Tanzania imezizima, dunia imetaharuki kwa kuwa Magufuli alifanya yale wanadamu waliyotarajia kama kiongozi. Je, yupo atakayeweza kuvaa viatu vyake?

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,906
20,784
Magufuli alionyesha utofauti kama kiongozi tangu mwanzo wa safari yake ya uongozi na siasa.Katika ngazi zote za utendaji na kama Waziri,alitimiza wajibu wake katika kila eneo.Akawa kivutio kikubwa kwa wananchi na hata adui zake ndani na nje ya nchi.

Kwa siri adui zake walikiri umahiri wake katika utendaji,ingawa hadharani,walionyesha chuki dhidi yake.Magufuli hakuwa fisadi.Hata hivyo adui zake walijaribu kila walipoweza kumpaka matope,ili aonekane kwamba naye ni fisadi na ana tabia za hovyo kama wao.Ila ukweli utabaki kuwa Magufuli hakuwa fisadi,kinyume chake alichukia ufisadi wa aina yeyote.

Chuki dhidi ya Magufuli zilionekana hata ndani ya chama chake.Yeye kwa sababu ya utendaji wake uliotukuka, alikuwa hukumu tosha kwa viongozi wengine wababaishaji.Sitaficha ukweli kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2015,CCM ilikuwa njia panda,CCM ilikuwa inakaribia kuaga duru za kiasa za Tanzania.Kama chama, CCM ilijisahau,ikaweka maslahi ya wananchi pembeni na kukumbatia mafisadi wa aina zote na mabeberu.Mtizamo huu wa CCM ulifika kilele chake kwa kupitishwa Azimio Zanzibar, Azimio ambalo lilikumbatia ubepari na mafisadi moja kwa moja.

Hali ya wananchi kiuchumi iliendelea kuzorota,huku mafisadi na mabeberu wakiendelea kuneemeka.Tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho ikazidi kuongezeka,na vilio vya maskini vikasikika kila kona ya Tanzania.Ikawa dhahiri kwamba madiliko yalihitajika,tena kwa haraka,ili kubadili hali hiyo.Hata hivyo wanyonge hawakuwa na mtetezi na hali yao ikazidi kuwa mbaya.Uonevu wa kila aina ulionekana kila mahali,haki zikapotea.Mahakama badala ya kutoa haki kwa wananchi kikawa chombo cha kulinda mafisadi na na mabeberu,huku chombo hicho kikinyang'anya haki za wananchi.Jeshi la Polisi nalo likasimamia dhuluma,badala ya kusimamia haki na kulinda wananchi na mali zao.Badala yake wakalinda maovu kama uuzaji wa madawa ya kulevya na wizi.Polisi wakaogopwa badala ya kuwa kimbilio la wanyonge.Magereza yakajaa vibaka,na waliopaswa kuwepo magerezani wakawa mtaani wakistarehe, huku wakikebehi wananchi.

Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa uchaguzi Tanzania.Lakini kwa jinsi hali ya nchi ilivyokuwa,hapakuwa na shaka yeyote kwamba CCM ingepoteza uchaguzi ule na upinzani,specifically CHADEMA wangeingia Ikulu

Nilishasema hapo awali kwamba Magufuli alikuwa hukumu kwa viongozi wenzie kwa sababu ya umahiri wake katika utendaji.Niseme hapa pia kwamba wananchi walimkubali sana Magufuli,kwa sababu ya uaminifu wake na utendaji wake.Kwa bahati mbaya ndani ya CCM hapakuwa na kiongozi aliyekuwa na sifa zinazokubalika na wananchi,isipokuwa Magufuli,ingawa alikuwa hakubaliki sana ndani ya chama chake.Hii ikakilazimu chama kumchagua kupereusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa 2015.

Ni historia, sasa kwamba Magufuli alishinda katika uchaguzi ule.Baada ya ushindi wa kishindo na kusimikwa kuwa Rais,Magufuli alianza safari ya kuitengeza Tanzania mpya,safari ambayo sina shaka yeyote kwamba imemgharimu maisha yake.

Katika kuitengeneza Tanzania mpya,Magufuli alisimamia sera ya CCM kikamilifu,akaanzisha miradi mingi ambayo iliifanya Tanzania ipae kuichumi mara moja.Hii iliwezekana kwa kuwa kwanza yeye mwenyewe alikuwa mtendaji makini na mwaminifu.Hii ilimuwezesha kuunda serikali yenye watendaji waaminifu,makini na wenye weledi.Kwa hiyo kama nchi tukaweza kuongeza mapato kutoka Sh. Bil.800( tril.0.8) mpaka Tri.1.3! Fedha hii ikawa chachu ya maendeleo makubwa Tanzania kwa muda mfupi.

Niwakumbushe wasomaji wangu kwamba Magufuli ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza kuwa na ujasiri wa kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania ni tajiri.Wengine wote walijitahidi kuwa-aminisha Watanzania kwamba Tanzania ni nchi maskini.Hatua hii ilionyesha wazi kwamba Magufuli hakuwa na la kuficha na kwa hiyo alikuwa Rais na kiongozi mwaminifu.

Tabia yake ya uaminifu na kuwa a "no nonsense President," iliwafanya watendaji wote chini yake nao kutenda kwa umakini na uaminifu mkubwa.Matokeo yake Tanzania ikapata maendeleo kwa muda mfupi,na akawa mfano wa kuigwa ndani na nje ya Tanzania.Magufuli akapata sifa kwa wananchi aliowaongoza,wakampenda na akapata sifa duniani kote.

Magufuli hayupo nasi tena,tunae Mama Samia Suluhu.Najua kwamba Magufuli sio Mama Samia,ila kama wananchi wa Tanzania,tunategemea utendaji uliotukuka kutoka kwake na hata zaidi.Tunajua the road ahead is bumpy and rough,kwa kuwa mazingira aliyokuwa nayo Hayati Rais Magufuli hayajabadilika na ina wezekana yakawa magumu zaidi.Hata hivyo tunategemea utumishi uliotukuka.
Ni lazima mmoja wetu afe kwa niaba ya wengi.Magufuli umekufa kwa niaba yetu,nenda kwa amani na kwa heri hero na jabali,kipenzi cha Watanzania na sisi tuko njiani.Karibu Mama Samia Suluhu.
 
Kuwa kiongozi na hata kuwa Raisi ni wengi Sana wanaoweza hayo

Shida kuwa kiongozi na Raisi mwenye kutoa maisha yake kupambana na wapenda Dunia, wapenda unyanganyi, mijitu iliyotayari kutoa maisha ya mtu anayekwamisha biashara haramu za madawa ya kulevya na kuyabana kwenye mikataba ya uwizi eti yakuangalue Tu,,, watu wa Aina hiyo ni wachache Sana Katika hii dunia
 
Maisha hayapo hivyo

Mungu ana vipawa vingi....
Hii ni wishful thinking mkuu.Maeneo mengi Marais makini waliondoshwa wakaja viongozi bora liende.Mifano ipo mingi.Kwa mfano, DRC Congo,the former Zaire,walimuua Patrice Lumumba, akaja Dictator Mobutu Sese Seko.It was a disaster for the DRC.

Shida sio kuwa kiongozi,shida ni kuwa kiongozi makini aliyejitoa kuwa mtetezi wa wananchi wa ngazi zote.Tuendelee kumuomba Mungu sana.

Dhana kwamba muda wake umeisha siikubali mkuu,Tanzania needed him.
 
Hii ni wishful thinking mkuu.Maeneo mengi Marais makini waliondoshwa wakaja viongozi bora liende.Mifano ipo mingi,sina haja ya kuitaja.Tuendelee kumuomba Mungu sana.Dhana kwamba muda wake umeisha siikubali,Tanzania needed him.

Ukijikita kwenye propaganda unageuka kuwa mjinga kwa watu wenye uelewa. Wakati wa Nyerere tuliambiwa hatuwezi kupata rais kama Nyerere, leo hii mnatuambia hatuwezi kupata rais kama Magufuli! Hivi mbona mnatuchanganya, au nyie ndio mmechanganyikiwa?
 
Kuzizima wapi na watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Nyongeza ya hiyo kila zama na kitabu chake, tuwape muda wanaochukua hicho kijiti.
 
Tofauti ya Jiwe na Marais waliomtangulia Ni:-
Kupeleka maendeleo kwa upendeleo nyumbani kwao,hata Kama hakukuwa na umuhimu wowote kwa Taifa
butiama x
Uzaramoni x
Lupaso x
Msoga x
CHATO ✓

Kodi za taifa zilitumika kujenga miundombinu toka Zama za
Mwalimu,
Mwinyi,
Mkapa,
kikwete,
Magufuli,
lakini yeye ndio anapewa sifa zaidi ya waliomtangulia.

Wafanyakazi hawajaongezwa mishahara tangu bwana huyu aingie madarakani,hi haijwahi fanywa na Maraisi waliomtangulia,nadhani inaweza kuwa rekodi ya dunia.

Wakulima,wamekiona Cha moto.
wakulima wa korosho wanaweza kuwa mashahidi.

wafanyabiashara wamefilisika,wamehamisha biashara zao,wamefunga na wengine kufa.

Wanafunzi wa elimu ya juu wamekiona Cha moto kuhusu Loan Board,waliomaliza vyuo wamekatwa mikopo zaidi ya makubaliano, walioomba mikopo wamebaguliwa tofauti na awali,

Waliobomolewa nyumba bila malipo,

Wapinzani waliteswa,kufukuzwa bungenj,kutekwa kupigwa risasi na kukimbilia uhamishoni,

Mambo ni mengi mda ni mchache.
 
Miaka mitatu iliyopita nilikutana na mzee mmoja, tukaketi chini akanipa soga.../

Alisema wangapi walikuwepo namba moja, leo wamebaki chini ni vioja... watu wamewasahau
 
Wanachofanya CCM na viongozi wa serikali ni kumweka Rais mpya,mh mama Samia Suluhu(double S) awategemee CCM hii na viongozi wa serikali waliopo.

Hii hali imetengenezwa kimkakati,hadi vifo kadhaa huko Dar.. Madam S.S anajitambua,bila kuwafumua hao waimba pambio(praise team) (baada ya kukabidhiwa mikoba ya CCM), hawezi kufanya yake.
 
JPM enzi zake zimekwisha. Tunamwangalia Rais mpya,Madam SS,atuongoze,akiendeleza yaliyo mema.. Katiba ni ya CCM,2020_2025, hakuna kampeni mpya..

Mama SS na Majaliwa(PM) walizunguka nchi nzima kuinadi.. Watembee hapo hapo... Ombi langu wateue team mpya...wengi wao walikuwa wanamwabudu JPM,sio kumheshimu.
 
JPM enzi zake zimekwisha. Tunamwangalia Rais mpya,Madam SS,atuongoze,akiendeleza yaliyo mema.. Katiba ni ya CCM,2020_2025, hakuna kampeni mpya...
Nadhani walikuwa wanamwogopa mkuu, sio kumwabudu.Anyway kama kiongozi unahitaji kuogopwa na kuheshimiwa.

Hata hivyo binafsi sioni haja ya ku-overhaul the whole cabinet.Kama kuna ambao sio wazuri kiutendaji na weledi awaondoe,ila kulifuta baraza zima for the sake of it,sioni kwamba ni busara.
 
Back
Top Bottom