Tanzania: Tumecheka sana na nyani, na sasa tunavuna mabua

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,892
3,196
Asalaam Aleykum wana jamvi.

Waswahili walisema, ukicheka nyani, utavuna mabua.

Hiki ndicho kinachotokea Tanzania.

Reports nyingi za CAG zinazoonesha "nyani" wanaolitesa Taifa hili zimekuwa zinapuuzwa kila mwaka, na matokeo yake ndo haya tunayoyaona sasa.

Sauti za Watanzania wengi wazalendo kwa nchi yao, imekuwa ikipuuzwa juu ya "nyani" waharibifu na matokeo yake ndo haya hapa sasa Tanzania tumekuwa kichekesho kwa majirani zetu!

Mwigulu akiambiwa, anatuambia tuhamie Burundi, haya sasa uchumi umemshinda. Maneno mengi na hakuna chochote anafanya kuimarisha uchumi wa nchi yetu.

Anachojua ni labda kuwahonga tu watu wa IMF ili wamwandikie report nzuri inayoonesha uchumi wetu uko vizuri ilhali hali ni mbaya sana katika historia ya nchi yetu.

Na nachelea kusema kwamba, endapo hali ikiendelea hivi kwa miezi mingine 6 ijayo, nchi yetu itatangaza "kufilisika" kama ilivyotokea kwa Ugiriki miaka kadhaa nyuma.

Just imagine, we have no enough sugar, no US dollars, no enough electricity, costs of living are at their peaks! (Hebu angalia, hatuna sukari ya kutosha, hatuna dola, hatuna umeme wa kutosha, gharama za maisha ziko katika vilele vyake)!

Halafu ukisema, anajitokeza "nyani" mmoja hivi mzee anakwambia "Hamia Burundi"!

Something must be done to rescue the situation (kitu fulani lazima kifanyike ili kuokoa jahazi).

Naomba kuwasilisha.

20240219_060553.jpg
20240219_060621.jpg
 
Hapo kwenye ripoti ya CAG, mimi mpaka siifuatilii tena siku hizi maana ina faida gani? Ubadhirifu unatajwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa waziwazi zikaonekana.

Ripoti yenyewe inasomwa na kuwekwa hadharani, na makabidhiano na Rais ni hadharani pia. Kwanini wahusika wa ubadhirifu huo wasishughulikiwe hadharani pia?
 
Asalaam Aleykum wana jamvi.

Waswahili walisema, ukicheka nyani, utavuna mabua!
Akina sisi hili tumeliuliza sana humu Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?
Halafu ukisema, anajitokeza "nyani" mmoja hivi mzee anakwambia "Hamia Burundi"!
Wa kuhamia Burundi, tupo tuliishahamia Tulioitika Wito Kuhamia Burundi, Tumefarijika Sana Kumuona Former First Lady, Mama Salma Kikwete. Kumbe Rais Akiwa Mwanamke, Nchi Haina First Lady!
Something must be done to rescue the situation (kitu fulani lazima kifanyike ili kuokoa jahazi).

Naomba kuwasilisha.
Please suggest!.
P
 
Hapo kwenye ripoti ya CAG, mimi mpaka siifuatilii tena siku hizi maana ina faida gani? Ubadhirifu unatajwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa waziwazi zikaonekana.

Ripoti yenyewe inasomwa na kuwekwa hadharani, na makabidhiano na Rais ni hadharani pia. Kwanini wahusika wa ubadhirifu huo wasishughulikiwe hadharani pia?
Halafu gharama za kendesha hiyo ofisi ni kubwa sana lakini product yake hailiwi. Kuna maana gani kulima shamba vizuri halafu mazao yake hayaliki wala kuuzika?
 
Asalaam Aleykum wana jamvi.

Waswahili walisema, ukicheka nyani, utavuna mabua.

Hiki ndicho kinachotokea Tanzania.

Reports nyingi za CAG zinazoonesha "nyani" wanaolitesa Taifa hili zimekuwa zinapuuzwa kila mwaka, na matokeo yake ndo haya tunayoyaona sasa.

Sauti za Watanzania wengi wazalendo kwa nchi yao, imekuwa ikipuuzwa juu ya "nyani" waharibifu na matokeo yake ndo haya hapa sasa Tanzania tumekuwa kichekesho kwa majirani zetu!

Mwigulu akiambiwa, anatuambia tuhamie Burundi, haya sasa uchumi umemshinda. Maneno mengi na hakuna chochote anafanya kuimarisha uchumi wa nchi yetu.

Anachojua ni labda kuwahonga tu watu wa IMF ili wamwandikie report nzuri inayoonesha uchumi wetu uko vizuri ilhali hali ni mbaya sana katika historia ya nchi yetu.

Na nachelea kusema kwamba, endapo hali ikiendelea hivi kwa miezi mingine 6 ijayo, nchi yetu itatangaza "kufilisika" kama ilivyotokea kwa Ugiriki miaka kadhaa nyuma.

Just imagine, we have no enough sugar, no US dollars, no enough electricity, costs of living are at their peaks! (Hebu angalia, hatuna sukari ya kutosha, hatuna dola, hatuna umeme wa kutosha, gharama za maisha ziko katika vilele vyake)!

Halafu ukisema, anajitokeza "nyani" mmoja hivi mzee anakwambia "Hamia Burundi"!

Something must be done to rescue the situation (kitu fulani lazima kifanyike ili kuokoa jahazi).

Naomba kuwasilisha.

View attachment 2908619View attachment 2908620
Tuwaunge mkono wapinzani la sivyo tutavuna mabua!
 
Mama aanze kuweka plan ya kubana matumizi yaa serikali ikiwemo kupunguza safari za nje sasa, yeye na watu wake.

Serikali iwe serious Sasa kudhibiti wizi na majizi waliojazana Kila Kona hivi Sasa na wengi wao hizo hela wanaficha nje na kununua vitu vya anasa kama magari ambavyo vingi hutoka nje

Tuanze kuacha kununua vitu visivyo na ulazima nje, kama furnitures, magari na matumizi mengine ya serikali na taasisi zake.

Tuache sasa kununua midege baadala yake tujikite kuongeza ufanisi kwa hizi zilizopo hasa kuzitafutia route nyingi za nje.

Serikali ianze Sasa kuwa serious kuwekeza kwenye kilimo cha kisasa na kuwawezesha wakulima vitendea kazi na kutafutia mazao yetu masoko serious.

Serikali ifikiri namna ya kuhakikisha viwanda vya nguo vya ndani vinafanya production ya kutosha na nguo quality ili tuache utegemezi wa kuagiza mitumba na nguo kutoka China.

Serikali iache kujenga jenga hovyo Kwa kutumia wakandarasi wa nje, baadala yake ijikite kutumia na kuwawezesha wakandarasi wa ndani, ujenzi ufanyike tu pale kwenye ulazima na sio Kila siku tunajengajenga tu hovyohovyo.

Mambo ni mengi sana, wengine wanaweza kuongeza hapo.
 
Halafu ukisema, anajitokeza "nyani" mmoja hivi mzee anakwambia "Hamia Burundi"!
Hahahaha Mshana Jr na mhamie Burundi enyi warundi hahahah. Unajua Rais Dkt Samia aliambiwa toka mwanzo amfukuze Dkt Mwigulu, amfukuze Makamba, amfukuze Baashe, amfukuze Dkt Ashatu ila basi yeye anawaonea huruma, na bado mchwa wataendelea kuitafuna hii nchi hatari, tuvumilie tu maana mambo ndivyo yalivyo hahaha.
 
Hapo kwenye ripoti ya CAG, mimi mpaka siifuatilii tena siku hizi maana ina faida gani? Ubadhirifu unatajwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa waziwazi zikaonekana.

Ripoti yenyewe inasomwa na kuwekwa hadharani, na makabidhiano na Rais ni hadharani pia. Kwanini wahusika wa ubadhirifu huo wasishughulikiwe hadharani pia?
Hahshaaaa," Mtanikumbuka,tena si kwa mabaya ila mi kwa mema.
 
Hapo kwenye ripoti ya CAG, mimi mpaka siifuatilii tena siku hizi maana ina faida gani? Ubadhirifu unatajwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa waziwazi zikaonekana.

Ripoti yenyewe inasomwa na kuwekwa hadharani, na makabidhiano na Rais ni hadharani pia. Kwanini wahusika wa ubadhirifu huo wasishughulikiwe hadharani pia?
Rais anaishia tu kuwatukana stupid na hakuna tena kitu wanafanywa!
Labda wanamdharau mama
 
Back
Top Bottom