Tanesco kutangaza kiama kwa wadeni na wahujumu ni mbwembwe?

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,541
12,402
Nimesikiliza taarifa ya habari Clouds Fm, Afisa uhusiano wa Tanesco Babra Masoud ametangaza kwamba wote wanaoihujumu Tanesco kwa kuiibia umeme wajisarimishe ndani ya wiki 2 na kwamba kwa wale wenye mademi wakalipe ndani ya muda huo yaani wiki 2 na kwamba kuna sheria ambayo inawaruhusu wao kupiga mnada nyumba ya mteja ikiwa watakuwa wamelimbikiza deni!

Swali:

kama hiyo sheria ilikuwepo nini walichokuwa wanasubiri maana sijawahi kusikia wamemwajibisha hata mteja mmoja hasa wateja sugu zikiwepo taasisi za serikali na mashirika mengine!

My take:

Wanaleta Propaganda na zaidi hakuna kipya chenye mlengo kulikwamua shirika hilo kutoka kwenye dimbwi la tope la utendaji wa mbovu na wa kimazoea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom