Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,999
Wakati serikali ya Tanzania imekuwa katika hali ya ukata wa kifedha nchini na kusababisha baadhi ya miradi na malipo mbalimbali kushindwa kufanyika serikali hiyo hiyo imekamilisha ununuzi mwingine mkubwa wa tatu wa majengo nchini Marekani ndani ya miaka miwili. Serikali ya Tanzania imekamilisha ununuzi wa jengo kubwa huko New York ambalo limegharimu dola za Kimarekani milioni 24.5 karibu sawa na shilingi bilioni 41.6 za Tanzania.
Jengo hilo jipya liitwalo Timekeeper Building (pichani) ni la ghorofa sita na lenye ukubwa wa futi 40,000 za mraba lipo jijini New York karibu na Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Jengo hilo limenunuliwa toka kampuni ya madalali wa majengo ya Amerimar ya huko Philadelphia jimbo la Pennsylvania. Kampuni ya Amerimar ilinunua jengo hilo mwaka 2005 kwa gharama ya dola milioni 15.45 kutoka kwa kampuni nyingine ya Mittman Associates. SOMA ZAIDI KWENYE FIKRAPEVU