Tanzania, Uganda kuzalisha umeme wa MW 16

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125











Sitta2(36).jpg





Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta


Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini hati ya makubaliano ya kuanzisha mradi wa pamoja wa nishati ya umeme utokanao na maji katika maporomoko yaliyo katika eneo la Murongo mkoani Kagera nchini, ambao utazalisha megawati 16 zitakazotumika katika nchi hizi mbili za Afrika Mashariki.
Taarifa hii ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikutano miwili ya mawaziri wanaoshughulika na jumuiya hiyo, iliyofanyika hivi karibuni jijini Arusha na katika nchi ya Rwanda.
Sitta alisema mradi huu utakaojulikana kwa jina la ‘Mradi wa Murongo –Kigagati utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani milioni nane (Sh. billioni 20),unatarajiwa kuchukua kipindi cha miezi 12 hadi kukamilika mwakani.
“Kigagati ni eneo ambalo liko katika nchi ya Uganda. Mradi huu utakapokamilika utamaliza matatizo yote ya umeme katika maeneo yaliyo katika mpaka wa nchi hizi mbili na kwamba kila nchi itachukua nusu ya megawati zitakazozalishwa.Fedha za kuugaharimia mradi huu, tumezikopa toka katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB),” alisema.
Alifafanua kwamba mradi huu ni mfano wa kile ambacho kimekuwa kikisisitizwa katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) ambapo nchi zimekuwa zikihimizwa kushirikiana kuanzisha miradi ya maendeleo ambayo itakuwa na tija kwa wananchi wa nchi za EAC.
Wakati huo huo Sitta alisema Bunge la Afrika Mashariki limepitisha sheria ya kuanzishwa kwa Taasisi ya mafunzo ya Mabunge ya EA, ambayo itatumika kutoa mafunzo kwa wabunge na wafanyakazi wa Mabunge badala ya kuendelea kutumia fedha nyingi kuwapeleka nje ya ukanda huu kupata mafunzo hayo.
“Hatukuwa na taasisi ya aina hiyo katika ukanda wetu, na kwa hiyo tulipohitaji kutoa mafunzo kwa wabunge au watumishi wa bunge kwa kozi mbalimbali, ziwe fupi au ndefu tulikuwa tunawapeleka katika mataifa ya nje. Sasa kwa kuanzisha taasisi ya aina hii, itatusaidia sana katika kutujengea mfumo unaofanana katika mabunge yetu,” alisema.





SOURCE: NIPASHE

 
Duh! mkuu hiyo Mg ni kipimo kipya nini????? anywayz waombe mods wakubadilishie iwe MW
 
Back
Top Bottom