Tanzania usipofisadi serikalini - adhabu ni hii

Kama tutakubali kubaki maskini tunaweza kuwa Ethical, nina maana 2kikubali mfumo wa ujamaa 2naweza kuwa ethical.
Katka mfumo wa uchumi wa kibepari haiwezekani kuwa Ethical.
Ufisadi is there 2 stay!
Ukiona m2 anapiga kelele ni kwasababu hajauona mfereji wa kuchota, akishauona kimyaa.
 
wafundishwe na sisi wenyewe wazazi wa sasa wenye watoto wadogo,tukianzia hapo nafikiri labda itasaidia kuwa na kizazi chenye maadili.
 
Mkuu,
Hii nadhani itakuwa ngumu kidogo. Mimi nakumbuka nilipokuwa mdogo(6-7yrs) huko kipindi cha nyuma nilikuwa nikipita jikoni nyumbani na kukuta nyama inachemshwa nilikuwa nanyakua Kama paka jizi na kukimbilia uwani kula..bila kujali nilikuwa naihujumu familia yetu,huku lawama zote zikienda kwa dada (house girl) kwamba ndiye aliyekuwa akifanya ufisadi wa mboga. Arobaini zangu zilifika nikakamatwa na mfupa uwani,nikatandikwa na fimbo ya mpera na tabia ya uhujumu mboga ikakomea hapo.

Kwa hiyo kuna uwezekano kabisa hivi vitabia tunavyo tokea utoto. Inahuzunisha lakini ndio ukweli.

Kwa hiyo unashauri tuwatafutie fimbo za mpera hawa mafissad ili waache kama wewe? Nimefurahishwa sana na comment yako
 
mafisadi sio serikalini tu, hata kwenye sekta binafsi. nilikuwa na kiduka changu cha dawa baridi nimemuweka mdada aniuzie nikienda kazini anaenda kkoo anachukua dawa zake ndio anauza hapo dukani zangu haziuziki mpaka nikafunga duka ndio jirani akaja kunipa hiyo siri. ukienda posta kwenye maduka ya wahindi wauzaji wanakwambia hii bidhaa inauzwa 300000,lakini nenda pale mlangoni umpe mlinzi 150000 na bidhaa utaikuta hapohapo! ukikaa ofisini unaletewa saa ya 300000 unaambiwa lete 150000, ukiuliza imetoka wapi unaambiwa imeibiwa airport! usiache mafundi wakutengenezee matofali wakati haupo watabadilisha ratio bila kujali ubora utajijua mwenyewe na nyumba yako
hayo ni machache niliyokutana nayo, sasa niambieni tunaanzia wapi kurekebisha hii hali!!

Nimechoka mwili mzima. Ila mimi naona jukumu hilo wakipewa wanahabari yaani magazeti, Radio na Tv ili wapandikize mbegu ya uzalendo kwa watoto wanaokua bila kuwasahau walimu has wale wa primary na secondary.
Matangazo yanayofaa kwenye Tv ni yale yanayotangaza biashara huku yakihimiza Maadili mema kama lile la safari larger. yeyote atakaye liangalia atahamasika kufanya kazi kwa kujituma sana ili kufikia malengo yake. Tangazo kama la Godoro la commfy linahamasisha rushwa, eti mtu kakamatwa anauza godoro feki la comfy anamwambia mnunuaji asimshitaki polisi ili ampe godoro halisi la comfy bure. Kama sio kufundisha na kuhamasisha rushwa ni nini hii?
 
Kama tutakubali kubaki maskini tunaweza kuwa Ethical, nina maana 2kikubali mfumo wa ujamaa 2naweza kuwa ethical.
Katka mfumo wa uchumi wa kibepari haiwezekani kuwa Ethical.
Ufisadi is there 2 stay!
Ukiona m2 anapiga kelele ni kwasababu hajauona mfereji wa kuchota, akishauona kimyaa.

Si bora hata kama wanachota wazielekeze kwenye uwekezaji hapa nchini ili waTz wafaidike na ongezeko la ajira. Walivyowajinga wanapeleka benki za nje ama wanawekeza nchi za nje bula kujua kuwa wanaendeleza nchi za wenzao na kuacha ya kwao ikisuasua. Lakini Maisha Bila ufisadi yanawezekana hata katika mfumo wa kibepari
 
wafundishwe na sisi wenyewe wazazi wa sasa wenye watoto wadogo,tukianzia hapo nafikiri labda itasaidia kuwa na kizazi chenye maadili.

Mkuu hao unaowaita wazazi ndio ambao mtoto wake akiokota bunda la pesa na kumpelekea aliyedondosha, nyumbani hapakaliki. Atamtandika mtoto na kumwita kila jina baya, mara kenge we! mjinga mkubwa.. ua unataka usile leo.. nisikilize vizuri we litoto lipuuzi, sikunyingine ukiokota pesa ficha na kimbia nyumbani uniletee.sawasawa?(kwa ukali na kitisho)
 
mafisadi sio serikalini tu, hata kwenye sekta binafsi. nilikuwa na kiduka changu cha dawa baridi nimemuweka mdada aniuzie nikienda kazini anaenda kkoo anachukua dawa zake ndio anauza hapo dukani zangu haziuziki mpaka nikafunga duka ndio jirani akaja kunipa hiyo siri. ukienda posta kwenye maduka ya wahindi wauzaji wanakwambia hii bidhaa inauzwa 300000,lakini nenda pale mlangoni umpe mlinzi 150000 na bidhaa utaikuta hapohapo! ukikaa ofisini unaletewa saa ya 300000 unaambiwa lete 150000, ukiuliza imetoka wapi unaambiwa imeibiwa airport! usiache mafundi wakutengenezee matofali wakati haupo watabadilisha ratio bila kujali ubora utajijua mwenyewe na nyumba yako
hayo ni machache niliyokutana nayo, sasa niambieni tunaanzia wapi kurekebisha hii hali!!

Ukweli mtupu huo mkubwa tena kama kuna bidhaa zinakaa ndani ya mabox usisite kufungua ili kujiridhisha kama bado zimo. Unaweza ukawa unaonyeshwa mabox tupu huku mali ilishauzwa kitambo
 
Back
Top Bottom