Tanzania denies President bribe claims in U.S cable

This is why I like Wikileaks, vitu vinakuja moja kwa moja kutoka jikoni na moto wake.

Salva ananikumbusha mbunge mmoja wa viti maalum aliyedai Wikileaks wanataka kumchonganisha JK na Hoseah. Anadhani Wikileaks ni kama gazeti lao la Jamba Leo.
 
Lazima tukubali kuwa kuna haki ya "utuhumiwa" na mtu hawezi kutiwa hatiani kwa tuhuma. Tatizo ni kuwa kwa Tanzania hakuna "haki ya kumchunguza Rais" tena sikwambii kushtakiwa. Hii ndiyo demokrasia yetu. lakini mahali ambako marais/mawaziri/viongozi wa juu wa serikali hawako juu ya sheria, huwa wanachunguzwa na kushtakiwa.

Mfano ni mawaziri wakuu waIsrael ambao walikumbwa na tuhuma za "kupokea zawadi na kitu kidogo" na kushtakiwa. Mfano mwengine wa karibuni ambako kesi kama hiyo ya kununuliwa suti, ni ile iliyomkuta Rais wa Valencian Autonomus Government, ambapo hatimaye ilimbidi kujiuzulu na kezi iko mahakamani. Bofya hapa: Valencian premier to stand trial for accepting suits as gifts · ELPAÍS.com in English

Kwa hiyo, hata kama WikiLeaks watakuwa kweli, lakini kwa kuwa tuna "Idara ya Ukanushi" na kila isemacho ni kweli, tusitarajie kuwa hilo litafichuka zaidi ya hapo lilipofika.

Masikini (Wa)Tanzania!
 
Nakubaliana na Salva ni habari za kudharirisha sana hizi. Lakini Salva, nadhani ungekaa kimya kabisa na kuzipuuza hizi habari,ungekuwa umefanya jambo la maana sana, lakini kwa kuzijibu , naona ndio umelikoroga zaidi.

Haya mambo ya WeakLeaks yapo Duniani kote, na yanawezwa kuwekwa mambo mengine hapa tukabaki midomo wazi. Nilihisi kuwa lazima watu wa magogoni wangelisemea hili kutokana na historia yao ya kujibu mambo mbalimbali, na kweli sikukosea.

Nadhani, tunahitaji kusikia mambo au habari nzito toka pale magogoni na wala si haya mambo ya suti. Usije jikuta kesho yakaja mengine ya vijiko na sahani na hayo tena mkaanza kuyajibu, sasa hizo zitakuwa habari au nini?
 
Hata mwizi akikamatwa huwa hakubali hata siku moja, wakati kaingiza mkono mfukoni mwako. No one has confidence to say yes, i did.
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu amekanusha vikali taarifa za Mtandao wa Wikileaks zinazodai kuwa Rais wa JMT Mh. Kikwete alinunuliwa suti tano huko London na aliyekuwa mmiliki wa hotel ya Kilimanjaro Kempinski.

Bw. Rweyemamu amedai taarifa hizo za Wikileaks ni za uongo na upotoshaji mkubwa na zinazomdhalilisha Rais wa JMT na akasema mwenye ushahidi wa tuhuma hizo aupeleke Ikulu!


Source:Chanel ten

Kazi ni kwenu watz!

Hivi hawa watu wamechanganyikiwa nini?? Ikulu siku hizi imekuwa mahakama mpaka ipokee ushahidi. Kama ni uongo na raisi amedhalilishwa si waushtaki mtandao wa wikileaks??. Wasitake kukataa ukweli hapa, mwisho watasema wikileaks ni mtandao wa chadema!!! Make kila kitu kinachoeleza ukweli kuhusu SRKL basi wanasema ni CDM!! Siri zitaendelea kufichuka mpaka wananchi wote watakapo waelewa CCM ni watu wa namna gani!!!
 
[SIZE=-1]
UMAARUFU WA MAFUNDI CHEREHANI WA SAVILE ROW PAMOJA NA SUTI ZAO BEI MPAKA PAUNDI STERLING 10,000 , JIJINI LONDON

Handmade bespoke suit from Savile Row in London for the gentleman can be regarded as the equivalent to an haute couture outfit for the lady from Paris: it is simply the ultimate indulgence and style.

Over the past couple of years Savile Row is seeing an amazing revival. Celebrities such as Sean Connery, Brian Ferry, Michael Caine, Charlie Watts and Tom Cruise all have joined the client lists of some of the most exclusive tailors on Savile Row. Elegant-Lifestyle has therefore visited Savile Row for its readers and has compiled a comprehensive and informative list of the most established names for the famous bespoke Savile Row suit.

The personal tailoring of your bespoke suit will require about 3 fittings and take four to twelve weeks. Prices start at £1,500 to £3,000 for the more famous names and can go up £10,000 for very exclusive materials. The addition of a waistcoat, which elevates the two-piece suit to an elegant three-piece suit will add another £200 to £500. Although all of the addresses listed below do the classic bespoke Savile Row suit, which is handmade,

Source and more info: Elegant-Lifestyle.com: Clothing: Shirts & Suits: United Kingdom: Savile Row's Best Bespoke Suit Tailors

[/SIZE]
 
Anasema madai haya ni ya kipuuzi na ni kumtusi JK....wange-shtum tu na kuipotezea
 
Baada ya kusoma ile habari ya Ukerewe ndipo nilijua kwamba wikileaks haina tofauti sana na wikipedia - A free encyclopedia which anyone can write or edit anything! - Haya na hizo habari za JK kaoa Burundi sijui Rwanda mbona mke mwenyewe hatumjui?
Sina comment kuhusu wikileaks kwangu kukubaliana nao na kutokubaliana nao yote ni majibu sahihi, ila kutaka kujua mke wa jamaa wa Burundi, Rwanda au kokote kwingineko inabidi UAMKE.
 
Kaka mtu akikuchukia hakuchagulii tusi, sasa angalia kuna mdau mmoja hapo juu anaikubali tu hiyo weaklinks kwa kuwa wamarekani wameipigia kelele...!

Kwani vingapi wamarekani wamevitengeneza na wanajitia kuvipigia kelele kuhadaa watu.
huku ndio kuwaza kwa kutumia masaburi
 
Salva anajua na kuelewa kuwa katika suala la ufisadi ikulu ilikataa katakata na leo ajenda hiyo ipo na mwenyekiti wa chama ambaye ni Rais wa nchi na anakaa ikulu. Inawezekana baada ya miaka miwili ikulu itakubali mimi sijui ila nilionelea niweke sahihi yangu kuwa nimeona ila napita nakuwaachia CCM watueleze na kuifutia Tanzania aibu hiyo.
 
Sio kila kitu kilichoandikwa kwenye wikileaks ni sahihi.

Mkuu kama sio sahihi kwa nini nchi nyingine huwa hazikanushi yanayowekwa dhidi yao kule? Ina maana Wikileaks inaweka vya kweli nchi nyingine na vya uongo nchi yetu? Halafu madai yalikuwa sio tuu Rais Kikwete alinunuliwa suti tano huko London. Ina maana yale madai mengine ni ya kweli?
 
Sina comment kuhusu wikileaks kwangu kukubaliana nao na kutokubaliana nao yote ni majibu sahihi, ila kutaka kujua mke wa jamaa wa Burundi, Rwanda au kokote kwingineko inabidi UAMKE.
Haya nijuze wewe ulokwisha amka maanake hakuna sababu ya kuficha ukweli - huyu ni rais wetu na tuna kila haki ya kufahamu wake zake...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom