Tanzania kupokea ndege mbili aina ya Bombardier C-Series mwezi Novemba 2018

-DODOMA

SERIKALI imeahidi kuleta ndege nyingine mbili za C Series ifikapo Novemba mwaka huu na Boeing nyingine Januari 2020, ikiwa na lengo la kutimiza ndoto yake ya kuhakikisha inafufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Ndege hizo zitakazowasili zitakuwa ni mwendelezo wa ndege zilizofika nchini awamu ya kwanza aina ya Bomberdiar na hivi karibuni kushuhudia kuwasili kwa ndege nyingine Boeing 878 Dreamliner.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi, alisema manufaa ya ndege hizo yameanza kuonekana na zinasaidia wananchi wengi kusafiri na kufanya biashara zao kwa haraka.

“Tangu tulete ndege hizi abiria wa ATCL waliongezeka hadi kufikia 107.207 katika mwaka 2016/17 wakati mwaka 2015/16 walikuwa 49,173 ikiwa ni ongezeko la asilimia 118,” alisema Dk. Abbasi.

Akizungumzia gawio la mashirika ya umma kwa serikali, alisema yemekuwapo maneno ya kupotosha kutoka kwa wanasiasa kuhusiana na gawio la Sh bilioni 700 lililotolewa hivi karibuni kwa Serikali na mashirika hayo kuwa sio sahihi jambo ambalo ni uongo.
 
Afu hizo Bombardier zinazokuja hazina mapanga sijui watasemaje hawa watu
Bado watabeza na kupayuka kwamba mibombadia mibaya haina hata mapanga...
Hali ni mbaya mnooooo kwa wapinga maendeleo na vibaraka hapa nchini.
#NogeshaJPM
 
Ni jambo zuri , ila ingependeza kama tungeanza kuziita Majina ya Vivutio, Mbuga au Hifadhi za Taifa letu Mfano ( Serengeti, Selous, Manyara, Katavi ) Nationa Park, Air Tanzania; Ngongoro Crater , Air Tanzania au Gombe National Game Reserve , Air Tanzania.
 
Mwanza Bukoba 300,000/- afu bado tunakenua eti ndege za wanyonge....
 
Back
Top Bottom