Tanzania kuna serikali tatu?

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Ninajua kuwa mnajua kuna serikali ya muungano na ile ya zanzibar. Lakini wabunge wetu bungeni kila wanapotoa mada utawasikia wanasema, na ninawanukuu...
  • huu ni umahiri wa serikali ya CCM
  • napenda kuipongeza serikali ya CCM
  • serikali ya CCm inajali matatizo ya wananchi wake
  • nk
mwisho wa kunukuu.

Hitimisho: kuna serikali ya muungano, serikali ya znz na serikali ya CCM, maana hata spika hajawi kumhoji mbunge hiyo serikali ya CCm iko wapi?

Wakuu naomba kuwakilisha
 
Yep, jibu liko wazi kuwa tunaserikali mbili tu. Zanzibar ni serikali inayoongozwa na CCM kwa kuwa na nyumba ndogo isiyo na maamuzi (CUF) wala ilani ya uchaguzi inayotekeleza. Hawajakosea !!! Ndugu yangu Zanzibar wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM
 
Kwa nini basi mbunge anaposimama bungeni Dodoma anasema naipongeza serikali ya CCM? Kwa nini asiseme kuwa anaipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwani kila mara tunahitaji kukumbushwa rais katoka chama gani? Unafiki huu utakwisha lini.....
 
Back
Top Bottom