Tanzania na Zambia kuimarisha uhusiano na ushirikiano

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
"Tumechaguliwa na wananchi ili kuboresha maisha yao, tunatakiwa kushirikiana kama nchi ya Tanzania na Zambia ili kuinua uchumi wa wananchi wetu"

Hii ni kauli ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, aliongea Mwaka jana Agosti, 2022 na waandishi wa habari kipindi ambacho Rais wa Zambia Mhe. Haikande Hichilema alikuja Tanzania kwa ziara ya siku mbili.

Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Zambia yameendelea kuimarika tangu enzi za waasisi wetu kati ya Hayati Julius Nyerere na Kenneth Kaunda.

Mahusiano ya kibiashara na uwekezaji
Licha ya kuwepo kwa Mahusiano na muingiliano wa kibiashara na uwekezaji biana ya wananchi wa mataifa haya mawili, bado kumekuwepo na vikwazo vya kikodi na visivyo vya kikodi ambayo vinakwambisha ukuaji wa biashara zetu.

Ilikukabiliana na changamoto hizo, Rais samia mwaka jana aliongea na Mhe.Rais Hichilema na kukubaliana kuwa sekta za uwekezaji na biashara, zishirikiane kukuza mapato ya mataifa yote mawili, pia kukaa na kutazama vikwazo ambavyo vinavyotukabili ili viondolewe.

Nishati na Kilimo
Ili kuimarisha upatikanaji wa nishati, mataifa haya yamekubaliana kutekeleza mradi wa pamoja wa umeme ambapo Tanzania ilianza utekelezaji wake tangu January 2023.

Kupitia ziara ya Mhe.Rais Dkt.Samia nchini Zambia watajadili Maendeleo ya Mradi wa Bomba la mafuta TAZAMA, Reli ya TAZARA na barabara ya TANZAM.

Mhe.Rais Dkt.Samia yupo nchini Zambia kwa ziara ya kikazi ya Siku 3 kwanzia tarehe 23 hadi 25, ambapo atakuwa mgeni Rasmi maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wa Zambia, atahutubia bunge la Zambia na kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na Zambia.
 
Back
Top Bottom