Tariffs za TANESCO zipoje?

Asante sana brother karibu

KAKA MI MITA YANGU IPO KWENYE TARRIF 4,,ILA MUDA MWINGINE MATUMIZI YANAZIDI UNIT 75_ KWA MWEZI,, JE! TANESCO HAWAWEZI KWELI KUNIONDOA KTK IYO TARRIF 4, YAANI NAHOFIA ILO LABDA,, AU UTARATIBU UPOJE,,maana inatokeaga Mara moja moja Sana matumizi kudhidi, aswa kipindi hiki cha likizo wageni wengi home,,
 
Kama matumizi yako kwa mwezi yanazidi unit 75 unatakiwa kuwa tariff 1, unit ambazo zinazodi unalipia Tsh 350 kwa unit.

Andika barua ufike ofisi ya TANESCO uliyokaribu nayo ukiomba kubadilishiwa Tariff.

Unaweza kujieidhisha kwa kuangalia kwenye risiti yako ya kununulia umeme inaonesha tariff uliyopo.

Pia unapounganishiwa umeme automatic unakuwa Tariff 1, Tariff 4 unaenda baada ya kuwa umeomba ndio unapelekwa.

Nafikiri ulishawahi kuomba kubadilishiwa Tariff? Kama bado angalia upo Tariff gani kwanza.
 
boss mimi nimefurahishwa na namna anavyotoa ufafanuzi hapa.
hili shirika ni la uma lakini limejaa ukiritimba sana.
mimi mama yangu nikimnunulia umeme anaweza kukaa miezi 6 unit hazijaisha.
niliomba kubadilishiwa tariff lakini mpaka leo wananizungu.
ninafanya kazi ya kulipa service charge tu.
you can immagine service charge ya miezi 6au 8 inavyokuwa hata unit ntakazopewa ni chache mno
mama yangu anawaza kaa miezi 3ukiangalia salio unaona zimepungua unit 5 labda.
sijui ntasaidikaje?
nahitaji msaada wako.
 
Naomba uni PM namba yako ili tufuatile kaka
 
Mkuu Koleba nakushukuru kwa ufafanuzi na hasa huu wa Error 77 umekubali kuzima na kuwaka vizuri
ila nimeshtuka hii ya kujinyima kutumia T1 nikitaka nihamishiwe T4
  • kumbe nikiirudisha friji heater na pasi ni lazima nitavuka unit 75 nazo nitatozwa zaidi kwa Tsh 52 yaani kutoka 298/ hadi 350/
  • bado Tanesco wanaumiza naona km umeme umepanda kwani matumizi yangu halali kwenye mita ya kizamani yalukuwa hayazidi 40,000/= unit km 120 kwa mwezi
swali lingine la kifizikia nikizimam Friji kutwa nzima ninapokuja kuiwasha naona inachukua muda mrefu kupata ubarudu na kugandisha nishauri nifanyeje ili isile umeme na ina thermostart 9umeme wa tz umeshakuwa shida )

Mkuu inategemea na aina ya friji labda ila kama ni haya ya kisasa wala hayatumii umeme mwingi.
Mama angu anatumia tariff 4 ananunua unit 75 kwa 9,150tshs ana friji kubwa, kettle hii inatumika kila siku, rice cooker japo hutumika mara chache, ana pasi TV na radio na yuko tariff 4 anasema katika kumbukumbu zake aliwahi kuvuka hizo unit 75 mara mbili au tatu. Hivyo kama huna familia kubwa hizo unit 75 zinakutosha lakini kama mko wengi sana bakia tu tarif 1.
 
nafanyaje ili kuhamia T4?

Andika barua kwa meneja ukiomba kubadilishiwa tariff. Ikiwezekana attach risit zako mbili tatu za hivi karibuni kuwekea uzito swala lako. Na wakiona unastahili watakuhamisha tu bila tatizo. Zoezi hilo wala halichukui muda mrefu na ukishabadilishiwa bili yako ya kwanza utaenda kuilipia Tanesco kisha utaendelea na utaratibu wako kama kawaida
Kila la heri mkuu
 
Ikiwa remote au CIU kitaalam inonyesha Err 77 ujue ni kuwa hakuna mawasiliano kati ya hiyo remote CIU na mita MCU hivyo kuna sababu kadhaa za kujua hilo tatizo linasababishwa na nini.
1) Hakuna complete path kati ya hivyo vitu viwili either kutokana na loose connection au umechomeka remote kwenye socket na haujawasha switch yake
2) Huenda hiyo remote sio ya mita uliyofungiwa hivyo haitaweza kuwasiliana milele hivyo unatakiwa kuioanisha kwa kubonyeza namba 0 ikifuatiwa na namba ya mita mara mbili alafu unabonyeza mshale wa Enter au Ok na tatizo linakuwa limeisha na kutumia remote yako kama kawaida
 
Mkuu Nando ni pm namba yako tuongee zaidi utaweza kusaidiwa.
Mkuu ile Error 77 imekwisha baada yakufuata maelekezo na kumbe init pia zilikwisha
asante sana kwa ufafanuzi
lakini bado naomba ushauri wa kuingia T4 kwenye unit 1- 75 @ 100/= (7.500) nikizidisha matimizi ya unit hata 20 bado 7,000/= na 22% nitaokoa vingi kuliko unit 95 kwa T1 X 298/= + 22% ni zaidi ya 28,310/=
bado nipo njia panda niingie T4?
 
Ila unit 75 kwa sasa ni 9,150 kumbuka kuna makato mengine madogo, zamani kabla Tanesco hawajapandisha bei umeme ilikuwa ni 3,500.
 
Ila unit 75 kwa sasa ni 9,150 kumbuka kuna makato mengine madogo, zamani kabla Tanesco hawajapandisha bei umeme ilikuwa ni 3,500.
Nashukuru kwa ushauri wako Mkuu
kuanzia leo nimeliwasha Friji langu nione km kwa siku litamaliza unit 2 pamoja na taa zikiwa unit 60 nitaimba kwenda T4
 
Koleba salute kwako. Umejibu maswali kitaalamu sana. Tanesco ingekua na watu 50 kama wewe tungekua mbali.
 
asante sana mkuu,hii inasaidia maana nimepiga hesabu nimeona kwa siku natumia wastani wa ujnit 3.9,nina friji,taa ,feni na TV,pasi natumia mara chache,vipi kwa utaalamu wako matumizi hayo yanweza kuwa shihi?
Andika barua kwa meneja ukiomba kubadilishiwa tariff. Ikiwezekana attach risit zako mbili tatu za hivi karibuni kuwekea uzito swala lako. Na wakiona unastahili watakuhamisha tu bila tatizo. Zoezi hilo wala halichukui muda mrefu na ukishabadilishiwa bili yako ya kwanza utaenda kuilipia Tanesco kisha utaendelea na utaratibu wako kama kawaida
Kila la heri mkuu
 
Wakuu msijichanganye tariff 1 inakuwa hivi.
1kwh = Tzs 298 (umeme bila vat)
Service charge = Tzs 5520 (bila vat)

Service charge inakatwa mara moja kwa mwezi

Mfano

Una shilingi 10,000

TANESCO SVC = 5520 + Vat (22% ya 5520)
Kwa hiyo jumla itakuwa = 6734.4

Kununua umeme unachukua 10,000 - 6734.4 = 3265.6 tuki approximate unapata Tzs 3266

Kila manunuzi yanakuwa na vat

3266 * 22% unapata 718.4

Kwa maana hiyo unachukua 3266 - 718.4 = 2547.568 tuki approxmate tunapata Tzs 2548.

Energy ( UMEME) 2548/ 298( 298 ni bei ya umeme kwa unit)
= unapata unit 8.5 uki approximate 9 Kwh
 
asante sana mkuu,hii inasaidia maana nimepiga hesabu nimeona kwa siku natumia wastani wa ujnit 3.9,nina friji,taa ,feni na TV,pasi natumia mara chache,vipi kwa utaalamu wako matumizi hayo yanweza kuwa shihi?

Kama unatumia unit 3 inamaana kwa mwezi ni unit 90 hivyo ukihamia tariff 4 itakula kwako. Ulipo ndio sahihi
 
Mkuu hapa nyumbani tukiweka umeme Wa laki moja unakaa siku mbili tu na hakuna kabisa vifaa vya kula umeme sana
 
Mkuu hapa nyumbani tukiweka umeme Wa laki moja unakaa siku mbili tu na hakuna kabisa vifaa vya kula umeme sana

Unatumia vitu gani mkuu, unamita za LUKU ama zile za kawaida?

Vitu vingi vinachangia kama uchakavu wa wiring, aina za bulb, cookers, birika, pasi, heaters etc.

Sheria ya tanesco inawataka wananchi kufanya ukaguzi wa wiring after 5 yrs wabongo hilo hawafanyi kwa nyumba zo, panya darisin wametfuna way, leakage inaweza kusababisha umeme kupotea.

earthrod ambayo sio pure Cooper ambayo inasababisha umeme kupotea.
 
Wakuu msijichanganye tariff 1 inakuwa hivi.
1kwh = Tzs 298 (umeme bila vat)
Service charge = Tzs 5520 (bila vat)

Service charge inakatwa mara moja kwa mwezi

Mfano

Una shilingi 10,000

TANESCO SVC = 5520 + Vat (22% ya 5520)
Kwa hiyo jumla itakuwa = 6734.4

Kununua umeme unachukua 10,000 - 6734.4 = 3265.6 tuki approximate unapata Tzs 3266

Kila manunuzi yanakuwa na vat

3266 * 22% unapata 718.4

Kwa maana hiyo unachukua 3266 - 718.4 = 2547.568 tuki approxmate tunapata Tzs 2548.

Energy ( UMEME) 2548/ 298( 298 ni bei ya umeme kwa unit)
= unapata unit 8.5 uki approximate 9 Kwh

Mkuu nilikua natumia meter ya kawaida,wakanibadilishia wakaweka ya luku.Units zimeisha wamesema nipeleke 32,000/= je,ni sawa mkuu?
 
Mkuu nilikua natumia meter ya kawaida,wakanibadilishia wakaweka ya luku.Units zimeisha wamesema nipeleke 32,000/= je,ni sawa mkuu?

Mita ikiwa mpya pale wanapokufungia wanakukopesha units kadhaa ili uanzie. Sasa unapoenda kununua mara ya kwanza unalipa deni na kuendelea kununua umeme kama kawaida. Nahisi hiyo hela ni kwa ajili ya kulipia zile unit za mwanzo na wewe kupata umeme, baada ya hapo utanunua tu utakavyo
 
Back
Top Bottom