Tanzania ya Rais Samia itapokea Viongozi wakubwa kutoka Mataifa mbalimbali Duniani

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,346
9,777
Ndugu zangu watanzania,

Kwa Sasa Tanzania chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa serikali ya CCM mikononi mwa Rais Samia inatazamwa kwa jicho la Tofauti na mataifa makubwa na viongozi wakubwa kutoka Mataifa makubwa yaliyoendelea kiuchumi kiviwanda , kiteknolojia na yenye demokrasia imara.

Tanzania kwa Sasa inatazamwa na kuonwa Kama Taifa kiongozi Barani Afrika katika suala Zima la utawala Bora na utawala unaozingatia misingi ya kisheria, Tanzania inachukuliwa Kama nchi iliyopevuka katika suala la demokrasia, Uhuru wa vyombo vya habari,Uhuru wa kujieleza ,uhuru wa kukusanyika, uhuru wa mikutano kwa vyama siasa na kuzingatia haki za binadamu.

Ndio sababu ya viongozi wakubwa Kama makamu wa Rais wa marekani kufungua njia kuja na kuitembelea Tanzania, kila mmoja wetu Ajiulize ndugu zangu Bara la Afrika Lina nchi ngapi? Kwanini Kati ya nchi Tatu atakazo Tembelea makamu wa Rais wa marekani Kati ya nchi 54 zilizopo Barani Afrika Tanzania imepata fursa hiyo ya kupokea ugeni huo mzito kabisa na wa heshima kabisa?

Kutembelewa na kupokea ugeni mkubwa Kama huo kutoka marekani kuna faida nyingi Sana za kiuchumi na kibiashara kwa kuwa Mara nyingi viongozi hao huambatana na wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa Sana, macho na masikio yote ya Dunia yataelekezwa Tanzania siku hiyo, watalii wote na wafanyabiashara kutoka kila pembe ya Dunia wataelekeza Tanzania siku hiyo.

siku hiyo Rais wetu na mama yetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Ataitetemesha na kuisimamisha Dunia kwa Hotuba Yake nzito na ya kuteka Hisia za watu Kama ilivyo kawaida yake ya kutoa hotuba nzuri na za kugusa mambo ya msingi huku akiwa katika Hali ya utulivu mkubwa Sana na kujiamini kwa hali ya juu Kama ilivyo kawaida yake mama yetu, Hakika watanzania siku hiyo tutakuwa Raha tupu na furaha kumuona na kumtizama Rais wetu akihutubia na kutoa hotuba inayotazamwa na kusikilizwa Dunia nzima.

Naamini Viongozi wengi Sana kutoka Mataifa makubwa watatua hapa Tanzania ,maana kwa Sasa Tanzania ndio chaguo namba moja na Tamanio la kiongozi yeyote yule kufika Tanzania na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia,Hakuna kiongozi asiye Tamani kuja na kuitembelea Tanzania kwa Sasa.

Kwa hakika haya Ni matunda ya kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Rais wetu mama Samia katika kuliheshimisha Taifa letu kimataifa ,ndio sababu kwa Sasa Tanzania ndio habari ya mjini, Rais wetu mama Samia Ndio kiongozi mwenye ushawishi mkubwa Sana Barani Afrika na Duniani na Ambaye mawazo na mchango wake wa kihoja umeleta Taswira mpya Sana katika Bara la Afrika hasa katika usimamizi Bora wa Rasilimali za Afrika kwa manufaa ya waafrika katika kutokomeza umaskini Barani Afrika.

Watanzania Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu mama Samia katika kazi kubwa anayoifanya katika kuwatumikia watanzania kwa moyo wa upendo na uzalendo mkubwa Sana ,Dunia imetambua mchango wa Rais Samia katika kuibadilisha Dunia,kuleta Tabasamu na matumaini kwa wananchi mbalimbali ndani ya Afrika,hivyo Hatuna budi kujivunia heshima hii anayoendelea kutupatia watanzania, Tusimkatishe Tamaa Bali Tumpe faraja na Kuendelea kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Wakija watasaini mikataba mingapi tujulishane mapema
ila mikataba iandikwe kiswahili maana wengi kiingerza chetu cha kuunga unga
 
So what?
 
Kupokea viongozi/mabeberu ni sifa? Inamsaidia nini mwananchi wa kawaida?
Fungua akili yako wewe, Beberu yupi unayemzungumzia wewe? Dunia Ni Kama Kijiji kwa Sasa, Tanzania haiwezi ikajitenga na Dunia na Wala haiwezi ikakaa Kama kisiwa ,Ni lazima Tushirikiane na wenzetu katika suala Zima la kiuchumi na maendeleo ya mwanadamu,
 
Wakija watasaini mikataba mingapi tujulishane mapema
ila mikataba iandikwe kiswahili maana wengi kiingerza chetu cha kuunga unga
Tuwe na Imani na serikali yetu kutokana na uzalendo mkubwa iliyonayo katika kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu
 
Wakija watasaini mikataba mingapi tujulishane mapema
ila mikataba iandikwe kiswahili maana wengi kiingerza chetu cha kuunga unga
Mikataba Ni Siri kwa maslahi mapana ya pande zote mbili,kikubwa Ni uzalendo ,kuisoma na kuielewa pamoja na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa
 
Uzuri siku hizi wagombanao ni chawa wa mama na watunza legacy.Wengine huwa tunaingilia ugomvi kwa makosa au kutokujua.Pambaneni hadi mng'oane meno.Luca,ongeza dozi!
 
Naamini Viongozi wengi Sana kutoka Mataifa makubwa watatua hapa Tanzania ,maana kwa Sasa Tanzania ndio chaguo namba moja na Tamanio la kiongozi yeyote yule kufika Tanzania na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia,Hakuna kiongozi asiye Tamani kuja na kuitembelea Tanzania kwa Sasa.
Kwa msingi huo huo nina imani atachagua viongozi wa kuwakaribisha kutoka mataifa hasa yenye nia njema na Tanzania.

Ajiepushe na mataifa ambayo yanataka watanzania tuache kuthamini misingi ya familia ya baba na mama, pia ajiepushe na mataifa ambayo yanaharibu fikra za wanasiasa wetu vijana. Wanasiasa hawa wanaenda huko na fikra pevu wakirudi huku wana fikra mbichi na zilizobunguliwa.

Hao nasema asiwakaribishe, nawaza sisemi!
 
Uzuri siku hizi wagombanao ni chawa wa mama na watunza legacy.Wengine huwa tunaingilia ugomvi kwa makosa au kutokujua.Pambaneni hadi mng'oane meno.Luca,ongeza dozi!
Tanzania Ni moja na CCM Ni moja na wamoja chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani Rais Jasiri mzalendo imara shupavu na madhubuti
 
Back
Top Bottom