Tangu tufahamiane naye, nimekuwa naota ndoto za ajabu ajabu

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,483
40,501
Ijumaa ya juzi niliamua nitoke kidogo angalau nikapate mbili tatu za baridi.

Nikiwa maeneo ya kujivinjari, huku napambana na mitungi yangu, mara akatokea lishangazi la makamo. Akaomba tukae naye pale mezani, kwa sababu nilikuwa mwenyewe nikamkubalia.

Akaagiza raundi, tukawa tunaendelea kunywa; ile namtazama puani,nikamuona ameweka kipini; na mimi watu wanamna hiyo huwa nawaogopa sana, kwa sababu wanamna hiyo huwa ni makonkodi kwenye mahusiano.

Baada ya kulewa, lishangazi likaanza kufunguka, ''unajua nakupenda sana, sitaki uwe mbali na mimi, nataka angalau nizae na wewe, kwa sababu nina mtoto mmoja ana miaka sita, anatakiwa apate mdogo wake''

Nikafikiria, nikamwambia tutaongea muda utakaporuhusu, kwa sasa tunywe pombe tu. Tukawa tumekubaliana Jumatatu jioni ndio tukutane kwa mazungumzo.

Baada ya kulewa sana, kila mmoja akarudi alikotoka; sasa jana jioni kwenye mida saa mbili nikaamua nipumzike; kutokana na uchovu nikapitiwa na usingizi mkali, nikawa naota ninatembea sebuleni, ghafla nikakutana na mwanamke ambaye sijui ameingilia wapi, ile namshika mkono nikawa naogopa. Ikawa hiyo ndoto inajirudia rudia; kushtuka naangalia saa, ni saa tano usiku.

Ikabidi niamke nianze kulikemea hilo pepo; kufika saa tisa ikabidi nirudi tena kulala; mara nikaota ndoto ya namna ile ile, ila hii ya sasa, walikuwa wanawake wawili wamekuja kitandani kwa kunishtukiza, wanalazimisha kutaka mapenzi; ile wananilazimisha, nikawakimbia nikajikuta nimedondoka kwenye ngazi, ile napambana nifungue mlango, nikawa nawasikia wengine wako jikoni.

Nimekuja kushtuka mchana huu, nipo hapa napata kongoro huku nikitafakari hizi ndoto, na kwa nini zitokee nyakati hizi.

Nimeanza kwa kufuta namba ya yule binti nikihisi labda kuna koneksheni, au labda itakuwa ni magonjwa ya akili.

Karibu kwa mawazo.​
 
Ulilikemea kwa jina gani hilo pepo?🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom