Tanzania inaguswa kwa namna ya pekee na historia ya Afrika Kusini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab pamoja na ujumbe wa Tanzania wamekutana na timu ya Afrika Kusini wamejadili juu ya namna bora ya kutunza Urithi wa Ukombozi wa Afrika Kusini yakiwemo makaburi yaliyopo Tanzania.

Makaburi hayo ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini yapo katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Kongwa mkoani Dodoma, Mazimbu na Dakawa mkoani Morogoro pamoja na Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Mei 26, 2023 Cape Town Afrika Kusini, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Tanzania inaguswa kwa namna ya pekee na suala ya historia ya Afrika Kusini kwa kipindi chote tangu wakati wa harakati za ukombozi hadi sasa ndiyo maana Tanzania inaendelea kuyatunza makaburi ya wapigania uhuru hao.

Amepongeza Afrika Kusini kwa jinsi ambavyo wanatunza historia yao katika maeneo mbalimbali nchini humo ikiwemo makumbusho ya Uhuru Park ambapo majina ya wapigania uhuru yameandikwa kwa kumbukumbu za kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Bw. Yakubu ameongeza katika ziara hiyo ya kikazi, Tanzania imekabidhi majina 93 ya Watanzania ambao walitoa mchango wao katika ukombozi wa Afrika Kusini na kufikisha jumla ya majina 95 yakijumuishwa na jina la Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo tayari lipo kwenye orodha ya nchi hiyo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya South African Heritage Resource Agency Wakili Lungisa Malgas amesema taasisi hiyo inasimamia masuala ya urithi wa utamaduni yakiwemo makaburi ya wapigania uhuru wa nchi hiyo na wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuyahifadhi, kuyalinda na kuyatunza makaburi hayo ambayo yanahistoria muhimu kwa nchi zote mbili.View attachment 2636011View attachment 2636012View attachment 2636015View attachment 2636014View attachment 2636013View attachment 2636016View attachment 2636017
IMG-20230526-WA0069.jpg
 
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab pamoja na ujumbe wa Tanzania wamekutana na timu ya Afrika Kusini wamejadili juu ya namna bora ya kutunza Urithi wa Ukombozi wa Afrika Kusini yakiwemo makaburi yaliyopo Tanzania.

Makaburi hayo ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini yapo katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Kongwa mkoani Dodoma, Mazimbu na Dakawa mkoani Morogoro pamoja na Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Mei 26, 2023 Cape Town Afrika Kusini, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema Tanzania inaguswa kwa namna ya pekee na suala ya historia ya Afrika Kusini kwa kipindi chote tangu wakati wa harakati za ukombozi hadi sasa ndiyo maana Tanzania inaendelea kuyatunza makaburi ya wapigania uhuru hao.

Amepongeza Afrika Kusini kwa jinsi ambavyo wanatunza historia yao katika maeneo mbalimbali nchini humo ikiwemo makumbusho ya Uhuru Park ambapo majina ya wapigania uhuru yameandikwa kwa kumbukumbu za kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Bw. Yakubu ameongeza katika ziara hiyo ya kikazi, Tanzania imekabidhi majina 93 ya Watanzania ambao walitoa mchango wao katika ukombozi wa Afrika Kusini na kufikisha jumla ya majina 95 yakijumuishwa na jina la Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo tayari lipo kwenye orodha ya nchi hiyo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya South African Heritage Resource Agency Wakili Lungisa Malgas amesema taasisi hiyo inasimamia masuala ya urithi wa utamaduni yakiwemo makaburi ya wapigania uhuru wa nchi hiyo na wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuyahifadhi, kuyalinda na kuyatunza makaburi hayo ambayo yanahistoria muhimu kwa nchi zote mbili.View attachment 2636011View attachment 2636012View attachment 2636015View attachment 2636014View attachment 2636013View attachment 2636016View attachment 2636017View attachment 2636018
Okay
 
Safi
 
Back
Top Bottom