Tanzania idadi ya watu imeongezeka lakini hali sio nzuri mkoa wa Kilimanjaro

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,601
10,099
Ukienda mkoa wa Kilimanjaro utashangaa mambo yafuatayo haya matatizo hayako tu uchagani bali hata upareni yapo

Idadi ndogo ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza, huku mikoa mingine wanafunzi wakiwa wengi na wengine wanakaa chini Hali ni tofauti mkoa wa Kilimanjaro idadi ya wanafunzi inazidi kushuka kila miaka inavyozidi kwenda Kuna shule inaandikisha darasa la kwanza wanafunzi 10, Kuna nyingine iliandikisha wa-nne sio tu vijijini hata mjini Kuna shule moja ipo manispaa ya Moshi mwalimu aliniambia wanastruggle sana kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza

Nyumba nyingi kuwa empty hili ni tatizo lingine kubwa Kuna idadi kubwa sana ya nyumba hazina watu na ukienda vijijini Hali ndo mbaya Zaid nyumba nzuri nyingine gorofa Ila hazina watu na Hali inakua mbaya pale bibi na babu wakifariki sanasana utamkuta kijana mmoja tu ambaye Yuko kwa ajili ya kuziangalia, vijana kutoka Tanga hasa wasambaa, kutoka singida na manyara wambulu ndo utawakuta wanaangalia zile nyumba nyingi na kulimia migomba

Mfano ukienda upareni ni kawaida sana kuona nyumba imeachwa na kugeuka kuwa kichaka huku manyasi yakiwa yameota ndani huku nyumba ikiwa imebomoka bomoka

Vijiji mkoa wa Kilimanjaro havina watu kama umepanga kwenda kukaa week kwa Ile Hali ya vile vijiji vyao utajikuta umehairisha hakuna watu kabisa yaani in-short mkoa wa Kilimanjaro una ukiwa sio sawa na kipindi tunakua

Changamoto nyingine hakuna vijana Kuna kijiji nilienda kijiji kizima kijana ni mmoja ambaye ni bodaboda wengine waliobaki ni watu wa miaka 40 na kuendelea ni nadra sana kumuona kijana wa miaka 20's
 
Ukienda mkoa wa Kilimanjaro utashangaa mambo yafuatayo

Idadi ndogo ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza, huku mikoa mingine wanafunzi wakiwa wengi na wengine wanakaa chini Hali ni tofauti mkoa wa Kilimanjaro idadi ya wanafunzi inazidi kushuka kila miaka inavyozidi kwenda Kuna shule inaandikisha darasa la kwanza wanafunzi 10, Kuna nyingine iliandikisha wa-nne

Nyumba nyingi kuwa empty hili ni tatizo lingine kubwa Kuna idadi kubwa sana ya nyumba hazina watu na ukienda vijijini Hali ndo mbaya Zaid nyumba nzuri nyingine gorofa Ila hazina watu sanasana utamkuta kijana mmoja tu ambaye Yuko kwa ajili ya kuziangalia

Vijiji mkoa wa Kilimanjaro havina watu kama umepanga kwenda kukaa week kwa Ile Hali ya vile vijiji vyao utajikuta umehairisha hakuna watu kabisa yaani in-short mkoa wa Kilimanjaro una ukiwa sio sawa na kipindi tunakua
Kitu simple tu wachaga ni watu wanaotafuta maisha kila kona ya dunia, si bora hiyo umekuta kuna kijana anaangalia nyumba, nyingine zinafugiwa mbuzi na nyumba za maana, kijana akifikisha miaka 15 aNasepa
 
Kuna mengi broo yanasababisha,
Mosi kutokana kafara wenyewe Kwa wenyewe,pombe za kienyeji,wanawake. Wengi wa kichaga hawazai kabisa,wanaume wa kichana hasa vijana nguvu za kiume zinayeyuka sana, mirungi alikisussu yaani
Sio tu uchagani hadi uko upareni Hali inatisha
 
Sensa imetuonesha kwamba wachaga wengi na wapare wanaishi nje ya mkoa wa Kilimanjaro.

Siwez kusema kama ni jambo zuri au baya.
 
Hayo maswali yako ni rahisi sana kuyajibu, Jamii ya wachagga ni jamii inayo jishughulisha sana kwenye masuala ya maendeleo hususani biashara n.k

Cha msingi kuwa na maisha bora kuweza kumudu kusaidia familia kuwa katika hali nzuri n.k sasa basi kutokana na hali hiyo mchagga lazima atoke kwao ili atoboe ni lazima akajichanganye popote panapo wezekana ili apate chochote kitu.

Hili ni jambo la kawaida sana kwa jamii hii tofauti sana na jamii zingine hapa nchini ambazo huwa hawa sanuki mapema kuanza harakati za kimaendeleo ikiwemo ku make mkwanja ndio maana kwa asilimia kubwa sana nchi hii wachaga wana miliki pesa ndefu sana ukilinganisha na jamii zingine.

Lakini pamoja na hayo yote jamii zingine hapa nchini kwa sasa zimeamka sii haba wana jichanganya na kufanya harakati zao za kusaka noti sehemu mbali mbali nchini na kwingineko duniani.
 
Back
Top Bottom