TANESCO yawasimamisha kazi Maofisa 7 kutokana na makosa mbalimbali, wizi na ubadhilifu

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Akizungumza leo Dec 6, 2015 mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema, Ukiacha kero zinazosababisha na Miundombinu TANESCO inachukua hatua madhubuti za kuwaadhibisha wafanyakazi wake wanaotoa huduma mbaya na kuwa kero kwa wateja baadhi ya kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa pamoja na lugha mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma kucheleweshewa huduma, ubadhirifu.

Shirika linapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa tayari limeanza kuchukua hatua kali kwa wafanyakazi wanaobainika kujihusisha na mambo hayo.

Katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa 7 waandamizi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera na kuripotiwa na vyombo vya habari jana.Walioachishwa kazi ni pamoja na wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, wahandisi na wahasibu.

Shirika litaimarisha hatua hizo ambapo mfanyakazi yeyote atakayebainika analaghai wateja, anadai rushwa anatoa lugha chafu au huduma mbovu atawajibishwa mara moja na pale atakapobainika kuachishwa kazi.

Tunataka kuona pia wakihukumiwaa kwa mujibu wa sheriaaa
 
Huyo mkurugenzi na timu yake walikua wapi mda wote hawakuchukua hatua? Kwanini nayeye asiwajibishwe kwa kuchelewa kuchukua hatua?
 
huyo mkurugenzi asijikombe ----- huyo yeye ndio anatakiwa afukuzwe na mashtaka juu aache uonevu kwa kuwatoa sadaka
 
Unawaachia ili wakale vizuri pesa walizo kwiba?
Wamesikia Magufuri karibu anawarukia wanaleta Futuhi!
 
Huyo mkurugenzi na timu yake walikua wapi mda wote hawakuchukua hatua? Kwanini nayeye asiwajibishwe kwa kuchelewa kuchukua hatua?

Mramba ataumiza wenzie bure, yeye mwenyewe kakalia kuti kavu. Angesubiri tu fagio la chuma lipite ambapo yeye pia hatapona
 
Akizungumza leo Dec 6, 2015 mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema, Ukiacha kero zinazosababisha na Miundombinu TANESCO inachukua hatua madhubuti za kuwaadhibisha wafanyakazi wake wanaotoa huduma mbaya na kuwa kero kwa wateja baadhi ya kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa pamoja na lugha mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma kucheleweshewa huduma, ubadhirifu.

Shirika linapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa tayari limeanza kuchukua hatua kali kwa wafanyakazi wanaobainika kujihusisha na mambo hayo.

Katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa 7 waandamizi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera na kuripotiwa na vyombo vya habari jana.Walioachishwa kazi ni pamoja na wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, wahandisi na wahasibu.

Shirika litaimarisha hatua hizo ambapo mfanyakazi yeyote atakayebainika analaghai wateja, anadai rushwa anatoa lugha chafu au huduma mbovu atawajibishwa mara moja na pale atakapobainika kuachishwa kazi.

Huyu Mramba atuambie , ni nani huwa anafungulia maji ya kwenye mabwawa na kuyamwaga huko ili kuwe na shida ya umeme na hivyo kujenga hoja ya hitaji la umeme wa dharula na kuimarisha biashara ya majenereta?
 
Jamaa kala dili na hao wafanyakazi ili apate gia ya kukwepa fagio la Magufuli kwa kutumia sanaa za maigizo
 
Magufuli anakuja ,Naona Mramba kaanza kujihami.Mungu mlinde Magufuli na mahasidi wote wasimuweze kwa husda zao
 
Huyu Mramba atuambie , ni nani huwa anafungulia maji ya kwenye mabwawa na kuyamwaga huko ili kuwe na shida ya umeme na hivyo kujenga hoja ya hitaji la umeme wa dharula na kuimarisha biashara ya majenereta?

Ukiona kimya ujue hakuna anaefungulia. Hata hivyo soma Mada uielewe
 
Back
Top Bottom