Tanzania na Israel zasaini mkataba(MoU) wa ushirikiano wa Kijeshi na Kiintelijensia

Thank God our eyes are now opened/Mungu ashukuriwe macho yetu yamefunguka.
Tanzania will gain enormous knowledge and expertise in many fields from Israel.

Tanzania itapata maarifa makubwa sana katika UJUZI wa Isarel
Naamini kuanzia sasa Tanzania haitabaki nyuma.
HONGERA rais Magufuli kwa kulivalia njuga jambo hilo.
 
Na kweli. Nasikia hata makomandoo wetu wakienda kusoma huko kwao, wanapewa assigment, swali linataka ueelezee labda silaha zetu zilipohifadhiwa, basi hapo mwanajeshi wetu anajikunja, anaelezeeeea, utapita hapa, ushuke vile, uende kushoto kisha urudi kulia, mmmmh! (si anatafuta maksi ufaulu). Kwa hiyo wale wazungu wanakuwa tayari wameshajua kila kitu kilipo
Sasa mkuu Israel kujua silaha za Tanzania zilipohifadhiwa inawasaidia nini hasa wao.

Unakumbuka kauli ya Jakaya wakati ule watu wanamlalamikia kuwa amezidisha military show ya silaha za kijeshi kwenye maadhimisho ya Uhuru pale Taifa??

Alisema hakuna siri kwenye mambo ya uhifadhi wa silaha za kijeshi kwa kizazi hiki.

Drone ikipita juu ya kambi ya jeshi ikarusha mionzi , inaweza kugundua kilichoko hata chini ya ardhi mita 5 kwenye chini.
 
Ili watu wajifunze kwako lazima uwe na teknolojia ambayo watu hawana, sasa sisi sijui tuna teknolojia gani ambayo watu hawana, au unamaanisha waje kujifunza hizi blah blah blah na uganga wa kienyeji???
tapatalk_1520427839811.jpeg
Hii teknolojia hawana
 
Ili watu wajifunze kwako lazima uwe na teknolojia ambayo watu hawana, sasa sisi sijui tuna teknolojia gani ambayo watu hawana, au unamaanisha waje kujifunza hizi blah blah blah na uganga wa kienyeji???

Kwenye ulimwengu wa intelijensia kuna kitu kinaitwa "indirect benefits"
Faida inayopatikana japo haionekani kuwa ipo.

Tanzania ndio link ya eneo la maziwa makuu na resources za eneo la maziwa makuu.

Ukiwa karibu na Tanzania ukawa na access naye nzuri maana yake umejipenyeza eneo tajiri la maziwa makuu kwa resources na kila kitu.

Hii kwao kiuchumi ni benefit nzuri sana kuliko mambo ya kivita, ndio maana uliona juzijuzi tu hapa Russia na America na Uchina nao walikuwa hapa.

Wanayo mengi tu ya kufaidika kutoka kwetu.
Tusijidharau
 
Nasikia wameleta meli imejaa kitimoto
ohh hiyo ni habari nzuri.hawa jamaa huko nyuma walikuwa marafiki zetu wakubwa sana si tu waliweza kutusaidia kijeshi pia hata maswala ya mambo ya vyama vya ushirika.Watalaamu wengi wa ushirika walikuwa wanapewa mafunzo ya uendeshaji wa vyama vya ushirika huko israel.So kurudisha uhusiano huo kutakuwa na faida kubwa kwa watalaamu wetu.waisrael ni watu walioendelea sana katk nyanja mbambali hivyo ni fursa kwetu kuitumia nafasi hii kwa ustawi wa nchi na watu wetu pia.
 
....
Tanzania has since established a fully-fledged embassy and ambassadorial presence in the Israeli capital Tel Aviv.
...
Huo ndio unafiki usiotakiwa. Israel Capital ni Mji Mtukufu wa Jerusalem; ubalozi ukafunguliwe kule kule sambamba na ule wa US unaotarajiwa kuhamishiwa huko na Trump.
 
Informer kwa ukanda huu wa East Africa??

Kuna kauli moja huwa inazunguka kwenye intelligence cycles kuwa, ukitaka kuishi vizuri eneo la maziwa makuu, basi jipenyeze Tanzania.

Naona Mossad wamelijua hilo, ndio maana wamekuja.

myahudi hana lolote zaidi ya kuongeza vyanzo vya taarifa tuu ili awe na update za kutosha ukanda wa e.a na maziwa makuu.. ili wakabiliane vyema na matishio ya maslahi ya bwana mkbw US...
 
Watatusaidia sana kutuletea bunduki zao nzuri za UZI Machine gun.


In return wao wanaongeza wigo wa coverege yao kiinteligensia na
kuweka backdoor zao mbalimbali
he he he he
kwani mkuu kuna ubaya kutumia UZI ??

Mbona tunatumiaga magobole na vipande vya nondo kwenye smg badala ya risasi??
 
Back
Top Bottom