Tathmini ya Viongozi wa Bunge 2011

Tanganyika2

Member
Oct 25, 2011
70
12
Siku ya Ijumaa tarehe 13 Julai 2012 kuanzia saa 4:00 asubuhi (10.00 Hrs EAT) Taasisi ya Raia ya Haki za Kisiasa na Mwenendo wa Bunge (The Civil and Political Rights Watch) itatoa taarifa juu ya tathmini ya Uongozi wa Bunge kwa mwaka 2011. Tathmini hii inaangalia utendaji na ufanisi wa viongozi wa Bunge, Spika, Naibu wa Spika na Wenyeviti wa Vikao vya Bunge. Tathmini hii imetumia dhana na zana za mfumo wa Uwajibikaji kwa Jamii (Social Accountability Monitoring) kama unavyotumiwa Afrika Kusini kupima vigezo vitano vya kuongoza vikao (Usikivu kwa wajumbe; Kuzingatia kanuni; kuzingatia hoja; Kukwepa Ushabiki; na Upendeleo kwa wajumbe).

Hii ni tathmini ya kwanza kabisa kufanyika Tanzania na kuwa itatumika kama nguzo ya kupima muelekeo wa utendaji na ufanisi wa viongozi wetu wa Bunge kwa miaka ijayo.

Waandishi habari wote mnakaribishwa (tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi).
Taarifa itatolewa kwenye ofisi za taasisi zilizopo Plot 522 Block E - Sinza Palestina (Off Shekilango Road) P.O Box 522 Dar es salaam:israel:
 
Siku ya Ijumaa tarehe 13 Julai 2012 kuanzia saa 4:00 asubuhi (10.00 Hrs EAT) Taasisi ya Raia ya Haki za Kisiasa na Mwenendo wa Bunge (The Civil and Political Rights Watch) itatoa taarifa juu ya tathmini ya Uongozi wa Bunge kwa mwaka 2011. Tathmini hii inaangalia utendaji na ufanisi wa viongozi wa Bunge, Spika, Naibu wa Spika na Wenyeviti wa Vikao vya Bunge. Tathmini hii imetumia dhana na zana za mfumo wa Uwajibikaji kwa Jamii (Social Accountability Monitoring) kama unavyotumiwa Afrika Kusini kupima vigezo vitano vya kuongoza vikao (Usikivu kwa wajumbe; Kuzingatia kanuni; kuzingatia hoja; Kukwepa Ushabiki; na Upendeleo kwa wajumbe).

Hii ni tathmini ya kwanza kabisa kufanyika Tanzania na kuwa itatumika kama nguzo ya kupima muelekeo wa utendaji na ufanisi wa viongozi wetu wa Bunge kwa miaka ijayo.

Waandishi habari wote mnakaribishwa (tafadhali wasiliana nasi).

Back
Top Bottom