Tanzania kutangaza hali ya hatari!?

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,466
9,028
Habari wanajamvi.

Katika pitapita zangu nimekutana na hili tangazo kutoka Jeshi la Ulinzi na Usalama Tanzania (TPDF) na limeniacha na maswali kadhaa. Naombeni mwenye fikira kama zangu aungane name au mwenye fikira tofauti atupe mwanga wa ni nini kinahusiana na tangazo hili.
1. Je yewezekana jeshi la polisi limeshindwa kazi?
2. Je, nchi inaweza kuingia katika hali ya hatari wakati wowote kuanzia sasa?
3. Je, yawezekana utawala wa demokrasia Tanzania umeshindwa?
4. Au tutegemea nini kama nchi!!

Kwa heshima na taadhima nawasilisha
attachment.php
 
Attachments

  • tangazo2.jpg
    tangazo2.jpg
    98.8 KB · Views: 1,026
  • Thanks
Reactions: dry
Maswali yako yana logic, inaelekea kuna kamkakati ka kuliingiza jeshi kwenye baadhi ya mambo hasa kufanya kazi ambazo ni za kipolisi. Na hivyo wanataka justification ya hilo, ili wananchi wakiwaona huko wajue kwamba linatimiza wajibu lilioutangaza.

Maana sioni kabisa mantiki ya hilo tangazo.

Inawezekana wanataka kumkamata Dr. Slaa na wanataka kuwatisha wananchi ili wasiandamane, kwa kuhofia kwamba jeshi litainvene.

Anyway hili halishangazi sana, maana hadi hivi sasa nchi haina kiongozi bali ina vivuli tu vya viongozi ambao kiujumla hawajui wanafanya nini na kwanini wapo pale walipo.
 
Nimelipenda sana hil Tangazo; kwani bila shaka hawataishia hapo tu bali kwa shughuli zote ambazo Jeshi la Polisi linaonekana kushindwa kuwajibika. Mfano vita vya Majambazi, vita ya Ufisadi, wabadhirifu wa mali ya Umma, matumizi yasiyo na lazima ya nguvu za silaha ya moto yanayofanywa na Polisi, Tume zinazoundwa na Jeshi la Polisi kwa nia ya kula pesa za Walalahoi.

Hongera sana Jeshi la Ulinzi tunaomba mchukue majukumu yote ya jeshi la Polisi kwani wameshindwa kazi na wapo kisiasa zaidi.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Tanzania bila shaka tuna majeshi matano kwa sasa(kama sipo sahihi unaweza nisahihisha).
Jeshi la Wananchi.
Jeshi la Polisi.
Jeshi la Kujenga Taifa
Jeshi la Uhamiaji (Mwanzoni ilikua ni idara ndani ya jeshi la Polisi)
Jeshi la Magereza

Jeshi la Wananchi - lipo ili kulinda mipaka ya nchi na usalama wa Taifa kwa ujumla n.k.
Jeshi la Polisi - kulinda raia ndani ya mipaka ya nchi n.k.

Inapotokea vurugu kubwa ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi au usalama wa Amri Jeshi mkuu, moja kwa moja JWTZ wanaingia kazini pasipo mjadala wowote na hicho ndio kinachomaanishwa katika hilo tangazo lao.
 
Hamjui kuwa jeshi lilisaidia kwenye mgomo wa madaktari uchwara?
 
JW walishaona hali inazidi kuwa tete!! EL mwaka huu atawatoa jasho CCM pamoja na serikali yao.
 
Acheni mambo yenu. mi siishi Dar ila naamini Jeshi walikuwa na Banda pale Sabasaba kama hilo tangazo linavyosema tena imesisitizwa "SABASABA 2012" mbona mnapenda kugusa mambo na pia hizo ni kazi ambazo jeshi linafanya.

Better be a greater thinker.
 
Tanzania bila shaka tuna majeshi matano kwa sasa(kama sipo sahihi unaweza nisahihisha).
Jeshi la Wananchi.
Jeshi la Polisi.
Jeshi la Kujenga Taifa
Jeshi la Uhamiaji (Mwanzoni ilikua ni idara ndani ya jeshi la Polisi)
Jeshi la Magereza

Jeshi la Wananchi - lipo ili kulinda mipaka ya nchi na usalama wa Taifa kwa ujumla n.k.
Jeshi la Polisi - kulinda raia ndani ya mipaka ya nchi n.k.

Inapotokea vurugu kubwa ambayo inaweza kuhatarisha amani ya nchi au usalama wa Amri Jeshi mkuu, moja kwa moja JWTZ wanaingia kazini pasipo mjadala wowote na hicho ndio kinachomaanishwa katika hilo tangazo lao.
Kilichowatuma kutangaza leo ni nini? Kwani wameona kuna tatizo gani hadi wajipendekeze kutoa tangazo la aina hii?
 
Hamjui kuwa jeshi lilisaidia kwenye mgomo wa madaktari uchwara?
kwa juu inaonekana hivyo lakini mimi naona katangazo haka kanaweza kuwa kamebeba 'makubwa' nyuma yake.
Ni kwa nini kalipiwe, japo ni ujumbe wa sabasaba!
Kilichowatuma kutangaza leo ni nini? Kwani wameona kuna tatizo gani hadi wajipendekeze kutoa tangazo la aina hii?
mkuu, ndio wanaoishi mijini wanasema sio kila unachokiona kinamaanisha maana ya juu ..."hata ukimuona ngedere ujue ana mwenyewe"

Acheni mambo yenu. mi siishi Dar ila naamini Jeshi walikuwa na Banda pale Sabasaba kama hilo tangazo linavyosema tena imesisitizwa "SABASABA 2012" mbona mnapenda kugusa mambo na pia hizo ni kazi ambazo jeshi linafanya.

Better be a greater thinker.
ukifikiria sana unaweza kugundua tofauti na ulichoandika lakini mbali na hapo usisumbuke sana bali muda utakuja kutueleza ukweli wa hili 'tangazo' mkuu

hawawezi kushindana na nguvu ya umma wakaulize misri,libya,tunisia nini kilitokea
 
Hamjui kuwa jeshi lilisaidia kwenye mgomo wa madaktari uchwara?
Unafikia kutukashifu kwa mapenzi yako na watawala unakumbuka 1987/1988 tulichofanya MMC kuwashughulikia polisi uchwara waliotumwa kutupiga virungu kwa kudai haki zetu, Madaktari askari waliokuja kutibu kipindi cha mgomo waliunga mkono asilimia 500% matokea wanayajua waliokuwa na ndugu zao pale mmc tafadhali soma hati ya kiapo cha madaktari ujue Hoja yako haiendani na tangazo changia hoja, ninyi mtalipwa hapa duniani utaomba kufa hautakufa Mungu anajua mema na mabaya ya kila mmoja wetu
 
Back
Top Bottom