuta thamani ya ardhi imeshabadilika. Kweli hali hii ndiyo itakayotuletea maendeleo na ndio aina ya uwezekezaji unaotakiwa ili tuendelee?