Tanzania Yatakiwa Kuwa na Vyanzo Vingi vya Umeme Ili Kufikia Megawati 10,000

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
PROF. SOSPETER MUHONGO - TANZANIA IWE NA VYANZO VINGI VYA UMEME KUFIKIA MEGAWATI 10,000 ILI KUKUZA UCHUMI NA PATO LA WATANZNAIA

Mbunge wa Musoma Mjini (CCM), Mhe. Profesa Sospiter Muhongo ameshauri kupunguzwa bei ya umeme ili Watanzania wengi waweze kuutumia. Profesa Muhongo ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 19, 2023 wakati akichangia mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/24.

Mhe. Profesa Sospiter Muhongo amependekeza bei ya umeme ipunguzwe sasa hivi umeme majumbani ni Dola za Marekani senti 9.7 na viwandani ni senti 10.

"Nchi ya Kenya wako juu (bei ya umeme) lakini siyo sababu, sisi tusipunguze bei ya umeme kwa sababu nchi za Afrika Mashariki ni bei ya juu. Bei ikiwa chini watumiaji watakuwa wengi" - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Hata hivyo, Mhe. Profesa Sospiter Muhongo amesema ili uchumi uweze kukua kwa kasi unahitaji umeme wa uhakika na hivyo inatakiwa kufikisha zaidi ya Megawati 10,000.

Aidha, Mhe. Profesa Sospiter Muhongo ametaja kitu kingine kitakachofanya uchumi kukuwa kwa kasi na kupunguza umasikini ni kuwekeza kwenye uchumi wa gesi mbali na maeneo mengine.

Mhe. Profesa Sospiter Muhongo Ameshauri bajeti ijayo kuweka mkazo katika umeme wa gesi trilioni 57.5 ni nyingi lakini hatujafanya kazi zaidi.

"Tanzania lazima tutafute Mafuta na Gesi kwa bidii zaidi na ndio maana hadi leo ninaamini TPDC (Shirika la Maendeleo la Mafuta Tanzania) kufanya kazi ya uagizaji wa Mafuta na kila mtu hawezi kutafuta Mafuta na Gesi" - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Wangapi wamepata fursa kwenye hicho Kijiji kupata umeme? Ripoti zetu zinapotoka serikalini ni lazima zitaje hizo takwimu badala ya kusema vijiji na vitongoji, Utakuwa hujajibu hoja Kiuchumi" - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Uchumi wa Tanzania lazima ukue zaidi ya asilimia nane, tunahitaji umeme mwingi na wa bei nafuu na Kipimo cha Uchumi siyo kusema unafikisha umeme kwenye Kijiji au Kitongoji suala linakuja ni wangapi kwenye hicho kitongoji wanatumia huo umeme" - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Lazima tutafute gesi na mafuta, TPDC iache kuuza mafuta bali itafute mafuta kwenye maziwa muhimu ili tuwe na uchumi wa mafuta na gesi. Ili uchumi wa nchi ukue na tufikie ukuaji uchumi wa 8%, inatakiwa tuwe na umeme mwingi usipungua megawati 10,000. - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), liache kazi ya kuuza mafuta yanayotoka nje ya nchi, badala yake lijikite kutafuta Mafuta na Gesi Asilia, ili yaanze kuchimbwa kwa ajili ya kusaidia nchi kupata maendeleo" - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Bei ya umeme napendekeza ipunguzwe, Kenya wako juu lakini hii sio sababu ya kutufanya sisi tusipunguze sababu nchi za Afrika Mashariki umeme uko juu. Bei ikiwa chini watumiaji watakuwa wengi na umeme utazalishwa kwa wingi" - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Unaweza fikisha umeme kwenye kijiji na vitongoji vyote, suala linakuja wangapi kwenye hicho kitongoji wanatumia umeme? Sasa naomba ripoti zetu zinapotoka serikalini zitaje hizo takwimu" - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Napendekeza kuwepo na vyanzo vingi vya kuzalisha umeme ili Tanzania iweze kuzalisha zaidi ya Megawati 10,000 hali itakayopelekea kukuza uchumi na kuongeza pato kwa Watanzania" - Mhe. Profesa Sospiter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Mhe. Profesa Sospiter Muhongo ameyasema leo Juni 19, 2023 bungeni Dodoma wakati akichangia mjadala wa kupitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
 

Attachments

  • Fy-j5P6X0AEy3Bl.jpg
    Fy-j5P6X0AEy3Bl.jpg
    42.1 KB · Views: 3
  • NSxe1jmR.jpg
    NSxe1jmR.jpg
    85.3 KB · Views: 3
  • Fy_JrhyXoAE3J9V.jpg
    Fy_JrhyXoAE3J9V.jpg
    39.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom