Tangu lini mwanaume anazaa! Mwanaume hazai anazalisha

Mwanaume akipata mtoto usimwambie hongera kwa kuzaa, mwambie hongera kwa kuzalisha. Wanaume huwa hawazai wanazalisha, waalimu wa somo la Kiswahili mnatakiwa kulaumiwa Sana watu wengi hawaongei kiswahili fasaha.
Sawa,
Kwa hiyo wanaposema utaje jina la wazazi au mzazi wako wanakua wanamaanisha mama tu? Sababu Kwa maelezo yako Baba anakua sio mzazi wako sababu hawezi kukuzaa
 
Sawa,
Kwa hiyo wanaposema utaje jina la wazazi au mzazi wako wanakua wanamaanisha mama tu? Sababu Kwa maelezo yako Baba anakua sio mzazi wako sababu hawezi kukuzaa
Elewa Kiswahili boss . Kuna kuzaa na kuzalisha , mwanaume anazalisha a mwanamke anazaa
 
Kuzalisha - mkunga, muuguzi, daktari, au mtu yeyote anayeweza kumsaidia mjamzito ajifungue

Kuzalisha - mchakato wa shughuli kama vile viwandani. Mfano: Kuna tatizo kubwa la uzalishaji wa bidhaa nchini.

Kuzaa - kujifungua (mwanamke)

Kuzaa - sifa asilia ya kiumbe hai chochote (kuongeza aina-nafsi husika, bila kujali jinsi)

Kuzaa - kuongezeka idadi, kupata matunda au mafanikio (mali, fedha, viumbe, nk).

Kuzaa - mwanamke kuwa na uwezo na kupata mimba; mwanaume kuwa na uwezo kutungisha mimba

Kuzaa - kuibua, kuchochea, kuamsha, kusababisha (induce, bring about, derive (zaari)

Kuzaa - to bypass. ^Alizaa ushauri wa marafiki zake, akaamua kuchepuka na kuzaa na mpenzi wake (he bypassed his friends' advice, deciding instead to fall for and have a child with his lover.)
 
Karata yako undhani umeicheza vizuri? Maana mzazi ni mtu anayeweza kuzaa au hata kuzalisha. Kwa hiyo hujamkamata bado, japo hayuko sahihi.
Tukubaliane kwanza Mzalishaji ni Mkunga, Nesi au Daktari. Yule anaemsaidia mjamzito kuzaa. Hakika huyu sio Mzazi, so uko wrong
 
Kuzalisha - mkunga, muuguzi, daktari, au mtu yeyote anayeweza kumsaidia mjamzito ajifungue

Kuzalisha - mchakato wa shughuli kama vile viwandani. Mfano: Kuna tatizo kubwa la uzalishaji wa bidhaa nchini.

Kuzaa - kujifungua (mwanamke)

Kuzaa - sifa asilia ya kiumbe hai chochote (kuogeza aina-nafsi husika, bila kujali jinsi)

Kuzaa - kuongezeka idadi, kupata matunda au mafanikio (mali, fedha, viumbe, nk).

Kuzaa - mwanamke kuwa na uwezo na kupata mimba; mwanaume kuwa na uwezo kutungisha mimba

Kuzaa - kuibua, kuchochea, kuamsha, kusababisha (induce, bring about, derive (zaari)

Kuzaa - to bypass. ^Alizaa ushauri wa marafiki zake, akaamua kuchepuka na kuzaa na mpenzi wake.^
Ndg yang umefafanua vizuri sana , una karama ya ualimu , bahati mbaya sio kazi yako , ila ungekuwa mwalimu darasa zima lingefaulu mitihani ya NECTA
 
Back
Top Bottom