Taratibu za kuacha kazi

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,926
Wakuu nina tatizo moja kuhusu sheria za kazi hususani hapa kwetu Tz.

Sijui kwingine zikoje lakini nafahamu kuwa wengine hufanya kazi kwa mikataba ambapo ukiisha kila upande una hiari ya kuundeleza. Sasa kama mimi nimeajiriwa kwa terms za PERMANENT AND PENSIONABLE ni awakati gani naweza kuachana na huo mnyororo nikalipwa haki zangu zote kama vilenimestaafu nikapomptezea mwajiri anayeniboa hususani JK?

Nataka nipambane na kiliomo na mifugo tu. Habari ya sh. 210, 000 ni ushenzi mtupu.

Mwenye kuelewa sheria tafadhali, na kama kama haipo tumwombe Mtikila atusaidie maana ni haki yangu kumsepa mwajiri mbovu na kuchagua kilicho bora bila kupoteza haki yangu ya msingi ya mafao.
 
Naungana na wewe muanzisha mada. Nataka kuacha kazi, lakini nina mkopo benki ninaoulipa kupitia mshahara na mwajiri wangu nio mdhamini. Nikipiga mahesabu NSSF yangu haitoshi kulipa deni hilo. Nikiacha kazi, nini hatima ya mkopo itakuwaje?
 
Naungana na wewe mtoa mada
Huyo mwajiri wako unatakiwa umpe notice ya mwezi mmoja na umfanyie kazi bure mtaachana kwa amani tele
Ama ukubali kumlipa mshahara wako mmoja ..unapotoa short notice
 
Ipitie hiyo attachment mkuu
 

Attachments

  • Employment and Labour Relations Act-2004.pdf
    469.6 KB · Views: 186
Naungana na wewe mtoa mada
Huyo mwajiri wako unatakiwa umpe notice ya mwezi mmoja na umfanyie kazi bure mtaachana kwa amani tele
Ama ukubali kumlipa mshahara wako mmoja ..unapotoa short notice

je ukila kona bila taarifa zozote kuna ishu gani itakuharibikia kwa upande wa mwajiriwa?
na kama je unadaiwa na mwajiri mkopo itakuwaje?
 
Naungana na wewe muanzisha mada. Nataka kuacha kazi, lakini nina mkopo benki ninaoulipa kupitia mshahara na mwajiri wangu nio mdhamini. Nikipiga mahesabu NSSF yangu haitoshi kulipa deni hilo. Nikiacha kazi, nini hatima ya mkopo itakuwaje?

kuna aina mbili za kuacha kazi one month notice ambapo utapata mshahara wako wa mwezi kama kawaida na stahiki zingine hasa michango yako ya hifadhi ya jamii.pili kuna 24hrs notice ambapo unamlipa mwajiri wako mshahara mmoja.then unapata michango yako kama kawaida, kuhus pension nadhani ukiacha kazi huwezi pata pension au mafao yako zaidi ya michango yako na ya mwajiri kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Na kama unamkopo benki na mwajiri alikuzamini, najua kwamba mabenki mengi ya bima ya mikopo hivyo ndiyo maana huwa wakata pesa fulani kwenye mkopo wako kwa ajili ya bima hiyo.na ndiyo maana siku hizi sheria inaelekeza cheki ya malipo yako ya mafao ya hifadhi ya jamii inaandikwa jina lako na si jina la muajiri kama zamani. cha msingi ukiacha kazi unawajulisha benki husika mtaanagali njia mbadala kwa pamoja jinsi ya kulipa deni lako.
 
Thanks kwa michango. Naona nitapata michango yangu ya pension kama ilivyoelezwa. Nataka nimpotezee yaishe. Siwezi kusubiri hadi nistaafu maana duh aibu. Nasepa.
 
Thanks kwa michango. Naona nitapata michango yangu ya pension kama ilivyoelezwa. Nataka nimpotezee yaishe. Siwezi kusubiri hadi nistaafu maana duh aibu. Nasepa.

if your employer is giving you a row deal, you better learn how to cut your own!
karibu katika chama.
 
kwenye kila mkataba halali wa kazi lazima utoe njia au namna kuacha kazi mara ambapo utakapo jisikia kua hauwezi kuendelea na kazi au mwajiri hakuitaji tena, mara nyingi hua ni notice ya siku 30 kumtaarifu mwajiri kua hutaendelea kua nae tena kwa siku za usoni, au mshahara wa mwezi mmoja inapotokea unataka kuacha kazi ndani ya saa 24 ua muda pungufu wa siku 30, (unamlipa mwajiri).

ila unapotaka kukatisha maktaba wa ajira kwa njia ya ndugu (mtoa mada) anavyo taka kufanya kunavitu kisheria unapoteza kama muajiriwa kuna kitu kinaitwa severence pay ipo kwenye S. 42 ya ELRA kama sikosei, ila terminal benefit zako utapata, hiyo ni pamoja na michango yako social secuity, gharama za kukusafirisha toka sehemu ulipotoka ulivyo anza kazi wewe pamoja na familia na mizigo na pia certificate ya employment yako toka kwa muajiri wako.
 
Nice ushauri kwa mtoa mada hasa yule aliyempa link ya labour relations
 
Back
Top Bottom