Tanzania ina ubavu wa kudhibiti kuyumba kwa uchumi?

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Chini ya serikali ambayo awali ilitupa matumaini kuwa hakutakuwa na athari za mparaganyiko wa uchumi uliotokea katika nchi tajiri, lakini baadaye ikaja na maelezo kuwa tatizo hili ni tishio, Je tunaweza kusema kwa uhakika kuwa hawa mabwana wapo makini katika kukabiliana na tatizo hili?

Hivi tutaendelea kumuachia mungu kwa matatizo kama haya hadi lini, itajafikia mungu atatuchoka kwa maombi yetu.

Hata hivyo mwenye dondoo juu ya hatua ambazo serkali inachukua kukabiliana na tishio hili naomba azinmwage hapa.

Tunatajiwa na wachumi kuwa athari ni pamoja na kushuka kwa mapato sekta ya utalii kwa asilimia 30, kahawa kwa asilimia 34 na Pamba kwa asilimi 54 ama hasara ya bilioni 41. Je katika sekta nyingine hali ikoje.

lakini napata shida kuona mbele kama tutasalimika na tuelewe kuwa tatizo hili lilichangia pia kuwepo kwa vita vya kwanza na pili vya dunia.
 
Awamu ya pili inaelekea kwisha, hasara tuipatayo kwa mfumko wa bei pekee, inaongeza mzigo mzito kwa mkulima
 
Back
Top Bottom