Tanzanite iliyonunuliwa na Serikali yavunja rekodi kwa ukubwa duniani | Inaweza kutumika kukuza Sekta ya Utalii

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
Na Malisa GJ

Tanzanite.jpg

Saniniu Laizer mchimbaji mdogo wa madini huko Mererani ameamka Bilionea baada ya kupata mawe mawili ya Tanzanite moja lenye uzito wa 9.2KGs na jingine 5.8KGs yenye thamani ya TZS 7.8 Bilioni.

Watu wengi wanajadili kuhusu Tanzania kumpata Bilionea mpya. Ni jambo zuri lakini kuna jambo jingine ambalo halijadiliwi. Na pengine ni la msingi zaidi kuliko Ubilionea wa Laizer.

Hii Tanzanite ya 9.3KGs inaweza kuwa ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana duniani. Hii ndio "angle"ya habari, ambayo inaweza ikabreak (as breaking news) ikatoa day 2 story na ikatengenezewa developing story hata kwa mwezi mzima.

Kabla ya Laizer kuushangaza ulimwengu kwa kuchimbua ardhi na kupata madini haya makubwa kabisa, Tanzanite kubwa zaidi duniani ilikua na uzito wa 3.3KGs na 16,839 carat. Hii ilichimbwa na kampuni ya TanzaniteOne mwaka 2005.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.mining.com Tanzanite hiyo yenye uzito wa 3.3KGs ipo Thailand katika mji wa Bangkok. Wathai wameamua kuifanya fursa ya utalii. Wanatangazia dunia kwamba "karibu Thailand uone Tanzanite kubwa zaidi". Na watu wanasafiri kila pembe ya dunia kwenda kuona hicho kinachoitwa Tanzanite kubwa zaidi na kupiga nayo picha.

Utalii wa aina yake Kwa kufanya hivyo Thailand iliweza kurudisha fedha ilizotumia kununua Tanzanite hiyo ndani ya miaka minne tu. Na kuanzia 2010 wanapata faida (super normal profit). Mradi huo umeiingizia Thailand pesa nyingi sana na kutoa ajira kwa watu wengi

Sasa ni wakati wa kibao kugeuka. Na sisi tutengeneze kituo tuweke haya mawe ya Laizer na tuiambie dunia kuwa Tanzanite kubwa zaidi ipo Tanzania na si Thailand tena. Watu waje washangae hayo mawe wapige nayo picha watulipe 'dollars" wakamalizie picknick Serengeti. Wakitaka kumuona na mchimbaji ruksa.

Hii itatulipa zaidi kuliko kuyauza haya mawe kama tulivyofanya 2005. Pia itafungua fursa mpya ya utalii wa madini ambayo hatujawahi kuwa nayo. Tuige kwa Wathai lakini tufanye kwa ubora kuliko wao (ujasusi wa kiuchumi).

Kama watu waliweza kusafiri kutoka Marekani, China, UK etc kwenda kushangaa Tanzanite ya 3KGs kule Bangkok, sisi tukisema tunayo ya 9KGs hata shetani si anaweza kuja kushangaa kidogo akapate cha kusimulia kuzimu?
 
----
Saniniu Laizer mchimbaji mdogo wa madini huko Mererani ameamka Bilionea baada ya kupata mawe mawili ya Tanzanite moja lenye uzito wa 9.2KGs na jingine 5.8KGs yenye thamani ya TZS 7.8 Bilioni.

Watu wengi wanajadili kuhusu Tanzania kumpata Bilionea mpya. Ni jambo zuri lakini kuna jambo jingine ambalo halijadiliwi. Na pengine ni la msingi zaidi kuliko Ubilionea wa Laizer.

Hii Tanzanite ya 9.3KGs inaweza kuwa ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana duniani. Hii ndio "angle"ya habari, ambayo inaweza ikabreak (as breaking news) ikatoa day 2 story na ikatengenezewa developing story hata kwa mwezi mzima.

Kabla ya Laizer kuushangaza ulimwengu kwa kuchimbua ardhi na kupata madini haya makubwa kabisa, Tanzanite kubwa zaidi duniani ilikua na uzito wa 3.3KGs na 16,839 carat. Hii ilichimbwa na kampuni ya TanzaniteOne mwaka 2005.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.mining.com Tanzanite hiyo yenye uzito wa 3.3KGs ipo Thailand katika mji wa Bangkok. Wathai wameamua kuifanya fursa ya utalii. Wanatangazia dunia kwamba "karibu Thailand uone Tanzanite kubwa zaidi". Na watu wanasafiri kila pembe ya dunia kwenda kuona hicho kinachoitwa Tanzanite kubwa zaidi na kupiga nayo picha. Utalii wa aina yake.

Kwa kufanya hivyo Thailand iliweza kurudisha fedha ilizotumia kununua Tanzanite hiyo ndani ya miaka minne tu. Na kuanzia 2010 wanapata faida (super normal profit). Mradi huo umeiingizia Thailand pesa nyingi sana na kutoa ajira kwa watu wengi.

Sasa ni wakati wa kibao kugeuka. Na sisi tutengeneze kituo tuweke haya mawe ya Laizer na tuiambie dunia kuwa Tanzanite kubwa zaidi ipo Tanzania na si Thailand tena. Watu waje washangae hayo mawe wapige nayo picha watulipe 'dollars" wakamalizie picknick Serengeti. Wakitaka kumuona na mchimbaji ruksa.

Hii itatulipa zaidi kuliko kuyauza haya mawe kama tulivyofanya 2005. Pia itafungua fursa mpya ya utalii wa madini ambayo hatujawahi kuwa nayo. Tuige kwa Wathai lakini tufanye kwa ubora kuliko wao (ujasusi wa kiuchumi).
_
Kama watu waliweza kusafiri kutoka Marekani, China, UK etc kwenda kushangaa Tanzanite ya 3KGs kule Bangkok, sisi tukisema tunayo ya 9KGs hata shetani si anaweza kuja kushangaa kidogo akapate cha kusimulia kuzimu?
 
Untitled-design5.jpg

Leo Record mpya ya Jiwe kubwa la Tanzanite imefikiwa baada ya mawe mawili yenye kilo 9 na 5 kupatikana Mererani Tanzania.

Apo awali, Mwaka 2005 lilipatikana jiwe lenye kilo 3.37(16,839 carats). Lililopewa jina la "Mawenzi"( Kilimanjaro’s second highest peak). Hili jiwe lilipatikana katika machimbo ya kampuni ya Tanzaniaone. Ltd.

The%20largest%20Tanzanite%20crystal%20ever-geology%20in.jpg

Ami Mpungwe, aliyekuwa mwenyekiti msaidizi wa TanzaniteOne.ltd alihaidi jiwe hilo kukatwa na kupolishiwa hapa hapa Tanzania na kupelekwa katika Jumba la makumbusho la Tanzania.

Cha kushangaza, hili jiwe halipo kwenye National Museum of Tanzania na halijulikani lipo wapi hivi sasa. ( kwa anayejua lilipo alete ushahidi).

Leo hii Tumepata mawe makubwa mawili ambayo yote kwa pamoja yamevunja Record. Yani limepatikana la kwanza ambalo ni mara 3 ya Mawenzi na la pili ambalo linazidi mawenzi kwa 2kg. Mawenzi sasa linakuwa la Tatu kwa ukubwa.

Haya yanaweza kuwa kivutio kikubwa cha utalii hapa Tanzania. Hebu fikiria Tanzanite kubwa kuliko zote duniani inayopatikana Tanzania tu na ipo katika jumba la makumbusho lililopo Tanzania.

Watamiminika watalii kila kona kuja kushuhudia Jiwe hili hili la ajabu.

Ushauri wangu; Serikali kwakuwa imeamua kununua jiwe hili. Basi isikimbilie kuliuza pia. Uwekwe utaratibu wa kulikata na kulipolish vizuri na kulidisply katika National musium of Tanzania. Hii inaweza kuwa fursa hata kwa watanzania kujionea jiwe hili linalopatikana nchini kwao tu.

Nacho omba tu, msije yapa haya mawe jina la "Hapa kazi tu".
 
Sijui simu ya RAİS ilikuwa inatufundisha hili au lile la kwanza! Natafakari
 
Back
Top Bottom