Tanzania ni shamba la bibi

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Imefikia hatua Tanzania yetu nchi yenye mali nyingi na vivutio vya kitalii inaitwa shamba la bibi, cha kujiuliza kweli tumeamua kuiita hivyo? je unavyoimba wimbo wetu wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wotee ni unafiki tu? mimi binafsi naumia sana nikisikia kauli hii ila huwa sina pa kwenda kushitaki.
 
sikubaliani na wewe kwamba tz ni shamba la bibi..........thibitisha umepata wapi na nani kasema habari hizi...............
 
sikubaliani na wewe kwamba tz ni shamba la bibi..........thibitisha umepata wapi na nani kasema habari hizi...............

1. Shirika la Ndege wamelivuna bila aibu
2. Shirika la Reli wamelivuna
3. Shirika la posta na Simu walilivuna bila huruma
4. Tanesco wameivuna ( Enzi ya Tetgroup solutions)
5. Maji Dar es salaam wamevuna - City water wakala pia
6. Nassako - Wakavuna
7. Sekta ya madili - wamevuna
8. Umeme wa Dharula - Wamevuna
9. TTCL - kuingiza Simu Net - Wakavuna kwa ujasiri mkubwa
10.TPDC - wakaivuna bila huruma
11.Mbuga za wanyama - Kule wanavuna ki usani hadi sasa
12.Ndege ya Mnene - wakashiba
13.Rada ya Taifa - wakapata dalali awasaidie kununua - wakalamba vizuri
14. Vihela vilivyokuwa benki kuu ya madeni ya nje wakavigundua -
Wakaamua kuvigawana
15. Reaserch centers za kilimo, ufugaji ya umwagiliaji zilizokuwa zimeanzishwa na mwasisi wetu - wamezigawana / kuzivuna bila aibu



Sasa baadhi ya mifano tu je huwezi kukubaliana na mimi kwamba nchi yetu ni shamba la bibi - Yaani halina Mlinzi? haisaidii kujua nani kasema wewe ndo utoe hoja why LISIITWE SHAMBA LA BIBI KIZEE LENYE KILA KITU ILA HALINA MLINZI?
 
...Minara pacha pale kwenye kihenge kikubwa mjini kati wamejihudumia, Kuna habari mpaka kale kaofisi kadogo ka bunge watu wamejivunia kiulaini, stika za zima moto wanajivunia, Speed governor, wanasubiri kale kamradi ka mabasi jijini wajivunie tena.........
 
Back
Top Bottom