Tanzia: Moto waua watu sita Kitunda, Apona mmoja tu aliyekuwa matembezini usiku!

DAKA MTUMBA

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,288
801
Ni familia ya watu saba, kapona mmoja aliyekuwa matembezini usiku.Alipofika nyumbani usiku saa 6 akakuta nyumba inawaka moto,milango yote ilikuwa imefungwa na haikuwa rahisi kuivunja.

Chanzo cha moto huo inasemekana ni shoti ya umeme.

Ndugu wote sita wamefia ndani na muda huu ndio maiti zainapelekwa hospitali.

Chanzo: Mdau aliyepo eneo la tukio!!!

Sina taarifa kwa kina ila ni watu ninaowajua sana. Wamefariki Mume, Mke na wajukuu. It's so Sad.


IMG-20150207-WA0066.jpg

Watu sita wamekufa kwa moto baada ya nyumba inayomilikiwa na mzee David Mpili, kuteketea kwa moto huko Kipunguni Ukonga jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi Februari 7, 2015. Taarifa zinasema, familia hiyo ambayo ina uhusiano na waziri wa nchi ofisi ya rais kazi maalum, Profesa Mark Mwandosya iliokana na hitilafu ya umeme. Profesa Mwandosya mwenyewe ni miongoni mwa watu waliofika kwenye eneo la tukio mapema leo hii Jumamosi, ili kuwapa pole na kujionea uharibifu na maafa yaliyosababishwa na moto huo, pichani majirani ndugu jamaa na marafiki, wakiangua kilio kwenye eneo la ajali mapema leo.
IMG-20150207-WA0069.jpg

Profesa Mark Mwandosya, (Mwenye suti), akiangalia uharibifu uliofanywa na moto huo, alipofika eneo la ajali mapema leo Jumamosi februari 7, 2015
IMG-20150207-WA0071.jpg

Hii ndiyo hali halisi, mabaki ya nyumba hiyo yakionekana leo jumamosi Februari 7, 2015
IMG-20150207-WA0065.jpg

Majirani wakiondoa mabaki ya nyumba hiyo.
 
Wanasema ni maeneo ya MAJI MACHAFU kabla ya kuvuka reli ya kwenda KITUNDA.

View attachment 225172

Akizungumza na gazeti hili eneo la tukio Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kipunguni A, Praxeda Mkandara alisema kuwa alipata taarifa saa 12:00 asubuhi kuwa kuna nyumba imeungua moto na kuteketeza kila kitu na kusababisha vifo vya watu sita

Dar es Salaam. "Yesu tuokoe, Yesu tuokoe". Ndiyo sauti ya mwisho iliyosikia toka kwenye nyumba ya vyumba vitatu na sebule iliyoteketea kwa moto na kusababisha watu sita wa familia moja kupoteza maisha, huku miili ya baba na mama wa familia hiyo ikikutwa pamoja imekumbatiana, ikiwa ni ishara ya kufa pamoja.

Kila aliyekuwepo kwenye eneo la tukio alikuwa ni mwenye simanzi, hasa waumini wenzake wa Kikristo kwakuwa jana (Jumamosi) ilikuwa ni zamu ya familia hiyo kuwa wenyeji wa sala ya pamoja ya wanajumuiya nyumbani hapo. Moto huo unaosadikiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme, ulitokea saa nane usiku katika eneo la Kipunguni A, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Godfrey Mwandosya ni kaka wa marehemu Selina Mpira ambaye ni mke wa David Mpira baba wa familia hiyo, aliwataja watu waliofariki dunia kwenye ajali hiyo ya moto kuwa ni dada yake Selina Mpira, mumewe David Mpira (waliokutwa wamekufa pamoja wakiwa wamekumbatiana), mtoto wao wa kwanza Lucas Mpira, mdogo wake aliyekuwa akiishi na dada yake Samwel Mayegela na wajukuu Selina na Paulina ambao ni watoto wa Emmanuel aliyenusurika baada ya kuwa nje ya nyumba hiyo.

"Tumepanga mazishi yatafanyika Jumanne saa 8:00 mchana katika makaburi ya Airwing Ukonga baada ya kuwasili ndugu wa marehemu waliopo mbali ambao tunatarajia watawasili siku ya Jumatatu," alisema Mwandosya.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya waliyokuwa wanasali ambayo marehemu Mpira alikuwa ni Mwenyekiti, Deus Mathias alisema kuwa alifika mahali hapo kwa ajili ya kusali Jumuiya , lakini akiwa njiani akaona moshi na watu wamejaa eneo hilo baada ya kusogea ndiyo akafahamishwa kuwa familia hiyo imeteketea kwa moto.

"Nilifahamishwa kuwa jana usiku walitizama mpira na kulala usiku mkubwa ndiyo maana tukio hilo lilipotokea hawakustuka mapema, lakini waliofika mapema wanasema kuwa walimsikia mwanamke akisema ‘Yesu tuokoe, Yesu tuokoe' huku mwanaume akiunguruma, lakini ilikuwa ngumu kuwaokoa kwa sababu milango ilikuwa migumu kufunguka na moshi ulikuwa umetanda sana, "alisema Mathias.

Kwa upande wa jirani wa familia hiyo Mohamed Mwagila alisema kuwa alipata taarifa saa 11:17 asubuhi na alipofika eneo la tukio alikuta tayari watu wamekusanyika na wakajaribu kuvunja dirisha la nyumba hiyo la nyuma ili wawaokoe lakini hawakuona mtu.

Alisema walijaribu kumwaga maji lakini hawakufanikiwa kwa sababu hayakuwapo ya kutosha, hadi Polisi walipofika saa 11:00 jioni na Tanesco walipoachanisha nyaya zinazoleta umeme katika nyumba hiyo, "Polisi wakazikuta maiti tatu ya mjomba na watoto wa dada yake chumba kimoja, ya kijana wao mkubwa chumbani kwake huku ya baba na mama zikiwa pamoja zimekumbatiana, "alisema Mwagila.

Akizungumza na gazeti hili eneo la tukio Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kipunguni A, Praxeda Mkandara alisema kuwa alipata taarifa saa 12:00 asubuhi kuwa kuna nyumba imeungua moto na kuteketeza kila kitu na kusababisha vifo vya watu sita.

Mkandara alisema katika nyumba hiyo wanaishi watu saba, lakini mmoja aliyemtaja kwa jina la Emmanuel Kirigiti inasemekana alikuwa Java kwenye muziki, wakati tukio hilo linatokea hakuwapo ndani na ndiyo manusura yake.

Akizungumza katikia eneo la tukio Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Jerry Silaa alisema kwa sababu waliokufa ni wanafamilia hivyo wao kama Serikali watalibeba jukumu hilo hadi siku ya Jumanne yatakapofanyika mazishi.

Alisema alikuta Polisi na Zimamoto wamefika na kutoa miili ya marehemu, walipotaka kuondoka jirani mmoja akasema ndani ya nyumba hiyo wanaishi watu sita mbona miili imetoka mitano, hivyo Polisi wakalazimika kurudi ndani na kupekua na kupata mwili mwingine.

Silaa alisema baba mwenye nyumba ambaye naye amefariki dunia katika tukio hilo alikuwa mwanajeshi mstaafu ambapo Jeshi limetoa hema moja, hivyo wao kama Serikali wataleta mahema na chakula kwa kipindi chote cha kuomboleza msiba huo.

Mbali na Meya Silaa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki alikuwapo eneo la tukio ingawa hakuwa tayari kuzungumza chochote mbali ya kuonekana akisikitika muda wote.

"Tunaubeba huu msiba kwa sababu baba wa familia ambaye angebeba jukumu hili kama angekuwa hai na yeye kwa bahati mbaya amefariki dunia, hii ni hali ambayo inaweza kumpata yeyote ajali ya moto ni mbaya sana, tutakuwa pamoja nao kwa chakula, mahema hadi watakapomaliza maombolezo, "alisema Silaa.

Akileleza hali ilivyokuwa baada ya kufika eneo la tukio alisema alikuta Polisi na Zimamoto wamefika na kutoa miili ya marehemu, walipotaka kuondoka jirani mmoja akasema ndani ya nyumba hiyo wanaishi watu sita mbona miili imetoka mitano, hivyo Polisi wakalazimika kurudi ndani na kupekua na kubahatika kupata mwili mwingine.
Chanzo: Mwananchi
 
Sina taarifa kwa kina ila ni watu ninaowajua sana. Wamefariki Mume, Mke na wajukuu. It's so Sad.
 
Familia rafiki tangu tu vijana imetuumiza sana na imetuachia majonzi mazito. Tunamwomba mwenyezi mungu awaweke mahali pema peponi amin.
 
So sad...Mungu awafariji wafiwa...alafu hii system ya kuzba madrsha kwa gril na alminium juu bila kuacha uwazi ni rsk sana cz moto uktokea milango hujizba
Umeona eeh kweli kabisa,sasa naelewa kwa nini nyumba ulaya madirisha yahana grill,yaani ni hatari sana kwa kweli
 
R.I.P familia, jamaa aliyebaki amshukuru sana Mungu, lakini akiwa amaetoka kwenye madhambi usiku huo atubu na amgeukie Mungu.
 
Back
Top Bottom