Tanzanite One yakwepa kodi kwa miaka mitano

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

[h=2][/h]JUMAPILI, JULAI 15, 2012 07:54 NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

WAKATI Kampuni ya Tanzanite One ya Afrika Kusini ikituhumiwa kukwepa kulipa kodi kiasi cha Dola milioni mbili za Marekani, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo, Balozi Ami Mpungwe, ameibuka na kudai makosa ya kiufundi kati ya kampuni yao na Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) ndiyo yaliyosababisha fedha hizo zisilipwe kwa wakati.

Kodi inayodaiwa kukwepwa kulipwa na Kampuni ya Tanzanite One inayochimba madini ya Tanzanite katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ni ya kuanzia mwaka 2004 na 2008.

Hata hivyo, alisema tayari Kampuni yao imekwisha anza utaratibu wa kulilipa taratibu deni hilo.

Kuibuka kwa madai hayo kulijitokeza juzi, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Masele, alipotembelea maeneo ya migodi katika eneo la Mererani, wilayani Simanjiro juzi.

Pamoja na mambo mengine, alielezwa malalamiko ya wachimbaji wadogo jinsi wanavyonyanyaswa na Kampuni hiyo kwa kumwagiwa maji chini ya ardhi pindi wanapochimba madini.

Katika majibu yake kwa Naibu Waziri Masele, Balozi Mpungwe, aliweka wazi kuwa hakuna jambo kama hilo, bali kinachofanyika kwa wakati huo wa kuchimba madini huwa ni kukutana na maji chini ya ardhi.

“Unapochimba chini ya mwamba lazima ukutane na maji na lazima uyatoe kwa kutumia mabomba yaliyofungwa chini ya ardhi ambayo hutoa maji migodini na kumwaga nje,” alisema Balozi Mpungwe na kuongeza:

“Tatizo linalosababisha wachimbaji wadogo kulalamika kuwa wanamwagiwa maji linasababishwa na uchimbaji usiozingatia sheria na taratibu. Hivyo tunaiomba Serikali kutukutanisha na wachimbaji hawa ili tumalize tofauti na kuangalia upya taratibu za kuvuta maji nje,” alisema.

Kwa upande wake, Masele, akizungumza baada ya kusikiliza apande zote mbili, kuhusu suala la kuongezewa mkataba au la alidai kwamba kwa sasa Serikali inaendelea kushughulikia suala hilo.

Akifafanua kuhusu tatizo la kuwapo kwa maji, Masele, aliitaka Kampuni hiyo kuhakikisha inaondoa maji hayo chini ya migodi mara moja.

“Ni vyema mkiandaa utaratibu wa kuwa na vikao baina ya vijiji vinavyozunguka mgodi huu kwa kuwa kutarahisisha kuainisha mambo mnayotaka na kuafikiana kwa pamoja ili kuondoa kero kwa wananchi.

Naye, mchimbaji mdogo, Hawa Karanga, akizungumza kwa niaba ya wenzake, alisema sheria ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite inamtaka mchimbaji kuchimba madini hayo kwa kwenda chini ya eneo lake na si kuingiliana mipaka chini ya ardhi.

Amy Mpungwe... Blessings

Kila Kiongozi wa Kitanzania anaiibia nchi yake; hakuna upenzi wa nchi hakuna anayejali...

Na nchini ni visa na masihara kati ya wananchi ili kujenga chuki na kusahau wezi...
 
Wamieba Tanzanite, wametesa WaTz wenzetu na kodi yetu wanatutapeli, waondoke hao.
 
JUMAPILI, JULAI 15, 2012 07:54 NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

WAKATI Kampuni ya Tanzanite One ya Afrika Kusini ikituhumiwa kukwepa kulipa kodi kiasi cha Dola milioni mbili za Marekani, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo, Balozi Ami Mpungwe, ameibuka na kudai makosa ya kiufundi kati ya kampuni yao na Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) ndiyo yaliyosababisha fedha hizo zisilipwe kwa wakati.

Kodi inayodaiwa kukwepwa kulipwa na Kampuni ya Tanzanite One inayochimba madini ya Tanzanite katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ni ya kuanzia mwaka 2004 na 2008.

Hata hivyo, alisema tayari Kampuni yao imekwisha anza utaratibu wa kulilipa taratibu deni hilo.

Kuibuka kwa madai hayo kulijitokeza juzi, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Masele, alipotembelea maeneo ya migodi katika eneo la Mererani, wilayani Simanjiro juzi.

Pamoja na mambo mengine, alielezwa malalamiko ya wachimbaji wadogo jinsi wanavyonyanyaswa na Kampuni hiyo kwa kumwagiwa maji chini ya ardhi pindi wanapochimba madini.

Katika majibu yake kwa Naibu Waziri Masele, Balozi Mpungwe, aliweka wazi kuwa hakuna jambo kama hilo, bali kinachofanyika kwa wakati huo wa kuchimba madini huwa ni kukutana na maji chini ya ardhi.

"Unapochimba chini ya mwamba lazima ukutane na maji na lazima uyatoe kwa kutumia mabomba yaliyofungwa chini ya ardhi ambayo hutoa maji migodini na kumwaga nje," alisema Balozi Mpungwe na kuongeza:

"Tatizo linalosababisha wachimbaji wadogo kulalamika kuwa wanamwagiwa maji linasababishwa na uchimbaji usiozingatia sheria na taratibu. Hivyo tunaiomba Serikali kutukutanisha na wachimbaji hawa ili tumalize tofauti na kuangalia upya taratibu za kuvuta maji nje," alisema.

Kwa upande wake, Masele, akizungumza baada ya kusikiliza apande zote mbili, kuhusu suala la kuongezewa mkataba au la alidai kwamba kwa sasa Serikali inaendelea kushughulikia suala hilo.

Akifafanua kuhusu tatizo la kuwapo kwa maji, Masele, aliitaka Kampuni hiyo kuhakikisha inaondoa maji hayo chini ya migodi mara moja.

"Ni vyema mkiandaa utaratibu wa kuwa na vikao baina ya vijiji vinavyozunguka mgodi huu kwa kuwa kutarahisisha kuainisha mambo mnayotaka na kuafikiana kwa pamoja ili kuondoa kero kwa wananchi.

Naye, mchimbaji mdogo, Hawa Karanga, akizungumza kwa niaba ya wenzake, alisema sheria ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite inamtaka mchimbaji kuchimba madini hayo kwa kwenda chini ya eneo lake na si kuingiliana mipaka chini ya ardhi.

Hawa TanzaniteOne wasichezee watanzania, TMAA wamebaini wizi wao waziwazi na wamewabana kisawasawa halafu wanasema eti kasoro za kiufundi. Ama kweli, mwizi hakubali kirahisi. Hawa ni wezi wakubwa, wanainyonya nchi hii kwa kivuli cha watanzania wenzetu akina Mpungwe. Naomba Mungu usiku na mchana Serikali isiwape leseni tena ili rasilimali ya nchi isiendelee kuporwa na hao wezi. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
 
Balozi wa Bongo South Africa then Amy Mpungwe ndio aliyeileta... wengine wanasema PRINCE ana share;

Nachanganyikiwa; sasa hawalipi kodi, madini ni yetu...
 
Back
Top Bottom