GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 5,306
- 7,211
Japo hazina uthibitisho wa kuaminika, lakini kutokana na hali ilivyo, unaweza ukashawishika kuziamini.
Maelezo ya mtu anayedai kuwa alikuwa Mwenyekiti wa wachawi wa Tanzania kabla ya kuachana nao mnamo mwaka 2000 ni kama ifuatavyo:
1. Tanzania inatawaliwa kwa msaada wa nguvu za kichawi. Kabla ya nchi kupata uhuru, kulifanyika tambiko Bagamoyo lililoikabithi nchi ya Tanganyika kwa Shetani. Kiongozi mkuu wa hilo tambiko alikuwa ni mchawi mashuhuri aliyeitwa Forojo Ganze
2. Mwenge uliasisiwa na tambiko la Bagamoyo. Lengo mojawapo la hilo tambiko ni kuifanya nchi kutawalika
3. Jina la Tanzania ni mpango wa Shetani. Jina ambalo lina baraka za Watanganyika ni Tanganyika, lakini Chama cha siri cha kichawi hawakuliridhia hilo jina kwa sababu lilikuwa likiwakwamishia mambo yao ya kuitawala Tanganyika
4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulilenga kupoteza jina la Tanganyika ili iwe rahisi kwa wachawi kuendesha utawala wa nchi bila bughudha
5. Mwanzoni, ililengwa kuunganishwa Tanganyika na Kenya na Uganda, lakini iliposhindikana, ndipo Zanzibar ilipogeukiwa
6. Katika shindano la kutafuta jina jipya la nchi mbili zilizoungana, walijitokeza watu zaidi ya 1,500, lakini walioshinda walikuwa watu 16. Wote waliibuka na jina la TANZANIA
6. Katika watu 16 waliolibuni jina la Tanzania, ni watu watatu au wanne hivi ndiyo waliofahamika. Hata hivyo, aliyekidhi vigezo vya kukabidhiwa zawadi ni mmoja tu, Ikbaru Mohammed Dar
7. Washiriki wengine ambao hawakufahamika, wanasadikiwa kuwa hawakuwa binadamu, bali majini
8. Maana halisi ya Tanzania kwa mujibu wa Ikbaru Mohammed Dar ni Tan = Tanganyika, Zan = Zanzibar, I = Ikbaru (jina la mtunzi), na A = Ahamadya (Jumuia yake katika dini ya Kiislamu)
9. Siku chache baada ya kupata huo ushindi, baba yake Ikbaru na familia nzima, Ikbaru akiwemo, waliondoka nchini na kuhamia Uingereza. Babaye alishauriwa kuondoka haraka sana nchini ikiwa hataki mabaya yaipate familia yake. Kitendo cha kijana wake kuweka herufi ya jina lake kwenye jina la nchi kiliwakasirisha majini. Ni kama vile aliingia kwenye vita na majini. Alijimilikisha nchi wakati majini yalikuwa yakiamini kuwa wao ndiyo wenye haki ya kuimiliki nchi
10. Chama cha kichawi kinaiendesha nchi kupitia ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wana "ofisi" yao kwenye ofisi ya Waziri Mkuu kama Wazee washauri, lakini ukweli ni kwamba wao ni wachawi wanaoitawala nchi kupitia chama chao cha kichawi.
11. Ajali iliyomuua Sokoine mwaka 1984 ilitengenezwa na Chama cha kichawi cha siri kinachoitawala Tanzania kwa sababu Sokoine alikuwa hakubaliani na mambo ya ramli, hivyo hakuwa akiwapa ushirikiano. Alikuwa akiamini katika majani ya miti shamba kama tiba lakini si katika majini na ramli.
12. Chama cha kichawi kinachoitawala Tanzania kwa siri kiliapa kuwa haitatokea kwa mtu aliyewahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika nafasi ya Urais wa Tanzania. Ni mpaka pale utawala wao wa kichawi utakapodhoofishwa au kupinduliwa ndipo mtu aliyewahi kushika huo wadhifa ataweza kuwa Rais. Ikitokea mtu atafanikiwa kushika huo wadhifa, itamaamisha kuwa ana nguvu kubwa za kiroho kukizidi hicho Chama cha kichawi, ama za Mungu au za giza.
Kwa hiyo hata kama Kasim Majaliwa na wengine waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu watatamani kuwa Rais wa Tanzania, hawataweza endapo huo utawala wa kichawi haujapinduliwa. Siyo kwamba hawana sifa, bali misimamo watawala wa gizani haiwakubali
13. Tambiko la kitaifa la 1990 lililofanyika mkoani Lindi, limekuwa na madhara kwa watu wa Lindi waliozaliwa baada ya tambiko hilo(baada ya 1990). Madhara ya hilo tambiko ni pamoja na udumavu wa kielimu na kimaendeleo kwa ujumla.
14. Neno Tanganyika lina asili ya kabila la Kichapu, na maana yake ni nchi yenye rutuba. Kama Tanganyika ingeachwa iendelee kulitumia jina lake la awali kungekuwa na maendeleo zaidi ya ilivyo sasa. Jina la Tanganyika ndilo limebeba baraka za Watanganyika.
Kama ndivyo, kuna haja ya kuendelea kulitumia jina la Tanzania ilhali lenye baraka ni la Tanganyika?
Kwa sehemu naweza kukubalianan na mzungumzaji kuwa huenda ni kweli Muungano ulilenga kulipoteza jina la Tanganyika. Kama sivyo, kwa nini jina la Tanganyika limefichwa wakati la nchi ya ya Zanzibar linaendelea kutumika?
Nimeambatamisha na clips chache.

Attachments
-
PART14_MWENYEKITI_WA_WACHAWI_TZ__SHEKHE_ALIEOKOKA_NILIUA_MKE_NA_KUISHI_NAE_TENA_UCHAWI__NIMESO...mp41.9 MB
-
PART14_MWENYEKITI_WA_WACHAWI_TZ__SHEKHE_ALIEOKOKA_NILIUA_MKE_NA_KUISHI_NAE_TENA_UCHAWI__NIMESO...mp41.6 MB
-
PART14_MWENYEKITI_WA_WACHAWI_TZ__SHEKHE_ALIEOKOKA_NILIUA_MKE_NA_KUISHI_NAE_TENA_UCHAWI__NIMESO...mp41.9 MB
-
PART15_MWENYEKITI_WA_WACHAWI_TZ__SHEKHE_ALIEOKOKA_NILIUA_MKE_NA_KUISHI_NAE_TENA_UCHAWI__NIMESO...mp42 MB