Ni miezi miwili sasa umeme umekuwa ukikatika kila wakati kwa maeneo na mikoa taofauti na mbaya zaidi nyakati za usiku sana unakuta umeme umekatika huku tukijua kuwa umeme nao ni sehemu ya ulinzi kwa baadhi ya mitaa kwa hapa Dar es salaam.

Na shirika hili la umeme limekuwa kimya kabisa hasa baada ya Prof Muhongo kuondolewa katika nafasi ya uwaziri wa Nishati na Madini kuhusu masula ya umeme kukatika katika na hata maendeleo ya kusambaza umeme kupitia upatikanaji wa gesi ya Mtwara.

Pamoja na kuwa na Gesi ya Mtwara ambayo tuliamini ndiyo mkombozi wa umeme hapa nchini lakini imekuwa kinyume chake kabisa.

Nilisikia kuna watoto walifariki waliokuwa ndani vyumba vya incubator katika hospitali moja hapa nchini baada ya umeme kukatika na hao watoto njiti ndiyo walikuwa wanategemea kuishi kwa huo umeme kwa joto na hewa ya oxygen.

TANESCO tafadhali jitahidini kutoa huduma kwa uhakika ya umeme kwasababu umeme ndiyo kila kitu hapa duniani.
 
Kigogo Kati (eneo Maarufu Kama Landa Bar) Umeme umekuwa ukikatika almost daily, tena bila taarifa za awali. Tatizo ni nini au kwa vile ni uswahilini? Mbona maeneo ya Masaki na Oysterbay dosari hiyo ni Kama haipo?
 
Ni miezi miwili sasa umeme umekuwa ukikatika kila wakati kwa maeneo na mikoa taofauti na mbaya zaidi nyakati za usiku sana unakuta umeme umekatika huku tukijua kuwa umeme nao ni sehemu ya ulinzi kwa baadhi ya mitaa kwa hapa Dar es salaam.

Na shirika hili la umeme limekuwa kimya kabisa hasa baada ya Prof Muhongo kuondolewa katika nafasi ya uwaziri wa Nishati na Madini kuhusu masula ya umeme kukatika katika na hata maendeleo ya kusambaza umeme kupitia upatikanaji wa gesi ya Mtwara.

Pamoja na kuwa na Gesi ya Mtwara ambayo tuliamini ndiyo mkombozi wa umeme hapa nchini lakini imekuwa kinyume chake kabisa.

Nilisikia kuna watoto walifariki waliokuwa ndani vyumba vya incubator katika hospitali moja hapa nchini baada ya umeme kukatika na hao watoto njiti ndiyo walikuwa wanategemea kuishi kwa huo umeme kwa joto na hewa ya oxygen.

TANESCO tafadhali jitahidini kutoa huduma kwa uhakika ya umeme kwasababu umeme ndiyo kila kitu hapa duniani.
Mwanzo walituona vilaza hatujui umeme wakidhani wao tu wamesomea walidai vikombe vilijaa udongo uliosababisha uzito baada ya kulowa na mvua!

Hivyo wanavodai vikombe haviwezi kuhifadhi udongo wala maji jinsi vilivotengenezwa na miaka yote zaidi ya mia tatizo hilo hakuwahi kutokea. Tanesco siku zote hufanya kazi kisiasa, udongo wanaweka mbele.
 
Hii kiu ya viwanda aliyonayo Mh Rais, haiweze kukatwa na kiwango cha umeme tulionao. Nipo huku Kibamba yaani hali ya ukatikaji wa umeme ni ya hali ya juu sana.

Ndani ya masaa 24 yaliyopita Nafikiri ni masaa 3 tu ndo yalikuwa na umeme mengine ni hola.

Kiwanda gani kitahimili na kuweza kujiendesha kibiashara.
Embu TANESCO toeni mkono wa shirika kwa Mh Rais ili njozi ya viwanda iwezekane.
 
Tanesco mnaibiwa umeme na wajaja mtaani, natamani kuwasaidia kuwakamata wezi lkn sioni faida nitakayopata.
 
TANESCO Mungu anawaona
Miezi miwili inakatika sasa kuhamisha nguzo tuu barabara utajayo Magomeni kwenda Sinza
Biashara zote zimesimama kwani umeme ni usiku tuu hakuna cha siku ya kazi wala nikienda
Nachelea mkiambiw as kujenga line ya km 200 inachukua miaka kumi
 
Transfoma imelipuka tangu ijumaa na umeme mpaka sasa hakuna kwenye line ya hii transfoma

Hii transfoma ipo maeneo ya chuo cha teku ,mitaa ya block T jijini Mbeya

upload_2018-3-12_12-11-56.png
 
Tumepokea taarifa kwa ufatiliaji mpendea mteja
Umeme umekatika Malya, Kwimba mkoani Mwanza tangu jana saa tano asubuhi mpaka muda huu hakuna dalili yoyote ya huduma ya umeme kurejea, mnampango gani na wananchi wa eneo hilo?
 
Kama hapa mjini umeme unakatika hivi na mda mrefu kiasi hiki watoto watakula nini sisi tunaotegemea umeme kuendesha shughuri zetu?

Je kama hapa hapa mjini uko hivi uko vijijn itakuwaje ? Mamlaka jitaidin mrudishe umeme
 
Kama hapa mjini umeme unakatika hivi na mda mrefu kiasi hiki watoto watakula nini sisi tunaotegemea umeme kuendesha shughuri zetu?
Je kama hapa hapa mjini uko hivi uko vijijn itakuwaje ?
Mamlaka jitaidin mrudishe umeme
Aisee kila siku wanakata,
 
Back
Top Bottom