Tanzania kuizidi S.Africa kiuchumi?

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,672
68,631
Wadau jana nilimsikia kiongozi wa serikali(sijamkariri jina) alisema kwamba tanzania imekua kiuchumi kwa 7% na kuizidi south Africa ambayo ina 6.3%,Je wanauchumi hii kitu ni kweli au changa la macho?

Nawasilisha.
 
Inawezeka umekuwa kwa asilimia kubwa kupita wao katika hicho kipindi lakini kuwapita kiuchumi ni ngumu kutoka na ukubwa wa GDP yao.

Kwa mfano, USA uchumi wao 2011 ulikuwa kwa asilimia 1.5 lakini kusema kwa sababu wa kwetu ulikuwa kwa asilimia 7 tunaweza kuwapita kiuchumi itakuwa ni ndoto ya mchana
 
Hata Greece uchumi wao ukiendelea kuwa kwenye matatizo kama ulivyo sasa hivi itatuchukuwa zaidi ya miaka kumi na tano kuwapita kiuchumi
 
Si ajabu sana kwa nchi ambayo haijaendelea sana kiuchumi kukuza uchumi wake kwa asilimia kubwa kuliko nchi iliyoendelea. Kumbuka kinachopimwa hapa ni kiwango cha uchumi kukua, si ukubwa wa uchumi.

Ghana wameanza kuchimba mafuta na ni moja kati ya chumi zinazokua haraka sana sasa hivi, wanafikisha mpaka 15% kwa mwaka.

Marekani wana uchumi ulioendelea sana lakini kukuza uchumi 3% kwa mwaka hawawezi, kwa sababu uchumi wao ushakua tayari.

Hili halimaanishi Ghana ina uchumi mkubwa kuliko Marekani, kinachoongelewa hapa ni rate ya kukua kwa uchumi.

Having said all that, all data coming from the Tanzanian government is suspect.
 
Wadau jana nilimsikia kiongozi wa serikali(sijamkariri jina) alisema kwamba tanzania imekua kiuchumi kwa 7% na kuizidi south Africa ambayo ina 6.3%,Je wanauchumi hii kitu ni kweli au changa la macho?

Nawasilisha.


Ni kweli, GDP gowth rate kwa Tanzania inazidi S.A lakini anachosahua huyo waziri ni ukubwa wa GDP. Ni hivi
7% ya 50 ni kubwa kuliko 6.3% ya 500?
Alichotakiwa kusema ni kwamba uchumi wetu umeanza kukuwa lakini sio uchumi mpana.
 
Ni kweli, GDP gowth rate kwa Tanzania inazidi S.A lakini anachosahua huyo waziri ni ukubwa wa GDP. Ni hivi
7% ya 50 ni kubwa kuliko 6.3% ya 500?
Alichotakiwa kusema ni kwamba uchumi wetu umeanza kukuwa lakini sio uchumi mpana.

dadavua vizuri mkuu, nani ana 50 na nani ana 500. toa somo kidogo mkuu. GDP inakokotolewaje? naomba uniingize darasa mkuu.
 
Si ajabu mtoto mdogo kukua kwa haraka kuliko mtu mzima.Mathalani, mtoto wa mwaka mmoja, akiishi kufikisha mwaka wa pili, katika huo mwaka aliofikisha mwaka wa pili atakuwa kakua kwa 50% ya umri wake .

Mtu mwenye miaka 100 katika muda huo huo atakuwa amekua kwa 1% ya umri wake wa awali.

Hii haina maana kwamba huyu mtoto mdogo mwenye miaka miwili ni mkubwa kuliko mzee wa miaka 101. Ila rate ya kukua ya mtoto ni kubwa kwa sababu tunaipata kwa kutumia umri wake mdogo. Vivyo hivyo rate ya mzee kukua ni ndogo kwa sababu tunaipata kwa kutumia umri wake mkubwa.

Vivyo hivyo kwa chumi.

Chumi kubwa zinatakiwa kufanya kazi kubwa sana kukua kwa 1% tu, ndiyo maana Mmarekani akifikisha growth ya 4% ni sherehe.

Chumi ndogo ni rahisi kufikisha hiyo 4-5% growth, ndiyo maana unaona huko Ghana watu wanapiga mpaka 15%
 
Usiamini moja kwa moja matamshi ya viongozi wetu. Kuwa na wasiwasi na kila kinachosemwa na shukuru Mungu ikitokea kuwa kweli. Madaraka matamu.
 
Ukitaka kujua ukweli na uongo wa huyo Waziri linganisha hivi:

Bajeti ya Tanzania kwa mwaka ni TShs. Trillion 13.
Bajeti ya Afrika kusini kwa mwaka ni sawa na TShs Trillion 200.
 
Back
Top Bottom