Tanzania ni moja ya nchi zisizo na furaha duniani

Mosalah_

JF-Expert Member
Jul 10, 2018
314
720
Leo katika pita pita zangu mitandaoni, nikakutana na post ikionyesha kwamba Tanzania ni moja ya nchi zisizo na furaha duniani.

Hivi hawa wachambuzi wanatazama nini hasa mpaka wanatoa hizi takwimu?
FB_IMG_1695729466907.jpg
 
Umeme hapa hakuna tangu asubuhi, tutakosa kununa?Hasira, unafuraha na karaha? Maji pia hakuna, bandari, bungeni posho wanajiongezea, mikopo chuo changamoto, dollar adimu, petrol bei juu, vifurushi, gharama za maisha, CCM, tuna sababu million za kukosa furaha
 
Leo katika pita pita zangu mitandaoni, nikakutana na post ikionyesha kwamba tanzania ni moja ya nchi zisizo na furaha duniani.

Hivi hawa wachambuzi wanatazama nini hasa mpaka wanatoa hizi takwimu?
View attachment 2763335
Bunge la kishabiki,mahakama hazitendi haki! Serikali ndio hivyo tena hadi bandari ambayo ni moyo wa uchumi inaenda kumilikishwa Kwa wageni! Mgao wa umeme! Fuel bei juu! Watoto wetu wanateseka kwa kukosa bima za matibabu. Kubambikiwa kesi polisi! Hospitalini hakuna madawa! Wamasai wanafukuzwa kwenye ardhi ya urithi wao. Wanyamapori wanabebwa na ndege kuhamishiwa Kwa wageni n.k Hiyo furaha otatoka wapi. Furaha yetu ni madhabahuni Kwa Mungu wa mbinguni pekee tunapokwenda kumsifu na kumuabudu na ndipo tumaini letu lilipo.
 
Takwimu hizo haziaminiki, 8 kati ya nchi 10 ni za Afrika kusini mwa Sahara. Watueleze Uingereza, Ukraine, Syria, Haiti ziko na. ngapi. Ajabu hata Somalia haipo kwenye hiyo orodha!
 
Wametukosea sana hiyo rank sio sahihi mi naona tuko top 3 maana raia hatuna furaha yoyote kukaa gizani huku unalipa tozo na kodi unakuwa na hasira sana! Vijana hawana ajira , sekta binafsi haiboreshwi, bandari Mali ya waarabu, katiba mbovu, dollar hakuna, raia maskini , wabunge matajiri!

Hii sirikali hakika ni ya kidhalimu au tuseme imeshindwa kazi
 
Wametukosea sana hiyo rank sio sahihi mi naona tuko top 5 maana raia hatuna furaha yoyote kukaa gizani huku unalipa tozo na Kodi unakuwa na hasira sana! Hii sirikali ni dhalimu au tuseme imeshindwa kazi
Mmeibiwa kura?😆😆
 
Umeme hapa hakuna tangu asubuhi,tutakosa kununa?Hasira,,unfuraha na karaha?Maji pia hakuna,bandari,bungeni posho wanajiongezea,mikopo chuo changamoto,dollar adimu,petrol bei juu,vifurushi,gharama za maisha,,CCM,tuna sababu million za kukosa furaha
Kweli kabisa. Changamoto zote hizo kweli wanataka tuwe na furaha tukifurahia nini? Kila kitu kiko ziiii, halafu tunaambiwa tuwe na furaha ?!
 
Umeme hapa hakuna tangu asubuhi,tutakosa kununa?Hasira,,unfuraha na karaha?Maji pia hakuna,bandari,bungeni posho wanajiongezea,mikopo chuo changamoto,dollar adimu,petrol bei juu,vifurushi,gharama za maisha,,CCM,tuna sababu million za kukosa furaha
Umepiga kwenye mshono
 
Wakitoa takwimu za idadi ya watu duniani au thamani ya dola mnaamini ila kwakuwa umeshiba ugali unacheka cheka hovyo bc unadhani wengine wapo kama wewe.
 
Wametukosea sana hiyo rank sio sahihi mi naona tuko top 3 maana raia hatuna furaha yoyote kukaa gizani huku unalipa tozo na kodi unakuwa na hasira sana! Vijana hawana ajira , sekta binafsi haiboreshwi, bandari Mali ya waarabu, katiba mbovu, dollar hakuna, raia maskini , wabunge matajiri!

Hii sirikali hakika ni ya kidhalimu au tuseme imeshindwa kazi
Eti top3 kijana hivi ushawai hata kumiliki passport & VISA angalau uvuke mipaka utembee huko dunian ujionee hali za wananchi wa nchi zingine zinavyotisha kwa kukosa usalama, chakula na unafuu wa maisha?

Ni kwel Tanzania inanuka shida lkn haiwezi kuwepo hata Top50 ya nchi za watu wasio na furaha.

Huwezi kusema hauna furaha na huujui hata mlio wa risasi wala bomu au hata machafuko ya kisiasa huyajui zaid ya kusikia ktk tv, basi hata mapinduzi ya kijeshi hujui yanatokea vipi.

Tz shida kubwa ni umasikini na masikin wa Tz wanafuraha tofauti na masikin wa nchi zingine ambazo hawana furaha kwa changamoto nyingi zikiwepo umasikin,ufinyu wa usalama kwa raia, magonjwa, Siasa mbovu+migogoro ya raia.

Tz bado hatujafikia huko japo shida yetu ni changamoto ya kiuchumi tu, tuache chuki za kitoto Tz nchi ya amani.

Tembeleeni nchi hata jirani mjifunze mambo ya msingi
 
Back
Top Bottom