TANESCO: na mgomo wa kuzima umeme

SIMBA mtoto

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
204
100
Baada ya wafanyakazi wa Tanesco kuanza kununua umeme kwa bei ya soko, wameanza mgomo usiokwisha. Wanachofanya ni kuzima umeme kwa kisingizio cha kufanya marekebisho, wanatuma mafundi maeneo mbalimbali, kama ni kukata miti wanakata miti michache kisha hutoweka eneo hilo, kama ni kurekebisha waya au nguzo, husimamisha ngazi kwenye nguzo na kuacha mtu mmoja hapo na wengine kutoweka, umeme hurudishwa jioni sana au usiku.

Zamani kila mfanyakazi alikuwa anapata unit 700 za umeme wa bure kila mwezi, zikiisha walikuwa wanauziwa kwa robo ya bei ya soko. Mgomo ni wa kimya kimya wakidai utakuwa endelevu hadi warudishiwe haki yao ya kupata umeme wa bure. Uongozi wa shirika bado upo kimiya kuzungumzia tatizo hili linalotafuna taifa na kuzidi kudidimiza uchumi wa taifa.

Umekurupuka na thread yako. Wafanyakazi wa Tanesco bado wanaendelea kupeta, kilichofanyika kwa wafanyakazi wa Tanseco ni kuendelea kupatiwa units takribani 750 kwa kununua umeme kwa kutoa Shilingi kama 6,500.00 na Shirika linawaongezea fedha kama Sh. 200,000.00
 
Back
Top Bottom