TANZIA: Mwandishi mkongwe, Mayage S. Mayage afariki dunia

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Wakuu,

Nasikitika kuwafahamisha kuwa mwenzetu Mayage Stephen Mayage ambaye ameandikia magazeti kadhaa pamoja na mtandao dada wa JF, FikraPevu.com (pia alikuwa mwanachama wa JF) amefariki leo Desemba 25, 2017.

9ca57d18a7a54a18fba9e3a16223f1eb.jpg

Marehemu Mayage wakati wa uhai wake...

Kwa mujibu mke wa Marehemu, Digna Mayage, mwenzetu amefariki majira ya saa 3 asubuhi ya leo akiwa hospitali ya Misheni huko Mbweni alikokuwa amelazwa.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Mbweni. Tutapeana taarifa zaidi kadri tutakapozipata.

Bwana alimtoa na sasa ameamua kumtwaa!

RIP Mayage

========
UPDATE:

Mayage S.Mayage kuzikwa Mbweni jijini Dar siku ya Alhamisi (28/12/2017)

MWANDISHI wa habari mwandamizi, Mayage Stephen Mayage, (56), amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda.

Mayage amekutwa na umauti katika Hospitali ya Misheni ya Mbweni, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa muda wa wiki mbili.

Taarifa kutoka kwa mdogo wake Emmanuel Mayage, alisema kuwa madaktari waligundua kaka yake kuugua saratani na kifua kikuu (TB).

Emmanuel alisema kuwa Mayage atazikwa keshokutwa (Desemba 28, 2017) katika makaburi ya Mbweni, eneo linaloitwa Maputo.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu Mbweni Kijijini, eneo la Maputo ambako ndugu na jamaa wanakutana.

“Mayage aligundulika kuwa na saratani mwaka mmoja uliopita na alianza matibabu katika hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Ocean Road na Muhimbili.

Alisema hali yake iliimarika kwa muda, lakini ikabadilika wiki tatu zilizopita na kusababisha kulazwa katika hospitali ya Mbweni.

Emmanuel alisema kuwa akiwa hospitalini hapo, kaka yake aligundulika pia kuwa na maradhi ya kifua kikuu na alianzishiwa tiba.

Mayage alianza kazi za uandishi wa habari mwaka 1995, akifanya kazi katika kampuni ya magazeti ya Habari Corporation; inayochapisha magazeti ya Mtanzania, RAI, Dimba, The African na Bingwa.

Baadaye Mayage aliondoka katika magazeti hayo na kuanza kazi ya uandishi wa habari wa kujitegemea, yeye akijiita “mwandishi huru.”

Akiwa mwandishi huru, Mayage alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali nchini, yakiwemo ya Raia Tanzania, MwanaHalisi na mtandao wa FikraPevu. Mpaka kufariki kwake, alikuwa mwajiriwa wa gazeti la TAZAMA.

Salva Rweyemamu, aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya Habari Corporation amemzungumzia Mayage na kueleza kuwa alikuwa mwandishi mzuri, mahiri, asiyeogopa na aliyefanya kazi yake kwa weledi, huku akiwa mchambuzi mzuri wa habari za siasa za nchi hii.

“Mayage hakushindwa kazi yoyote aliyotumwa, ukimwagiza lazima uwe na uhakika wa kuifanikisha, hakika tumepoteza mchapakazi,” alisema Salva kwa masikitiko.
 
Poleni ndugu, jamaa na marafiki..Mungu amlaze marehemu mahala pema peponi...hakika kila nafsi itaonja mauti.
 
Kuna yule jamaa alikuwa anaandika(Mhariri? Mmiliki?) kwenye gazeti la Tazama. Ndio huyu au ni mtu mwingine?
 
Back
Top Bottom