TANU: Ni Mzazi aliyepata mtoto ambaye YUKO tofauti sana na yeye kwa sasa

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
TAFAKURI.


TANU: Ni Mzazi aliyepata mtoto ambaye YUKO tofauti sana na yeye kwa sasa.


Kwa wazazi mnajua wote kuwa ukiwa na mtoto wako unategemea vitu fulani kutoka kwa huyo mtoto vinaweza kuendana na wewe au kushabihiana kwa mbali. TANU kama mzazi alipata mtoto akafurahi na kurukaruka sana na kufanya sherehe za kujipongeza kwa kitendo hicho maana ni cha amani na furaha. Baada ya kuzaliwa mtoto huyo ndugu,jamaa na marafiki walijitolea kwa moyo wa dhati kabisa kufanikisha sherehe ya mtoto huyo. Na bahati iliyopo mtoto huyo hata wana kijiji walileta kuni za kupikia ili sherehe ifaane.


Kwa nini walifanya hivyo kwa mtoto huyu?. Walifanya hivyo kwa sababu moja tu. TANU alikuwa anawajali akipambana na changamoto zao za maisha. Najua naye si Mungu alifanya makosa mengi lakini kitu walichokuwa wanakipenda kutoka kwake ni tabia yake iliyo ya wazi; kwa mfano kusimamia;


a) UTU
b) MAADILI MEMA
c) UTII KWA JAMII INAYOMZUNGUKA
d) UAMINIFU KWA WATU WALIO KARIBU YAKE
e) ALICHUKIA RUSHWA NA DHURUMA YA AINA YOYOTE.
f) ALIYAFANYA AMBAYO ALISEMA HAYAPENDI NA HAKUMUONEA HAYA MTU YOYOTE........na kadharika.


Hizi ni baadhi ya sababu za wananchi za kumpenda TANU si kumpenda tu bali na kumwamini pia. Alikuwa na madhaifu yake kama binadamu lakini watu walimpenda sana.


Kwa wale wasiomjua vizuri TANU alizaliwa mnamo 7/7/1954 katika mtaa wa LUMUMBA Dar es Salaam. Alizaliwa katika mazingira magumu sana na ya hatari sana. Mashuhuda wanasema kuwa alizaliwa kwenye masanduku tu yale ya kusafirishia mizigo. Mashuhuda wakubwa walikuwa ni Mwl. Nyerere,Ally Sykes, Abdual Sykes na Doss Azizi. Kuna mtu mmoja maarufu sana naye ni Rashid Kawawa alitaka kuja kushuhudia kuzaliwa kwa mtoto huyu, alizuiwa na serikali ya kijiji wakati ule kwa sababu tu ni mfanyakazi wa serikali kwa hiyo hakufanikiwa kabisa na aliumia sana. Kwani Rais ambaye aliingia kwa Mabavu Twinning bila hata ridhaa ya wananchi wa kijiji alimzuia kwa nguvu Rashid kwa zuio lake.


TANU alitokea kwenye ukoo wa T.A.A. Alipozaliwa tu akiwa mtoto akawa anaonyesha uwezo wa ajabu kabisa. Haikumchukua umri mrefu akaanza kumpinga Twinning na baadae Twinning akakikimbia kijiji. TANU alikuwa vizuri sana na aliwapenda watu wake vyema kwa moyo wake wote na alijitoa sana katika kijiji. Watu wengi walimwamini sana kwa ujasiri mkubwa aliokuwa nao. Kwa kifupi alitokea kuwa kiongozi akiwa mdogo sana katika kijiji alikozaliwa na kweli watu walimwamini sana.


Alipotimiza miaka kumi na kuendelea alionyesha uwezo ambao kwa binadamu lazima ushangae sana. Matajiri wote Duniani aliwaambia wasimchagulie marafiki, na alisema misaada yote inayozalilisha utu wa binadamu alikuwa hautaki kuusikia. Na alikosana na watu wengi sana Duniani hasa matajiri waliokuwa wanataka kukiangamiza kijiji chake pamoja na wananchi wake....kwa kweli TANU alikuwa shujaa sana pamoja na madhaifu yake aliyokuwa nayo.


Kwa mfano, baada ya kumfurumusha Twinning mnamo 1961, alikuwa na urafiki na watu kama Nkwame Nkrumah kutoka kule Ghana, Patrice Lumumba Kongo na Sekou Toure Guinea na wengine wenye misimamo isiyoyumba na wenye uzalendo mkubwa. Akawa kijana wa kuigwa na Mataifa mengi sana ya Afrika hasa vijana wenzake.


Mnamo mwaka 1977 Alikuwa tayari ameshakuwa, kwa hiyo TANU akapata mtoto anayeitwa CCM, malezi na maadili yote ya mtoto huyu CCM yaliyokana na Mzazi wake TANU. Kwa kweli alikuwa vizuri sana huku akiwa anafuata nyayo za Mzazi wake TANU. Alipigania utu wa mwanadamu na kusema kweli alionyesha njia kama mtoto baada ya kukua tu. Kijiji kilimwamini sana kwa sababu ya kufanana na Baba yake TANU. Ilikuwa IKITOKEA ukamsema vibaya wana kijiji wangekuchukia sana na wakati mwingine wangekuzomea sana na ungeona aibu tu kwa nini unamchukia huyu mtoto wa shujaa TANU?.


Kuna mda ukafika wana kijiji wakaanza kutomwelewa kabisa na wakaanza kumhoji. Lakini ilikuwa ukihoji kama wewe ni mwenyeji wa kijiji unahamishwa na sungusungu kwa nguvu ili ukaishi kijiji kingine. Wana kijiji wakashangilia kwa kitendo hiki wakidhani kuwa huyu mtoto wa TANU anafanya vizuri. Baada ya hapo mtoto huyu akawa anatamani utajiri wa wananchi wake uwe wake peke yake na viwanda vya wananchi ambavyo Mzazi wake TANU kwa kushirikiana na wananchi walivijenga, akaanza kuvichukua kwa nguvu na kuwapa marafiki zake wa nje, mbaya zaidi watoto wa yule Twinning!!!!!!!!!!!. Wana kijiji wakaduwaaa sana.


Mnamo 1995 watoto wa Twinning wakaja na ushauri mzuri na wakamshauri kuwa nafasi ya mwenyekiti wa kijiji lazima ipambanishwe. Baadhi ya watu walikuwa wameanza kumchoka wakaanza kuonyesha ishara hizo japo kwa UOGA sana. Lakini watu waliokuwa pamoja na TANU walianza kumuonya kuwa usipobadilika UKAWA kama Mzazi wako hali ya kijiji itakuwa mbaya sana.


Mnamo mwaka 1994, mtu ambaye tunaweza kusema ndiyo alimulea TANU na kukua alichoka sana kumshauri mtoto CCM na akamwandikia barua yenye aliyoiwekea kichwa cha habari UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA. Katika barua yake ambayo mtoto huyu CCM huwa hataki kujirudia kuisoma alimuasa mambo mengi sana ili aweze kuongoza kijiji alichomwachia ambacho ni Tanzania. Mwisho alimalizia na WOSIA mkubwa sana ambao ni;


WOSIA
Ole wake Tanzanai
Tusipoisadia!
Niwezalo nimefanya:
Kushauri na kuonya.


Nimeonya: Tahadhari!
Nimetoa ushauri:
Nimeshatoka kitini;
Zaidi nifanye nini.


Namlilia Jalia
Atumlikie njia;
Tanzania ailinde,
Waovu wasiivunde.


Nasi tumsaidie
Yote tusiyamwachie!
Amina,tena Amina!
Amina tena Amina!.


Naweza kusema dhahiri kuwa TANU ilipata mtoto CCM. Huyu mtoto aliaminiwa sana na wana kijiji. Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba wana kijiji wanaanza kuhoji tabia za huyu mtoto kwani zinatofautiana sana na Mzazi wake TANU. Wana tofautiana sana kitabia, ki mwenendo, ki maadili na kwa sasa wananchi wa kijiji hicho wanahoji sana mbona Mzazi alitoa mafunzo mema sana na huyu mtoto kwa sasa haambiliki?. Ebo mtoto anakaba? Leo hii wazee wakimuonya anawatukana matusi ya nguoni na kuwaambia wanamshauri hivyo kwa sababu ni wazee na watakufa wakati wowote!!!!.


Huyu mtoto anapenda rushwa,dhuruma, na wakati mwingine huyu mtoto haambiliki. Hawasikilizi walezi wake kabisa na wakati mwingine amepata marafiki hovyo sana nje na ndani maana wanamudanganya kuwa YUKO sawa. Anashauriwa vibaya hasa lile la kuwatukana hata wazee walioishi na baba yake TANU. Anafanya hivi huku akiwa anasaidiana na marafiki zake wa nje na ndani. Vikao vingi vinafanyika ili kumuonya lakini tatizo kwa sasa haambiliki. Wananchi wanamvumilia tu kama mabadiliko ya hali ya hewa.


Eti hawampendi kwa sasa mbona wanachagua au anasingiziwa tu? Eti imegikia wengine wanasema uchaguzi anashinda maana watu wamebadilika sana enzi zake; nao wanadhamini pesa kuliko utu, na yeye pesa si tatizo maana alishachukua shamba la jirani akaliuza kwa nguvu kwa wajukuu wa Twinning. Kama huamini kawaulize Wamakonde, Wasukuma, Wakurya pamoja na misimamo yao lakini kokoto zao wamezuiwa kuzitumia kujengea hata msingi wa nyumba. Mimi sitochimba sana kawaulize maana nitaambiwa mchochezi kama waliosema eti na sisi tunataka tufaifike na kokoto zetu....wakaambiwa ni marufuku na wakaletewa sungusungu wa kutosha....huyu ndiyo mtoto wa TANU.


Huyu mtoto mbona alilelewa vizuri....vipi usemi usemao MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO?. Mbona huyu alikuzwa na kulelewa vizuri mbona kabadilika sasa?. Mimi naona wananchi wamwambie wazi kuwa unakosea ili abadilike lasivyo ataona kuwa hakosei wala hawakosei wananchi anaowaongoza. Mimi naona wananchi wamwambie ukweli maana kumkosoa huyu kiongozi anahitaji ushauri wa hali ya juu japo HAAMBILIKI. Tunaweza kumshauri na akatusikiliza maana bado watu ambao wana uwezo wa kufanya hivyo wapo japo yeye hawataki kuwasikia au kwa sababu wao pia hawatofautiani na yeye wakimtaka abadilike au wako tofauti na yeye.


Lakini siku hizi ni mkali ukimshauri anaweza akakuporomoshea matusi kibao tu. Maana ukisema ukweli yeye ataona unampinga kwa hiyo unaweza usiwe salama kisa umetoa ushauri tu. Tafakari.
 
Back
Top Bottom